Mtini
JF-Expert Member
- Apr 28, 2011
- 1,487
- 2,344
Kwa muda mrefu Serikali imeshindwa kusimamia kwa ukamilifu ukusanyaji wa kodi katika majengo ya kibiashara. Kuna nyumba nyingi sana mijini na vijijini zinafanya biashara ya upangishaji ila hazilipi kodi kutokana na kipato inachoingiza. kwa hesabu za haraka bei ya nyumba za kujitegemea za kupanga mijini ni kuanzia sh. 150,000 hadi 400,000 kwa mwezi kwa nyumba za kawaida na hizi ndio nyingi, ingawa zipo nyumba zinaenda hadi sh. 6,000,000 kwa mwezi.Nyumba nyingine zinapangishwa kwa vyumba, chumba kimoja sh. 20,000 hadi 50,000 kwa mwezi na unakuta nyumba moja inavyumba kama 4 hadi 10+. Kuna vyumba vya biashara bei yake ni sh. 50,000 hadi 500,000 kwa mwezi.
Nashauri yafuatayo:
1. Serikali iachane na ukusanyaji wa hizi kodi kwa mfumo wa withholding tax
2. Kila nyumba ilipe kodi ya 10% kama inavyotozwa kwenye withholding tax
3. Serikali ibadirishe sheria ya ukusanyaji kodi, kuwa biashara zenye mauzo chini y ash. 4,000,000 zisilipe kodi, nyumba za biashara ziondolewe kwenye hii sheria
4. Kila nyumba inayofanya biashara ya kupangisha ipewe TIN
5. TRA iongezewe nguvu ya ukusanyaji wa hizi kodi