Ushauri kwa wanaume wenzangu: Mke ndio kila kitu ndani ya nyumba

Relief Mirzska

JF-Expert Member
Jun 13, 2017
13,962
22,333
Salaam wajameni, hope mmemaliza siku salama na ilikuwa ni siku ya mafanikio.

Wiki kadhaa zilizopita mimi na mke wangu tulipata likizo ila yangu ilikuwa ni wiki mbili na yake ni ya mwezi mzima. Hao tukaamua tuelekee Tanga tukawasalimu wazee.

Mke wangu anapendwa sana na wazee wangu kwani ana tabia njema sana, tulipofika bi mkubwa akaniambia kwa kuwa mwenzio ana likizo ndefu na ni mjamzito (mimba yake ya kwanza) ukiondoka muache aendelee kubaki hapa mainly for two reasons:- (i) nataka nikae nae nione hivi ukiwa wewe hupo tabia zake ni zipi? (ii) apumzike maana mimba inamsumbua kidogo.

Mimi nikakubali kwa roho safi, pia nikaona huu ndio uchochoro angalau nionane na washkaji zangu ambao hatujaonana kitambo (wakubwa mshanielewa) maana mke wangu tukiwa nyumbani hataki hata nichati na "marafiki" zangu.

Aisee likizo imeisha nimerudi nyumbani peke yangu kila kitu sikioni kuwa sawa. Nakula mi chipsi tu, nakula mi-mikate tu, mivyakula ya migahawani mibaya ajabu. Kitanda changu hata sikipendi kudaadeki, nyumba naiona kubwa balaa, siku mbili mivyombo michafu noma.

Nimemaliza suruali zote mpaka leo nikawa nafikiria nikifika mjini ninunune japo jeans moja. Yaani wadau balaa juu ya balaa. Jiko la gesi limejaa mifuta ya kupikia iliyomwagika wakati nakaanga samaki, fridge halipendezi kama akiwepo mwenyewe. Hicho choo yaani you can see the difference.

Nimempigia simu arudi kesho ndege kutoka Tanga kuja huku kesho tumekosa nafasi, may be Ijumaa atarudi lakini nimeshika adabu yangu na huu mchezo siurudii tena.

Wanaume wenzangu: Mwanamke ndio nyumba, tuwaheshimu hawa watu japo nawajua pasua kichwa hawa ila mwanamke ndio mpango mzima ndani ya nyumba.

Big up wanawake wote respect kwenu aisee.....
 
Mpende sana mkeo na mimi nikipata mke nitampenda sana
Usijali mwanangu, hilo ndio somo kuu kwangu. Nampenda sana wife na hata hawa wadada humu ninaowatokea wasidhani kwamba kuna chembe ya upendo itahama ndani ya moyo wangu kwenda kwao.... No no no no! Wao ni game za ugenini tu, mapenzi haswa kwa maana ya mapenzi ni kwa wife
 
Ila story zenu jaman,kila mtu ana hela humu za ndege,kumiliki gari,ndoa zenye amani,nyumba matawi

Mmh maskin hatuna pa kujidaia
Wala usijali kuhusu hizo numbisa, chukua cha kujifunza majivuno yawache. mimi nimekwenda Tanga na basi tena Tashriff pamoja na yeye. Nimerudi na basi Tawakkal alone yeye nimemuacha home, nimeamua kulipia 135,000 ya flight coz wife ni mjamzito and a not gonna risk and let her travel alone with bus. gari ninalo japo bovu, ndoa yangu inayo amani japo sometimes anakamata vi-sms na kinanuka. Nyumba sina ndio kwanza najenga. nini zaidi rafiki?
 
Hahaaaaaa nimecheka kwa sauti acha kumsaliti shemeji mungu hapendi
Ni kweli mwanangu nalijua hilo lakini hii dunia yetu hii ni balaa kaka. Ukioa utajua, me nlipooa mara ya kwanza namsaliti wife ni baada ya mwaka mmoja na miezi mitatu. nlijikaza sana mwanangu ila usijali mark my word ukioa utakuja ona
 
Ni kweli mwanangu nalijua hilo lakini hii dunia yetu hii ni balaa kaka. Ukioa utajua, me nlipooa mara ya kwanza namsaliti wife ni baada ya mwaka mmoja na miezi mitatu. nlijikaza sana mwanangu ila usijali mark my word ukioa utakuja ona
Sawa boss wangu pamoja wanaume tunapata mitihani mingi ya kimapenzi
 
Kaka Relief Mirzska afadhali umepata kujitathmini lakini mkuu ungemuacha kidogo shem apumzike ni wakati sasa wa wewe walau kuzijua kazi za ndani, ni very interesting. Mimi wife akipata safari kama hizo huwa ninanunua vitabu vya mambo ya mapishi na najaribu kujipikia mwenyewe mkuu, very interesting, wakati mwengine unachanganya mambo unapata msosi harufu ya inye basi unabakia kucheka peke yako tu.
 
Kaka Relief Mirzska afadhali umepata kujitathmini lakini mkuu ungemuacha kidogo shem apumzike ni wakati sasa wa wewe walau kuzijua kazi za ndani, ni very interesting. Mimi wife akipata safari kama hizo huwa ninanunua vitabu vya mambo ya mapishi na najaribu kujipikia mwenyewe mkuu, very interesting, wakati mwengine unachanganya mambo unapata msosi harufu ya inye basi unabakia kucheka peke yako tu.
hahahahahah! harufu ya inye?????? aisee wife afanye arudi maana kutaharibika na naona dalili zote za huku kuharibika. Niombee mungu anistiri
 
Back
Top Bottom