Ushauri kwa wanaume wenzangu: Mke ndio kila kitu ndani ya nyumba

Kuna kwaya moja huko Kigoma waliimba "Mke mwema nani atakayemwona, maana ni mali adimu mke mwema yu wapi"...... Huwa natamani sana nije kupata wife material, nahisi nitaishi kama nipo peponi hata kama nitakuwa sina kitu. Tatizo wanawake wa siku hizi ni kama mabasi ya mwendokasi!

HONGERA SANA MKUU KWA KUMPATA MKE MWEMA, hiyo ni mali adimu kabisa karne hii...
 
I know man! and ain't gonna fight against it....
Its reality, has been said in Qur an as well.....
respect to you mentor......
Ila naamini waweza kujizuia.

Ukishindwa fuata dini yako inavyokuelekeza mkuu.

"Kila aziniye na mwanamke hana akili kabisa, tena aiangamiza nafsi yake mwenyewe." Alisema hayo mfalme Daudi. Unajua alichokifanya kwa mke wa askari wake baada ya kumuonja? Alimuua mumewe. Tendo hilo la dakika kadhaa lilikuwa karibu kuangamiza mema yote aliyokwisha kuyafanya.

Najua ni tendo la muda mfupi ila ni tendo pendwa lakini unapolifanya na mtu asiye sahihi, linakuangamiza kiuchumi (wazijua gharama za uchepukaji hasa ukiwa wa kiume), athari za kijamii (kila binti mzuri utayemuona badala ya kuwa na mazungumzo ya kujenga utawaza jinsi ya kumvua chupi), kiimani nk nk nk. Athari zake ni nyingi kuliko faida ya dakika tano uipatayo.

"...tena aiangamiza nafsi yake mwenyewe."

**Si rahisi, ila inawezekana.
 
Kuna kwaya moja huko Kigoma waliimba "Mke mwema nani atakayemwona, maana ni mali adimu mke mwema yu wapi"...... Huwa natamani sana nije kupata wife material, nahisi nitaishi kama nipo peponi hata kama nitakuwa sina kitu. Tatizo wanawake wa siku hizi ni kama mabasi ya mwendokasi!

HONGERA SANA MKUU KWA KUMPATA MKE MWEMA, hiyo ni mali adimu kabisa karne hii...
Ahsante sana mkuu! tatizo humu ukisema kitu wadau wanasema unapenda sifa, sijui unajifanya una pesa, ila ukweli unabaki kuwa ukweli tu. Namshkuru mungu mke wangu ni mtu mwema sana. na kila siku nagundua hilo. Tangu ni girlfriend wangu tupo chuo hakuwahi kunidharau au kunifanya nijiskie vibaya kwa kuwa nlikuwa sina kitu, na Fernando amini usiamini mimi nlikuwa sina kitu haswa yaani. nlikuwa kapuku kinoma chuo mwaka wa kwanza, nakaa na njaa hadi nahisi mungu kanionea. Na huyu mke wangu alinipenda hivyo hivyo, leo nimepata cha mboga ukisema watu wanasema unajisifia. Kudaadeki acha nijisife ndio nina gari, nina mke mzuri, nina uwezo wa kwenda holiday nje ya nchi.
 
Ila naamini waweza kujizuia.

Ukishindwa fuata dini yako inavyokuelekeza mkuu.

"Kila aziniye na mwanamke hana akili kabisa, tena aiangamiza nafsi yake mwenyewe." Alisema hayo mfalme Daudi. Unajua alichokifanya kwa mke wa askari wake baada ya kumuonja? Alimuua mumewe. Tendo hilo la dakika kadhaa lilikuwa karibu kuangamiza mema yote aliyokwisha kuyafanya.

Najua ni tendo la muda mfupi ila ni tendo pendwa lakini unapolifanya na mtu asiye sahihi, linakuangamiza kiuchumi (wazijua gharama za uchepukaji hasa ukiwa wa kiume), athari za kijamii (kila binti mzuri utayemuona badala ya kuwa na mazungumzo ya kujenga utawaza jinsi ya kumvua chupi), kiimani nk nk nk. Athari zake ni nyingi kuliko faida ya dakika tano uipatayo.

"...tena aiangamiza nafsi yake mwenyewe."

**Si rahisi, ila inawezekana.
Nakukubali sana broo. Na trudst me nayajua yote hayo, kabisa kabisa. Ila duh..... acha nsiseme sana broo.
 
Salaam wajameni, hope mumemaliza siku salama na ilikuwa ni siku ya mafanikio.

