Ushauri kwa wanao ingia kwenye mahusiano

Ushauri kwa wanao ingia kwenye mahusiano

Reen tz

Member
Joined
Jul 14, 2021
Posts
6
Reaction score
9
Watu wengi katika maisha wamekuwa wakilaumu upande mwingine iwe mke wake au mume wake kwamba ndiye sababu ya kuvunjika kwa uhusiano au ndoa yao. hakuna jambo muhimu maishani mwako kama huo uamuzi unaotaka kufanya, unaweza kukupa furaha ya maisha au uchungu wa maisha.
Unaweza kujenga ndoa kwa kuvutiwa na umbo la mtu (mvuto wa nje) au urembo tu. Pia sasa hivi kuna uzuri mwingi tu na unauzwa dukani (body shops)
Unavutiwa na kipande kimoja tu cha mwili wake kama vile shingo, matiti, shepu, unene, au wembamba, nywele, anavyotembea, miguu, au kifua nk. anaweza kubadilika kuna kuugua, kuna ajali, kuna kubadilika mwili nk kwa hiyo ku-base kwenye mwonekano wa nje peke yake lisiwe jibu kwako kuona huyu mtu ananifaa.
Watu wengi katika maisha wamekuwa wakilaumu mwingine iwe mke wake au mume wake kwamba ndiye sababu ya kuvunjika kwa uhusiano au ndoa yao.
muhusika mara nyingi ni wewe kwa asilimia 99.
Niushauri tu,Tuzingatie hizo changamoto, pale tunapo itaji kuingia katika mahusiano.
 
Back
Top Bottom