Ushauri kwa waziri wa mambo ya ndani ,Msongamano mahabusu na wafungwa

KIRUA

Senior Member
Feb 6, 2012
131
40
Ndg Mh waziri Charles Kitwanga suluhisho la tatizo la msongamani na gharama kubwa kwa magereza yetu upo wazi ,Pale wizarani kuna kitengo cha Probasheni na Huduma kwa jamii wanao deal na wafungwa wa nje,kurekebisha tabia na after care service hawa watu wanatosha kabisa kuwa mbadala na suluhisho la tatizo hili either kwa wafungwa na mahabusu.
kinacho takiwa nikuwapa maafisa na watumishi nguvu ya kisheria ya kufanya kazi hizi bila kuingiliwa na MTU mwengine.Mfano sheria ya Huduma kwa jamii na.6 ya 2002 haimpi afisa nguvu ya kufanya maamuzi juu ya mfungwa kutumikia adhabu yake nje ya gereza bila hakimu kujiridhisha ,ili hali afisa husika amefanya uchunguzi na kuona anafaa kufanya hivyo!Hii inaongeza garama kwa serikali kwani hugharamikia uchunguzi husika na kukataliwa na mahakimu kwa sababu zao au kutaka kitu kodogo kutoka kwa mfungwa!
sheria hii iliwekwa kwa nia nzuri ya kupunguza gharama na msongamano lakini inakabiliwa na changamoto kubwa kutoka kwa watendaji na pia Penal Code yetu kwani haina mbadala wa hukumu ya kifungo cha nje!
chamsingi fuatilia kitengo hiki kina kila suluhisho la tatizo hili!
asante!
naomba mwenye kujua zaidi juu ya sheria za vifungo vya nje atufafanulie zaidi!
 
Nadhani wakipatikana wafungwa 30 kwa mwezi ,wenye vifungo visivyo zaidi miezi 12 ,wapewe kazi ya kusafisha miji
 
Nadhani wakipatikana wafungwa 30 kwa mwezi ,wenye vifungo visivyo zaidi miezi 12 ,wapewe kazi ya kusafisha miji

kweli kabisa kila mkoa inatoa 30 kwa mwezi itapunguza sana na sheria inataka wafungwa wa miaka mitatu!Nandiyo wengi magereza!
 
Back
Top Bottom