Ushauri kwa Waziri wa fedha: Serikali inapoteza zaidi ya bilioni 200 kila mwaka kwa kupotezea chanzo hiki cha kodi

lakini mkumbuke sikuzote anayelipa kodi ni mlaji, wenye nyumba watapandisha ili kufidia halafu mtalalamika tena bei za nyumba zimepanda.
 
Nyumba zinazofanya biashara zinalipa kodi kupitia mikataba ya wafanyabiashara husika waliopanga kwenye nyumba hizo
 
Kwa muda mrefu Serikali imeshindwa kusimamia kwa ukamilifu ukusanyaji wa kodi katika majengo ya kibiashara. Kuna nyumba nyingi sana mijini na vijijini zinafanya biashara ya upangishaji ila hazilipi kodi kutokana na kipato inachoingiza. kwa hesabu za haraka bei ya nyumba za kujitegemea za kupanga mijini ni kuanzia sh. 150,000 hadi 400,000 kwa mwezi kwa nyumba za kawaida na hizi ndio nyingi, ingawa zipo nyumba zinaenda hadi sh. 6,000,000 kwa mwezi.Nyumba nyingine zinapangishwa kwa vyumba, chumba kimoja sh. 20,000 hadi 50,000 kwa mwezi na unakuta nyumba moja inavyumba kama 4 hadi 10+. Kuna vyumba vya biashara bei yake ni sh. 50,000 hadi 500,000 kwa mwezi.

Nashauri yafuatayo:

1. Serikali iachane na ukusanyaji wa hizi kodi kwa mfumo wa withholding tax

2. Kila nyumba ilipe kodi ya 10% kama inavyotozwa kwenye withholding tax

3. Serikali ibadirishe sheria ya ukusanyaji kodi, kuwa biashara zenye mauzo chini y ash. 4,000,000 zisilipe kodi, nyumba za biashara ziondolewe kwenye hii sheria

4. Kila nyumba inayofanya biashara ya kupangisha ipewe TIN

5. TRA iongezewe nguvu ya ukusanyaji wa hizi kodi
Jambo hilo haliwezi kupita, baba na mama wenye nyumba wengi ni watumishi wa umma na watunga sera, lingekuwa linatuhusu akina chakubanga peke yetu tungekuwa tulisha anza kusulubiwa.
 
Kwa magufuli akilivalia njuga naamini wote tutaisoma namba kwa pamoja

PunguzaJazba
Kodi hailipwi na mwenye nyumba wewe nyumbu kumbuka kamwisho wa siku anayemlipa ni mpangaji kwa hiyo ukiongeza kodi unafikiri atalipa mwenye nyumba au mfanyabiashara? Tatizo ni Elimu kodi it’s very simple widen the tax base and lower the rate you attain voluntary compliance! Hawa washauri wanaotoka shamba ni matatizo! Kodi kwenye mazao hulipwa na anayekula tonge la mwisho wafanyabiashara na madalali in the value chain are just mawakala wa kodi tu! Hakuna mfanyabiashara anayetoa fedha mfukoni kwake kulipa kodi it’s just a pass through cost hao masikini unaotaka kuwalipia Elimu watalipia through the back door! Endeleeni kujifanya na kucheka pamoja ni kujidanganya big time ndio shida ya kuwapa washamba madaraka!
 
Nyumba za kupanga ni huduma, tena basic needs. Ndo maana majengo ya kibiashara yanalipwa 10% with holding tax na yale ya makazi hayalipi chochote. Kwenye mfumo wa kodi, unapo ontroduce kodi fulani anayelipa ni mlaji wa mwisho si mfanya biashara. Mfanyabiashara ana i pass kwa final consumer. So mwisho wasiku nyie mnao panga ndo mtakao athirika.
 
kodi ya ardhi ni kidogo sana ukilinganisha na gharama za upangaji
Unataka mtu alipe kodi wakati jengo linalipa huduma za maji umeme na mengineyo....na huyo mpangaji ushamkata payee na bado unamkata kodi ya ardhi....fikiri mara 2 kabla ya kuja na hoja za kishuleshule.
 
Kwa muda mrefu Serikali imeshindwa kusimamia kwa ukamilifu ukusanyaji wa kodi katika majengo ya kibiashara. Kuna nyumba nyingi sana mijini na vijijini zinafanya biashara ya upangishaji ila hazilipi kodi kutokana na kipato inachoingiza. kwa hesabu za haraka bei ya nyumba za kujitegemea za kupanga mijini ni kuanzia sh. 150,000 hadi 400,000 kwa mwezi kwa nyumba za kawaida na hizi ndio nyingi, ingawa zipo nyumba zinaenda hadi sh. 6,000,000 kwa mwezi.Nyumba nyingine zinapangishwa kwa vyumba, chumba kimoja sh. 20,000 hadi 50,000 kwa mwezi na unakuta nyumba moja inavyumba kama 4 hadi 10+. Kuna vyumba vya biashara bei yake ni sh. 50,000 hadi 500,000 kwa mwezi.