Wiki kadhaa zilizopita mimi na wife tulipata likizo ila yangu ilikuwa ni wiki mbili na yake ni ya mwezi mzima. Hao tukaamua tuelekee Tanga tukawasalimu wazee.......
Mke wangu anapendwa sana na wazee wangu kwani ana tabia njema sana, tulipofika bi mkubwa akaniambia kwa kuwa mwenzio ana likizo ndefu na ni mjamzito (mimba yake ya kwanza) ukiondoka muache aendelee kubaki hapa mainly for two reasons:- (i) nataka nikae nae nione hivi ukiwa wewe hupo tabia zake ni zipi? (ii) apumzike maana mimba inamsumbua kidogo.

Me nkakubali kwa roho safi, pia nkaona huu ndio uchochoro angalau nionane na washkaji zangu ambao hatujaonana kitambo (wakubwa mshanielewa) maana wife tukiwa home hataki hata nichati na "marafiki" zangu.

Aisee likizo imeisha nimerudi ghetto alone kila kitu sikioni kuwa sawa. Nakula mi chipsi tu, nakula mi-mikate tu, mivyakula ya migahawani mibaya ajabu. kitanda changu hata sikipendi kudaadeki, nyumba naiona kubwa balaa, siku mbili mivyombo michafu noma. Nimemaliza suruali zote mpaka leo nkawa nafikiria nkifika town ninunune japo jeans moja. Yaani wadau balaa juu ya balaa. Jiko la gesi limejaa mifuta ya kupikia iliyomwagika wakati nakaanga samaki, fridge halipendezi kama akiwepo mwenyewe. Hicho choo yaani you can see the difference.

Nimempigia simu arudi kesho ndege kutoka Tanga kuja huku kesho tumekosa nafasi, may be ijumaa atarudi lakini nimeshika adabu yangu na huu mchezo siurudii tena.

Wanaume wenzangu: Mwanamke ndio nyumba, tuwaheshimu hawa watu japo nawajua pasua kichwa hawa ila mwanamke ndio mpango mzima ndani ya nyumba.

Big up wanawake wote respect kwenu aisee.....
Kuna kitu nimekinote kwako mkuu ambacho si cha kawaida kwetu wanaume... inaelekea maisha yako yote ulikaa na wazazi mara paap ukaoa... hujawai kuishi peke yako...pia it seems siku mkikorofishana ama akiugu utalia kama mtoto mdogo.. jifunze sana kuishi mwenyewe bila kutegemea mtu nakuhakikishia utakuwa na amani siku zote.. Halafu mkuu mwanaume aelezei kila kitu ndani mwake hivyo hayo ni mambo ya kawaida sana uliktakiwa tu kuweka kwa kifupi kwamba kila kitu ndani hovyo.... na hata hilo la ndege duuuh kwa misifa hujambo tetetetteeehh
 
We jamaa unaonekana ni mchafu sana, na mkeo anavumilia mengi sana juu ya uchafu wako.
Aiseee mwanangu ukinifananisha na wadau mimi si mchafu sana. Sometimes narudi kwa mungu wangu na kujiuliza hivi neema zote hizi ambazo mungu wangu amenipa halafu bado nashindwa kumshkuru kwa kuacha aliyonikataza huwa nalia. Huwa najuta, na mara zote broo wazungu wakitoka tu majuto yanakuja, nisiseme sana aiseeee.......
"we are who we are"
 
Kuna kitu nimekinote kwako mkuu ambacho si cha kawaida kwetu wanaume... inaelekea maisha yako yote ulikaa na wazazi mara paap ukaoa... hujawai kuishi peke yako...pia it seems siku mkikorofishana ama akiugu utalia kama mtoto mdogo.. jifunze sana kuishi mwenyewe bila kutegemea mtu nakuhakikishia utakuwa na amani siku zote.. Halafu mkuu mwanaume aelezei kila kitu ndani mwake hivyo hayo ni mambo ya kawaida sana uliktakiwa tu kuweka kwa kifupi kwamba kila kitu ndani hovyo.... na hata hilo la ndege duuuh kwa misifa hujambo tetetetteeehh
Thanks kwa ushauri Mago! ila sio kweli kwamba maisha yote nlikaa na wazazi, nlikaa na wazee darasa la kwanza mpaka la sita, nkawa nasumbua kinoma nkapelekwa mbali sana na bi mkubwa. Nlipomaliza darasa la saba nkarudi kukaa na bi mkubwa kwa miaka minne ya o'level na nlisoma day school. baada ya hapo nkaenda advance nkakaa mbali na wazee halafu nkaenda chuo kanda ya ziwa huko miaka mitatu. Tangu nlipoenda chuo sijakaa na wazee isipokuwa likizo tu maana nliwahi kupata kiajira
 
Back
Top Bottom