The only
JF-Expert Member
- May 19, 2011
- 11,172
- 14,727
UCHAMBUZI WANGU JUU YA MAKOSA YAKE
1.Kuhubiri waumini wake wanywe pombe na kuinywa madhabahuni mwake-Kisheria hafanyi kosa lolote kwani pombe ni halali kisheria na swala la mjadala kama ukristo unaruhusu pombe ni la kidini na watanzania wanahaki ya kutofautiana mitizano ya kidini ,mfano kanisa katoliki kwenye sherehe za kuwaapisha mapadre baada ya misa hukutana kunywa pombe Je Mh Kardinali pengo akamatwe maana anahubili kunywa pombe kiasi sio kosa kibiblia ,kwenye hili aachwe aifurahiye katiba yake .
2.Kuhubiri kutembea na mahausi geli
-Point of collection anasema anashauri kuwaoa amablo si kosa kisheria ,hata yeye alimuoa kijakazi wake . Kona makosa aina tatu jinai mfano kuua ,madai mfano kudai fidia ya kutumiwa jina lako kibiashara bila makubaliano na aina ya tatu inaitwa maadili (moral crime) hizi hazishitakiki mfano umekutana na mtu mzima hujamwambia shikamoo na umegoma ,umepanda daladala kaingia mzee umegoma kumpisha ,umealikwa kwenye harusi ya kaka yako wa kuzaliwa umegoma kwenda umeamua kulewa baa ya nje ya ukumbi haya yanatabia kama makosa mengine ya kuumiza wengine ila dunian nzima huwezi mshitaki mtu kwa hayo.
3.Kuvaa hereni na kucheza taarabu
sheria yetu haitambui popote kuvaa heleni kama kosa bali kuwa uchi,pia taarabu ni mziki halali wa kuburudisha na unalipia kodi zikiwemo zilizokusomesha ,na aina yoyote ya kucheza haijakatazwa kisheria ndo maana nyimbo kama ''nyama ya bata'' zinalipiwa kodi na tafsiri inabaki jambo binafsi mno ,unless upatikane ushahidi mwingine
4.Unasema tra ichunguze mapato yake sababu unywaji wake pombe
Napenda nikuhakikishie tra basi itabidi iajiri nusu ya watanzania maana ukienda sinza kuna watu elfu wanalewa kila siku na ni wale wale ,nakumbuka mm nikiwa chuo mapato yangu ya kuishi yalikuwa hayatoshi kununua hata creti kwa wiki mbili lakini hakuna club mjini sikuingia mi kazi yangu ilikuwa kubeba mapochi ya mashemeji na kuwa na heshima kwa mabroo waliokuwa wanasoma na wameajiliwa hao walikuwa washafanya kazi muda sana na wanamiradi inayolipa kodi sasa akitokea mtu kama tito akaja na maneno yake washalewa atakunywa bia hadi atamba na hela juu.Usiwasumbue tra waache wakomae na wezi wa madini yetu.
HITIMISHO KIKRISTO
Anachokifanya Tito ni ukosefu wa mila za kiafrika na kidini ya kikristo kwa tafsiri ya jamii (HAKUNA OWNER WA TRUTH) Hivyo kazaneni kumdeal kiroho zaidi na mmwite kiupole na kistaarabu kumkanya kama ndugu someni hapa
Matayo 18:15-18Neno: Bibilia Takatifu (SNT)
Ndugu Yako Akikukosea.
15 “Kama ndugu yako akikukosea, nenda ukamwambie kosa lake mkiwa ninyi wawili peke yenu. Akikusikiliza, utakuwa umempata tena ndugu yako. 16 Kama hatakusikiliza, nenda na mtu mwingine mmoja au wawili kusudi wawepo mashahidi wawili au watatu wa kuthi bitisha jambo hilo.17 Akikataa kuwasikiliza, liambie kanisa. Kama akikataa kulisikiliza kanisa, basi mhesabu yeye kama ni mpa gani au mtoza ushuru.
18 “Nawaambieni kweli, lo lote mtakalokataza duniani lita kuwa limekatazwa mbinguni. Na lo lote mtakaloruhusu duniani litaruhusiwa mbinguni.
Hata yesu alipokuwa anahubili mambo ambayo wayahudi waliona hayaendani na mafunzo yao kwa mtizamo wao kama ulivyo wako ,walifanya kosa lako la kumpeleka kwa pilato pilato wa watu aliona huo ni upuuzi ila akaogopa kupinduliwa akawaambia haya
yHANA 19 😛ilato akatoka tena nje, akawaambia, "Tazameni, namleta nje kwenu, mpate kujua kwamba mimi sikuona hatia yoyote kwake." 5 Basi, Yesu akatoka nje amevaa taji ya miiba na joho la rangi ya zambarau. Pilato akawaambia, "Tazameni! Mtu mwenyewe ni huyo." 6 Makuhani wakuu na walinzi walipomwona wakapaaza sauti: "Msulubishe! Msulubishe!" Pilato akawaambia, "Mchukueni basi, ninyi wenyewe mkamsulubishe, kwa maana mimi sikuona hatia yoyote kwake." 7 Wayahudi wakamjibu, "Sisi tunayo Sheria, na kufuatana na Sheria hiyo, ni lazima afe, kwa sababu alijifanya kuwa Mwana wa Mungu."
Pilato kwa hofu ya kupoteza ufalme maana alipo muhoji yesu aliona anahoja na ni mabo ya kiroho si kitawala alitoa hukumu hivi iliyowapa laa alisema
19 Pilato aliandika ilani akaiweka juu ya msalaba. Nayo ilikuwa imeandikwa hivi: "Yesu wa Nazareti, Mfalme wa Wayahudi."20 Wayahudi wengi waliisoma ilani hiyo, maana mahali hapo aliposulubiwa Yesu palikuwa karibu na mji. Tena ilani hiyo ilikuwa imeandikwa kwa Kiebrania, Kilatini, na Kigiriki. 21 Basi, makuhani wakuu wakamwambia Pilato, "Usiandike: Mfalme wa Wayahudi, ila Yeye alisema, Mimi ni Mfalme wa Wayahudi." 22 Pilato akajibu, "Niliyoandika, nimeandika!"
maana yake pilato hakuona hatia yoyote na aliamini kwa hoja za huyu myahudi mwenzenu na huu ujinga wenu wa kudeal na mtu bila kuzingatia sheria bali miamko ya kidini nasi ni wajinga mmepoteza mwenye akili kuwazidi na ni mfalme wenu akasisitiza ''niliyoandika nimeandika''
MSIMAMO WANGU JUU YA TITO BINAFSI
Mimi mkatoliki naamini huyu bwana ni nabii wa uwongo anayetaka kujinufaisha kwa kuhubili ulaini kwenye dhambi zilizowanogea watu ,yaani ni sawa na uje na post ya kuwasifu wadada wanaojiuza lazima wakutafute inbox,ila sioni hatia yake kisheria tupambane naye kwa maombi na kumkanya kwani adui yetu si yeye ni shetani
"Kwa maana kushindana kwetu sisi si juu ya damu na nyama; bali ni juu ya falme na mamlaka, juu ya wakuu wa giza hili, juu ya majeshi ya pepo wabaya katika ulimwengu wa roho." Waefeso 6:12
ASANTENI WAKUU