Nashauri yafuatayo:

1. Serikali iachane na ukusanyaji wa hizi kodi kwa mfumo wa withholding tax

2. Kila nyumba ilipe kodi ya 10% kama inavyotozwa kwenye withholding tax

3. Serikali ibadirishe sheria ya ukusanyaji kodi, kuwa biashara zenye mauzo chini y ash. 4,000,000 zisilipe kodi, nyumba za biashara ziondolewe kwenye hii sheria

4. Kila nyumba inayofanya biashara ya kupangisha ipewe TIN

5. TRA iongezewe nguvu ya ukusanyaji wa hizi kodi
Zile nyumbu zilishabikia sana hili swala early 2016, sielewi labda boss wao alizifunga break au ziligundua zipo OP
 
Hahaha mimi hata sikubaliani na makodi yenu hayo wakati matumizi ya pesa hizo hayanisaidii mimi mwananchi. Tizama viongozi serikalini hadi leo wengi wanakaa nyumba za bure, magari na mafuta bure, umeme na maji hawalipi na wanalipiwa gharama na serikali kutoka kwenye pesa zetu za kodi. Hawa viongozi wanaolipiwa wote wana nyumba zao, pia wana magari yao, kwanini waendelee kutumia pesa zetu hovyo na mishahara wanalipwa tena minono kuliko yetu?!
Mnazidi kuwaongezea mapato wataanza kuongoza kutokea dubai. Barabara zetu zinajengwa kwa mikopo, utasikia WB, au BA wamekubali kutokopesha tunajenga flyover ya madale na blabla kama hizo halafu kodi zetu wanajilipa mipesa miingi. Hospitali tabu tupu, wao kimya kimya Agha Khan au nje utadhani wanatumia pesa zao. Hatutaki kodi zaidi hizo zinawatosha.
Hata mgeanzisha kodi ya idadi ya nywele zetu, lakini zituike sahihi. Sasa mnaanza kunyemelea vibanda vyetu. Acheni ubinafsi nchi hii yetu sote nasi tunahitaji kufaidi nchini humu japo kidogo.
Kodi kodi utadhani mi vampire na damu duh aaagrh mna kera sana. Yani kila kitu mali yenu mmekuwa miungu?! Ebo, mnataka hata tusipumue?! Nyie vipi?!
 
Kwa muda mrefu Serikali imeshindwa kusimamia kwa ukamilifu ukusanyaji wa kodi katika majengo ya kibiashara. Kuna nyumba nyingi sana mijini na vijijini zinafanya biashara ya upangishaji ila hazilipi kodi kutokana na kipato inachoingiza. kwa hesabu za haraka bei ya nyumba za kujitegemea za kupanga mijini ni kuanzia sh. 150,000 hadi 400,000 kwa mwezi kwa nyumba za kawaida na hizi ndio nyingi, ingawa zipo nyumba zinaenda hadi sh. 6,000,000 kwa mwezi.Nyumba nyingine zinapangishwa kwa vyumba, chumba kimoja sh. 20,000 hadi 50,000 kwa mwezi na unakuta nyumba moja inavyumba kama 4 hadi 10+. Kuna vyumba vya biashara bei yake ni sh. 50,000 hadi 500,000 kwa mwezi.

Nashauri yafuatayo:

1. Serikali iachane na ukusanyaji wa hizi kodi kwa mfumo wa withholding tax

2. Kila nyumba ilipe kodi ya 10% kama inavyotozwa kwenye withholding tax

3. Serikali ibadirishe sheria ya ukusanyaji kodi, kuwa biashara zenye mauzo chini y ash. 4,000,000 zisilipe kodi, nyumba za biashara ziondolewe kwenye hii sheria

4. Kila nyumba inayofanya biashara ya kupangisha ipewe TIN

5. TRA iongezewe nguvu ya ukusanyaji wa hizi kodi

Mtihani sana. Kuna mtu wangu wa karibu anafanyabiashara mtaa wa Congo Kariakoo. Analipa pango la nyuma kasehemu kadogo tu cha upana wa mita moja na nusu anapangishwa kwa Tshs 500,000. Nilipomuuliza je mpangaji analipa kodi katika pesa ya pangi unayomlipa? Jibu likwa ndio lakini tunashusha hadi Tshs 150,000 badala ya Tshs 500,000 kwa mwezi. Nilipomuuliza kwanini unampunguzia, akaniambia kuwa akikatwa kodi kutokana na pango la Tshs 500,00 ninayomlipa, mimi pia TRA wataikadiria biashara yangu nilipe kodi ya juu inayolingana na kipato ninachopata kinachoweza kulipa pango la Tshs 500,000 kwa mwezi. Kwahiyo hili suala linahitaji usimamizi na uchubguzi wa hali ya juu sana. Believe me, Kariakoo tu peke yake kama TRA ikisimamia vizuri kwa ufanisu Mkubwa kutokana na data nilizopewa na rafiki yangu anayefanyakazi TRA kitengo cha quality system auditing anakili kuwa mapata yanayoweza kupatikana pale pekee yake yanazidi mikoa mitani ya kusini akaenda mbal kwakusema hata TRA wakiamua kufunga ofisi zao zote za hiyo mikoa mitano na walete wale wafanyakazi waje Kariokoo Serikali itapata zaidi.
 
