Guys, hongereni kwa mjadala mzuri wenye maelekezo muhimu na Hongereni pia kwa kuingia kwenye Historia UDOM, Napenda kutoa angalizo tu kwamba mjadala huu ni wa muda mrefu tokea 2012 ila yapo baadhi ya mambo/ushauri ambao ni endelevu kwa maana ya kwamba utakusaidia. Mambo mengine yamepitwa na muda kutokana na uzoefu wa mtoa post kwa wakati huo na nawashauri muendelee kuuliza ili wenzetu waliopo huko kwa sasa watupe taarifa sahihi kwa mujibu wa wakati huu. Unaweza kwende kugombana na Makonda wa daladala wakati nauli ilibadilika....unaweza kwenda kwa Wajasi kumbe cafe za chuo wamebadili huduma zao.....sasa tuwe makini na uzi huu! Thanks na masomo mema "White University" (Hii ndio rangi yake)
Naomba niulize swali la Kipimajoto:::
Katika Tanzania hii, ni chuo Kikuu kimoja tu ambacho kinaanza na article "THE" unapokitaja. nacho ni THE UNIVERSITY OF DODOMA...unafikiri ni kwa nini????