Ushauri kwa shule za Dsm na wizara ya Elimu

Ushauri kwa shule za Dsm na wizara ya Elimu

Ushauri wangu kwa serikali ninkuwabia wananchi wake ukweli kuwa elimu na huduma za afya sio completely bure.

Ushauri wangu kwa wazazi ni kuhudhiria bikao vya wazazi, mambo haya yote huamuliwa kwenye vikao vya wazazi. Na ukienda ukiona wengi wanapitisha sera ambayo wewe huitaki, nyoosha mkono sema “mimi flani mzazi wa flani sitachangia huduma hio na mtoto wangu asibuguziwe”
 
Pamoja na malalamiko yote hayo kiini cha tatizo ni wazazi.
Hapo wengi mko tayari kuwa na watoto lakini malezi ya watoto hamko tayari.

Wanaume wengi wa kibongo matuzimizi yao binafsi kwa siku ni zaidi ya tsh 10000,, tena hao ni wa kipato cha chini wengine matumizi Yao binafsi kwa siku ni zaidi ya 100000 tena hapo anakwambia kajibana sana.

Mtoto juu ya miaka mitano anahitaji malezi kupitia pesa yako zaidi maana hapo mtoto kaanza shule, muda na akili.
Wazazi wapeni malezi stahili watoto ikiwepo haki ya kufurahia mazingira ya shule bila kuwa na njaa na bila kutamani vya wengine.
Baadae mtoto akiwaka tamaa akaanza wizi au uhuni utamlaumu Nani!?

Pia muwe mnahudhuria vikao vya shule na kushiriki mijadala kuepusha malalamiko kama haya.
Una hoja nzuri ila umeongea kwa ujumla sana, yaani mimi matumizi yangu binafsi yawe juu ya yale yanayo takiwa nyumbani kwenye watu wengi?
 
Una hoja nzuri ila umeongea kwa ujumla sana, yaani mimi matumizi yangu binafsi yawe juu ya yale yanayo takiwa nyumbani kwenye watu wengi?
Point kuu ilikuwa ni uwajibikaji. kama unavyowajibika juu ya mahitaji yako,, timiza wajibu huo kwa mwanao ikiwemo hitaji la chakula shule.
 
Inasemekana kwa mikoa ya kaskazini moja ya sababu inayochangia wanafunzi kufanya vizuri ni uwepo wa chakula shuleni, wewe mtaalamu unatuambia wazazi wanabebeshwa mzigo mzito wanapotakiwa kuwapa watoto wao buku buku za maosi shuleni, kwa hiyo unamaanisha hakuna haja ya mwanao kupata chakula awapo masomoni?
Kuna hoja namba 2, huenda ikapunguza hii changamoto kiasi flani.
 
Na wewe mzazi ukijua mwanao kachapwa kisa hajaenda na hela wakati si kosa la mtoto nenda shuleni uwaambie walimu . Mtoto anahusika vipi na mzazi kukosa hela? huko ni kumharibu mtoto kisaikolojia hadi anachukia shule.
Nakumbuka nikiwa shule ya msingi kuna mwalimu alichapa wanafunzi kisa hawajalipia hela ya masomo ya ziada , kumbe yule mwalimu ana madeni yake alikuwa anategemea hela za tuisheni akalipe. Mwalimu mkuu akapata taarifa, aling'aka hadi sio poa ikabidi yule mwalimu aje kuomba msamaha kiushkaji. Mtoto apewe adhabu pale anapokosea, kwanini mtoto aadhibiwe kwa sababu mzazi wake hajatoa hela? Mtoto anahusika vipi na mzazi kutokuwa na hela? huko ni kuadhibu au kutengeneza trauma?
 
Mimi binafsi sifurahishwi kabisa na tabia inayojitokeza katika baadhi ya shule za msingi ambapo mtoto anatakiwa kwenda kila siku na shilingi 1000 kwa ajili ya chakula, na endapo akikosa hela hiyo anapewa adhabu ya fimbo au kubezwa.

Ninapenda kutoa maoni yangu kwa heshima, lakini pia kwa uwazi:

1. Si kila mzazi ana uwezo wa kutoa pesa kila siku, hasa katika mazingira ambayo mambo ya kiuchumi ni magumu.

2. Kama mzazi nina uwezo wa kumpikia mtoto chakula nyumbani na kuweka kwenye chombo chake, si sahihi kwa shule kukataa mtoto kutumia chakula alichopewa nyumbani.

3. Shule kutaka pesa pekee kama njia ya kupata chakula, bila kuzingatia hali tofauti za familia, kinaweka mzigo usio wa lazima kwa wazazi.

4. Mtoto kupigwa fimbo kwa sababu ya kukosa fedha ni jambo linaloumiza sana—kisaikolojia na kimwili—na halipaswi kuwa adhabu ya kosa kama hilo.

5. Elimu ya msingi hapa nchini inapaswa kuwa bila vikwazo, na mzazi kumwandalia mtoto chakula si kosa, wala haitakiwi kuwa chanzo cha adhabu.

6. Tunapaswa kufundisha watoto utu, heshima, usawa na upendo—sio kuwaogopesha au kuwaumiza kutokana na changamoto za nyumbani ambazo hawana uwezo wa kuamua.

7. Wizara ya Elimu na mamlaka husika zingeangalia suala hili kwa makini, kwani linaathiri motisha ya watoto kusoma na linaweza kuchochea unyanyasaji wa kimyakimya shuleni.

8. Naamini kuna njia bora zaidi za kusimamia chakula cha wanafunzi, kama maelewano na wazazi, si adhabu.

Kwa kifupi: Mimi binafsi sina furaha na mwenendo huu, na ninaamini kuna haja ya mabadiliko ili kulinda usalama, utu na haki ya mtoto kupata elimu bila hofu au shuruti zisizo na msingi.
Habari huu ujumbe nimekutana nao Facebook amepost mdau

#followerseveryone
#wizarayaelimu
#WatotoKwanza
#trackandfield
Hilo la kuchapwa hapana, lakini hebu fikiria mtoto anakaa shuleni asubuhi hadi jioni bila kula, si atapata utapiamlo? Hilo la mzazi kumpikia mwanae chakula sidhani kama ni njia sahihi ya kutatua tatizo, wapo wazazi ambao watawapa watoto wao bagia moja na hiyo bagia atakwenda kugawana na wenzake. Hapa hiyo 1000/= kwa mwezi ni wastani wa Tsh 28,000/= sidhani kama mzazi anaweza kuikosa!
Kaeni vikao na uongozi wa Shule kama wanavyofanya huko kaskazini, mkubaliane kiasi kwa mwaka kwa ajili ya chakula mlipe. Hakuna elimu bila gharama... lakini pengine hili linaweza kuisha endapo serikali itatoa ruzuku ya fedha za chakula
 
Back
Top Bottom