MotoYaMbongo
JF-Expert Member
- Jan 7, 2008
- 2,146
- 887
Mimi ni Mwalimu wa level ya Shahada, ni kweli matatizo yako mengi sana yanayoua elimu yetu, kinachokatisha tamaa Serikali imekuwa inashughulikia majengo, vitabu, ajira, Motisha kwa maafisa elimu, lakini Mwalimu ambae ndio anawasiliana na mtoto moja kwa moja darasani hathaminiwi.
Inauma sana leo Mwalimu nina Shahada yangu nazidiwa sana mshahara na Mtumishi wa kada nyingine kama Afya mwenye Stashahada eti kisa tuko wengi, kwa hiyo kuwa wengi ni dhambi? Naiomba tume, isifiche ukweli kwamba, pamoja na yote yatakayorekebishwa, kama Mwalimu ambae ndie mtekelezaji mkuu darasani ataendelea kupuuzwa, kudharauliwa, hatutafanikiwa kwa kweli.
Kumlipa Mwalimu pekee bila kurekebisha mfumo mzima hakutasaidia na pia kurekebisha mfumo mzima bila kumlipa Mwalimu vizuri pia hakutasaidia, yote yafanyike kama kweli Serikali ina nia ya dhati ya kupunguza tatizo hili kama si kulimaliza kabisa.