Jambo jema huigwa, bali lile baya utaachiwa mwenyewe. Tangu Tanzania izuie safari za usiku kwa mawazo ya mtu mmoja bila hata utafiti wa mlinganisho wa faida na hasara, hakuna hata nchi moja iliyotuiga. Hii inonyesha kuwa hasara ya uamuzi huu ni kubwa kuliko faida. Baadhi ya faida za kusafiri usiku;
1. Kuongeza muda wa kufanya kazi kwa kufanya kazi mchana na kulala kwenye basi usiku
2. Kupunguza gharama za safari kwa kutumia muda mfupi. Mfano unasafiri usiku, mchana unamaliza shughuli zako halafu usiku unarudi. Kwa sasa unasafiri mchana, unalala guest house, unafanya mambo yako siku ya pili, unalala tena halafu siku ya tatu ndio unarudi.
3. Hali nzuri ya hewa usiku ambayo haichoshi sana.
4. Ubaridi usiku hupunguza kupasuka matairi hivyo kupunguza ajali
5.Kupunguza msongamano wa magari mchana hivyo kupunguza ajali