Ushauri kwa Serikali kuhusu vijana

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
814
1,000
Habari Watanzania!

Heri ya mwaka 2020. Niende moja kwa moja katika ushauri wangu kwa serikali kwenda kwa vijana.

Serikali naishauri anzisheni taasisi ya "MAMLAKA YA VIJANA, WALEMAVU NA UWEZESHAJI" ambayo itakayojikita kuhusu vijana namna ya kuwatambua, kujua viwango vya elimu zao, mahali walipo, namna ya kuwawezesha kiuchumi na kuwafikia moja kwa moja. Hii itasaidia kweli kupunguza uhaba wa ajira kwa vijana maana mamlaka itasaidia taasisi nyingine kiutendaji.

Vijana watatambulika kitakwimu kwa usahihi, kiuchumi, kimaendeleo, kielimu pamoja na kiutendaji.

Serikali hamtakuwa mnasumbuka kuhusu kudai mikopo kuhusu vijana mfano, HESLB, Banks, NEEC nk.

Pia hii itasaidia kuondokana na wanasiasa kutumia changamoto za vijana kama mtaji kujipatia kura.

NB
Ruksa kuongeza maoni.
 

guzman_

JF-Expert Member
Jan 27, 2016
1,161
2,000
Serikali haiwezi na haitokas iweze kuwasaidia vijana kiuchumi na mtu akisema hivo huyo ni tapeli. La msingi na bora ni mfumo mzuri wa vijana kujiwezesha kiuchumi. Mfano: Kuna vijana wenye nia na ujuzi mkubwa wa utengenezaji furniture mathalani serikali inaweza zuia au kucontrol imported low quality from outside na kuhamasisha wenye mitaji kuwekeza huko. Mbili: Kuondoa kodi kubwa na mlolongo mkubwa wa ufanyaji biashara na uanzishaji biwanda vidogo kuwasaidia wenye mitaji midogo kushiriki katika shunguli za uchumi.

Sent using Jamii Forums mobile app
 

Masalu Jacob

JF-Expert Member
Jul 26, 2017
814
1,000
labda alikua anamaanisha kuwekwe mpango maalumu ku tackle tatizo la ajira kwa vijana..maana hili tatizo linazidi kukua in magnitude.
Lengo sio hilo bali pawepo na taasisi moja "one stop centre" itakayo jihusisha na vijana tu ktk taifa ili kuondoa matatizo na malalamiko huku pakiwekwa uboreshaji huduma nchini.
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom