USHAURI: Mabasi yaruhusiwe kusafiri usiku

USHAURI: Mabasi yaruhusiwe kusafiri usiku

Chukulia Mfano mtu anatoka Moshi Jumatatu anatumia siku nzima kuja Dar, akifika analala gharama ya Malazi, Jumanne anaenda Kariakoo ananunua mzigo anarudi kulala Jumatano anapanda basi kurudi Alhamisi ndio anakuwepo Moshi .
Wakati Mkenya aliyepo Kisumu au Kisii anashinda Jumatatu akifanya biashara saa Moja usiku anapanda basi Jumanne asubuhi Anaanza shoping Nairobi na Jioni anapanda basi kurudi, Jumatano yupo kwenye biashara Kisumu

Wapi tutakaa tuwakute wakati yeye hapo hana gharama za Lodge wala muda
 
Jambo jema huigwa, bali lile baya utaachiwa mwenyewe. Tangu Tanzania izuie safari za usiku kwa mawazo ya mtu mmoja bila hata utafiti wa mlinganisho wa faida na hasara, hakuna hata nchi moja iliyotuiga. Hii inonyesha kuwa hasara ya uamuzi huu ni kubwa kuliko faida. Baadhi ya faida za kusafiri usiku;

1. Kuongeza muda wa kufanya kazi kwa kufanya kazi mchana na kulala kwenye basi usiku

2. Kupunguza gharama za safari kwa kutumia muda mfupi. Mfano unasafiri usiku, mchana unamaliza shughuli zako halafu usiku unarudi. Kwa sasa unasafiri mchana, unalala guest house, unafanya mambo yako siku ya pili, unalala tena halafu siku ya tatu ndio unarudi.

3. Hali nzuri ya hewa usiku ambayo haichoshi sana.

4. Ubaridi usiku hupunguza kupasuka matairi hivyo kupunguza ajali

5.Kupunguza msongamano wa magari mchana hivyo kupunguza ajali
Zambia nao wameiga ila huku ni magari yote makubwa hayaruhusiwi kusafiri usiku mwisho SAA 3 usku kuanza safari ni SAA 11 asubuhi usiku ni GARI ndogo tu
 
Ombeni tuu safari za usiku, ila mkitekwa na majambazi msilalamike !!
 
kweli mbona kenya wanasafiri usiku hizo ajali kenua wamedhibiti vp cc tushindwe

Kenya mchana magari aina zote isipokuwa mabasi ya abiria halafu usiku ni mabasi ya abiria tu barabara yote hutaona usiku gari yoyote isipokuwa mabasi ua masafa na kuna wakola huko
 
Hebu tupe na side effects za kusafiri usiku kwa akili za madereva wa kitanzania
 
Kusafiri usiku itasaidia kuzungusha uchumi,kuongeza mzunguko wa fedha utaongezeka.
Sehemu za kuuza chakula atauza chakula mchana na usiku.
Taifa halitalala,itakuwa ni kuchacharika.
Hebu angalia mfano huu: vijijini watu wanalala mapema(mzunguko wa fedha ni mdogo,na fedha ni ngumu kuipata),mijini watu wanachelewa kulala(mzunguko wa fedha ni mkubwa).
Tanzania,tuanze utaratibu huu,ili kukuza uchumi.
Na askari wapangiwe kazi,na walipwe pesa(na wao kipato kitaongezeka)
Kwa kweli kama ni mfanyabiashara unafunguka duka mapema,hautalingana kipato na mfanyabiashara anayefungua duka mpaka usiku.
Hata wenye mabasi watapata mapato mara mbili(mapato kutokana na mabasi yanayosafiri mchana,namapato yatokanayo na safari za usiku).
Kwa vile mipango ni kuchagua,sasa ni wakati KUTAMKA HAYA MABADILIKO ILI KUONGEZA PATO LA TAIFA.
Waziri wa Fedha achukue wazo hili alitumie wakati wa kuwasilisha bajeti 2017/2018
 
Usiku ni hatari sana kwa barabara zetu.
Usalama mdogo,
Ajali zikitokea si rahisi kupata msaada
Majambazi hupendelea usiku kwa uporaji
Madereva huenda mwendo mkali
Madereva wengi husinzia
 
Usiku ni hatari sana kwa barabara zetu.
Usalama mdogo,
Ajali zikitokea si rahisi kupata msaada
Majambazi hupendelea usiku kwa uporaji
Madereva huenda mwendo mkali
Madereva wengi husinzia
Tanzania ni hatari usiku kuliko Zambia, Kenya au Uganda
 
Faida ya kuwepo na barabara za lami nchi nzima iko wapi. Kama kutoka Mwanza to Dar. Inamchukua mtu siku mbili.
Lami ya nini hapo.
 
Jambo jema huigwa, bali lile baya utaachiwa mwenyewe. Tangu Tanzania izuie safari za usiku kwa mawazo ya mtu mmoja bila hata utafiti wa mlinganisho wa faida na hasara, hakuna hata nchi moja iliyotuiga. Hii inonyesha kuwa hasara ya uamuzi huu ni kubwa kuliko faida. Baadhi ya faida za kusafiri usiku;

1. Kuongeza muda wa kufanya kazi kwa kufanya kazi mchana na kulala kwenye basi usiku

2. Kupunguza gharama za safari kwa kutumia muda mfupi. Mfano unasafiri usiku, mchana unamaliza shughuli zako halafu usiku unarudi. Kwa sasa unasafiri mchana, unalala guest house, unafanya mambo yako siku ya pili, unalala tena halafu siku ya tatu ndio unarudi.

3. Hali nzuri ya hewa usiku ambayo haichoshi sana.

4. Ubaridi usiku hupunguza kupasuka matairi hivyo kupunguza ajali

5.Kupunguza msongamano wa magari mchana hivyo kupunguza ajali
Hilo nalipinga kwa nguvu zote mpaka hapo hali ya usalama wa barabarani na Huduma za usiku itakapokuwa safi.

Kwa sasa hapana.Usiku tutaleta maafa makubwa.
 
Enzi za Nyerere tulikuwa tunasafiri usiku iliwezekana tu
Enzi za Mwl na sasa ni tofauti kabisa huwezi kulinganisha.

Barabara za lami enzi za Mwl lilikuwa za kuhesabu kwa hiyo mwendo ulikuwa mdogo.

Usalama ulikuwa mkubwa sana silaha hazikuzagaa mtaani kama sasa.

Magari yalikuwa machache sana.

Wasafiri nao walikuwa wachache.
 
Hakuna taifa litakalokuza uchumi wake kwa speed kwa ku operate day time pekee tu.
 
Hakuna taifa litakalokuza uchumi wake kwa speed kwa ku operate day time pekee tu.
Nakumbuka enzi za Mabasi za zainabu tulikuwa tunatoka Iringa saa moja jioni tunaingia Dar alfajiri asubuhi unaqahi mishe mishe jioni unapanda gari pale mnazi mmoja kesho ya asubuhi unapanga mzigo biashara anaendelea hakuna hela ya kulala logde hapo. Ilikuwa safi.
 
Naunga Mkono ushauri, lakini magendo ya Madawa ya kulevya yatapita kirahisi sana
 
Back
Top Bottom