Tatizo huwajui wamiliki au unajisahaurisha kwa makusudi!?

Jiulize, ni kwa nini nyumba zingine zinabomolewa zingine hazibomolewi!?
Mfano, zilizo kwenye fukwe za bahari au hifadhi za barabarani!?

Kwa nini, mashamba ya wengine yasiyoendelezwa yalichukuliwa tena kwa/mbwembwe na matarumbeta wakati baadhi ya watu mashamba yao hayakuchukuliwa na hadi leo hajaendelezwa!?

Kazi njema mkuu.
Hivi kwa nini watu wanapenda kujikatisha tamaa kabla hata hawajajaribu

Huu ushauri ni mzuri sana. Ndio, kuna vigogo wenye nyumba za kupagisha na wanaweza kujaribu kukwepa kulipa kodi lakini nionavyo mimi hao ni wachache sana.

Pia, huu mkondo wa kodi ukienea sehemu zote basi wanaokwepa kulipa hii kodi wataumbuliwa na majirani zao.

Huu mfumo uanzishwe halafu tutawashughulikia wale wajanja fulani wanaotaka kukwepa. Kama inavyofanywa sasa kwa biashara kutumia mashine za kulipa kodi.

Tusikatishe tamaa mawazo mazuri eti kwa sababu kuna wajanja watakwepa.
 
wafanyakazi wa TRA wale mabosi ndio wamiliki wa hizo nyumba nyingi wanaanzia wapi kuweka utaratibu utakaowabana..

unajua mawaziri, makatibu wakuu, wakurugenzi ndio wamiliki wa nyumba nyingi za kupanga... so hili jambo kufanikisha ni ngumu kuliko unavyofikiri
Hii haitawaathiri wenye nyumba. Kama anataka kodi ya 50,000 au juu basi atapangisha kwa 60,000.

Atalipa kodi ya TRA ya 10% (au 6,000) na yeye atabaki na 54,000.

Kwa hiyo, kama ilivyo kwenye biashara nyingine, mlipaji kodi ya TRA ni mlaji. Bei zote zinahakikisha kuwa, baada ya TRA kuchukua chao, mfanyabiashara atapata faida yake ileile.

Na kama kutakuwa na sheria ya serikali kumnyang'anya mtu nyumba yake na kuipiga mnada kama atakwepa kulipa kodi ya TRA, hakuna mwenye nyumba atakaethubutu kukwepa kodi ya TRA ya 10%.
 
D
Mtihani sana. Kuna mtu wangu wa karibu anafanyabiashara mtaa wa Congo Kariakoo. Analipa pango la nyuma kasehemu kadogo tu cha upana wa mita moja na nusu anapangishwa kwa Tshs 500,000. Nilipomuuliza je mpangaji analipa kodi katika pesa ya pangi unayomlipa? Jibu likwa ndio lakini tunashusha hadi Tshs 150,000 badala ya Tshs 500,000 kwa mwezi. Nilipomuuliza kwanini unampunguzia, akaniambia kuwa akikatwa kodi kutokana na pango la Tshs 500,00 ninayomlipa, mimi pia TRA wataikadiria biashara yangu nilipe kodi ya juu inayolingana na kipato ninachopata kinachoweza kulipa pango la Tshs 500,000 kwa mwezi. Kwahiyo hili suala linahitaji usimamizi na uchubguzi wa hali ya juu sana. Believe me, Kariakoo tu peke yake kama TRA ikisimamia vizuri kwa ufanisu Mkubwa kutokana na data nilizopewa na rafiki yangu anayefanyakazi TRA kitengo cha quality system auditing anakili kuwa mapata yanayoweza kupatikana pale pekee yake yanazidi mikoa mitani ya kusini akaenda mbal kwakusema hata TRA wakiamua kufunga ofisi zao zote za hiyo mikoa mitano na walete wale wafanyakazi waje Kariokoo Serikali itapata zaidi.
Kweli kabisa
 
Nipo hapa kariakoo. Kuna hotel nimelala presidential suite kwa 25,000 tu. Narudia nimelala kwa elfu 25 tu na inawezekana kwa siku ya leo haina wateja zaid ya 5 wakat inavyumba zaid ya 50.

Jaman hali ni mbya. Hii hotel ni mpya na alyeijenga amejenga kama apartment ila naona kakosa wateja kaamua kuifanya hotel.
 
Back
Top Bottom