Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,093
- 11,716
Nimesoma mahali kuwa Makamu wa Rais ameshauri Magereza yaachane na matumizi ya ndoo kama sehemu ya kujisaidia wafungwa.
Ni jambo jema ikiwa litafanikiwa lakini tatizo ni kubwa zaidi ya hilo.
Tatizo kubwa ni kuwa mtazamo wetu kuhusu waliokuwa kwenye magereza haujabadilika toka wakati wa ukoloni. Magereza yanachukuliwa kama sehemu ya kumdhalilisha anayehifadhiwa sehemu ile. Udhalilishaji huo uko hivi:
1. Nguo anazovaa. Ni mithili ya za mtoto mchanga.
2. Kumtaka mfungwa achuchumae anapoongea na afisa magereza. Hamna sababu ya kufanya hivi bali ya kutaka kumuonyesha kuwa yeye ni mtwana.
3. Muda wa kula na kulala usioendana na hali halisi.
4. Aina ya chakula anacholishwa.
5. Kunyimwa sehemu ya kulala kwa staha. Vigodoro na viblanketi vinavyotumika sio rafiki.
6. Kuwajaza kupita kiasi katika chumba kimoja.
7. Kukosa sehemu za kujisaidia na kuoga kwa faraga. Kuweka miundo mbinu nzuri kwa ajili ya hiyo katika magereza yaliyojengwa wakati wa ukoloni sio rahisi. Utawekaje choo cha shimo au kinachotumia maji katika bwalo linalotumika kama chumba?
Matatizo ni makubwa mno na kwa kweli hakuna msukumo kutoka kwa wananchi kuhusu suala hili. Ndio maana watu wanafurahi kuwaambia wenzao kuwa waende kunyea debe!
Kunahitaji political will ya kufumua mfumo mzima wa magereza na mtazamo wetu dhidi ya mfungwa.
Ni tamko jema lakini sidhani kama litaleta mabadiliko yeyote.
Amandla...
Mag3 JokaKuu Nyani Ngabu