Relief Mirzska
JF-Expert Member
- Jun 13, 2017
- 13,988
- 22,379
Salaam wajameni, hope mmemaliza siku salama na ilikuwa ni siku ya mafanikio.
Wiki kadhaa zilizopita mimi na mke wangu tulipata likizo ila yangu ilikuwa ni wiki mbili na yake ni ya mwezi mzima. Hao tukaamua tuelekee Tanga tukawasalimu wazee.
Mke wangu anapendwa sana na wazee wangu kwani ana tabia njema sana, tulipofika bi mkubwa akaniambia kwa kuwa mwenzio ana likizo ndefu na ni mjamzito (mimba yake ya kwanza) ukiondoka muache aendelee kubaki hapa mainly for two reasons:- (i) nataka nikae nae nione hivi ukiwa wewe hupo tabia zake ni zipi? (ii) apumzike maana mimba inamsumbua kidogo.
Mimi nikakubali kwa roho safi, pia nikaona huu ndio uchochoro angalau nionane na washkaji zangu ambao hatujaonana kitambo (wakubwa mshanielewa) maana mke wangu tukiwa nyumbani hataki hata nichati na "marafiki" zangu.
Aisee likizo imeisha nimerudi nyumbani peke yangu kila kitu sikioni kuwa sawa. Nakula mi chipsi tu, nakula mi-mikate tu, mivyakula ya migahawani mibaya ajabu. Kitanda changu hata sikipendi kudaadeki, nyumba naiona kubwa balaa, siku mbili mivyombo michafu noma.
Nimemaliza suruali zote mpaka leo nikawa nafikiria nikifika mjini ninunune japo jeans moja. Yaani wadau balaa juu ya balaa. Jiko la gesi limejaa mifuta ya kupikia iliyomwagika wakati nakaanga samaki, fridge halipendezi kama akiwepo mwenyewe. Hicho choo yaani you can see the difference.
Nimempigia simu arudi kesho ndege kutoka Tanga kuja huku kesho tumekosa nafasi, may be Ijumaa atarudi lakini nimeshika adabu yangu na huu mchezo siurudii tena.
Wanaume wenzangu: Mwanamke ndio nyumba, tuwaheshimu hawa watu japo nawajua pasua kichwa hawa ila mwanamke ndio mpango mzima ndani ya nyumba.
Big up wanawake wote respect kwenu aisee.....