Ushauri kwa serikali kuhusu SALARY SLIP

Ushauri kwa serikali kuhusu SALARY SLIP

kweli nchi imechoka, hata salary slip wanashindwa ku print? sidhani kama ilishawahi tokea siku za nyuma
 
Sizani Kama wewe ni mtumishi kwa unavyokoment. Yani mtu atoke kigoma huko aje Dar kufuatilia salary slip?
 
Kuna lundo la watumish halina email addresses,na huko walipo wengine hata mitandao ya sim haipo
Ni nafuu kutembea kilomita 5 kuufuata mtandao ulipo, kuliko kilomita 300 kuifuata ofisi ya utumishi ilipo.
Zipo namna za kuwasaidia wasiojua kutumia email. Hata tulipotaka kutoka analog kwenda digital, watu kama nyinyi mlikuwepo.
Leo tupo digital.
 
Ni nafuu kutembea kilomita 5 kuufuata mtandao ulipo, kuliko kilomita 300 kuifuata ofisi ya utumishi ilipo.
Zipo namna za kuwasaidia wasiojua kutumia email. Hata tulipotaka kutoka analog kwenda digital, watu kama nyinyi mlikuwepo.
Leo tupo digital.
Ni kweli,ila kwa mfano kwenye hizi halmashaur huwa salary slip zinapatikana,uwekwe utaratibu ofis husika impe mtu posho ya kufata salary slip,mie ofisin kwangu kila aendae halmashaur huchukua za watu wote na kuzileta ofsin
 
Hata zinazokuja hazitufikii! Na watendaji halmashauri wamekosa ubunifu yani hata kuweka salary slip alphabetically katika bahasha wanaona shida! Unakuta salary slip zimechanganika mpaka shida;
 
Mada inajadiliwa kwa maslahi ya taifa na sio wa dar es salaam pekee.
Kwanza kwanini ufunge safari uifate wakati ni haki yako halali kupewa...
Wanatakiwa waache kuendesha mambo kianalojia..dunia imebadilika...email huwa zinajazwa kwenye particular za mfanya kazi za nini...
Mi nahisi kuna hela zinaibiwa kimya kimya [emoji13] [emoji13] [emoji13] [emoji23] [emoji23] [emoji23] wakikata 10000 kwa kila muajiriwa wana sh ngpi kwa mwezi[emoji99] [emoji99] [emoji99] [emoji99] [emoji99]
 
Mbona huku Private tunatumiwa Kwenye e mail mpunga ukishaingia? Aisee kumbe serikalini mnapelekwa kishamba hivyo?


Poleni na Endeleeni kuisoma namba
acha ushabiki maandazi,,,,unasifia prvate sector wakat kimoyo moyo unatamani kuwa mtumishi wa serikali...
 
Habari za asubuhi ndugu wanajukwaa?

Kwa wafanyakazi wa serikali mtafahamu kuwa imekuwa ni muda mrefu sasa wafanyakazi wa serikali hatupati haki yetu ya hati za malipo ya mshahara - salary slip. Hapa ofisini mara ya mwisho kupata salary slip ilikuwa mwezi wa 5, 2016.

Tumekuwa pia tukiskia mambo mengi kuhusu hili, ikiwemo serikali kukosa karatasi za kuprint hizo slips na mengine wanayoyajua wao.

Nitoe wito kwa HAZINA kuwa kama suala ni kukosa karatasi basi iachane na kusubiri bajeti ya serikali kwenye karatasi ianzishe mfumo wa kieletronic ambapo kila mtumishi wa serikali kupitia "check number" yake ataweza kuaccess system na kuona e-slip yake na kama atapenda aprint mwenyewe kwa gharama zake.

System hiyo ipatikane kama webpage au mobile app au hata kwa wasio na uwezo wa kupata internet iwepo namba maalum ya mtu kurequest hiyo slip kupitia simu yake (Nokia torch).

Nawasilisha.
Salary slip ni za muhimu sana kwa mtumishi.Nakumbuka mimi ziliniokoa kupata pesa yangu PPF niliacha kazi wakati nafuatilia mafao yangu.
Jeduwali lilikuwa ninaonyesha sikuwa nimechangia kwa muda wa miaka 2 na pili linaonyesha nilishachukua michango yangu.
Ikabidi nipeleke salary slip zangu zote tangu nilipoanza kazi mpaka nilipoacha kazi ndio wakaanza kufanya marekebisho.nilipata pesa zangu lkn nilisota kuzipata.
 
Kuna kampuni fulani nilikuwa nafanya kabla sijahama yaani tulikuwa tuna account Kwenye HRM system.. Unaingia unapakuwa fasta...


Nilikuwa natamani kuhamia serikalini Lakini kama mambo ndo yako Local hivyo... Aisee mmmh!!!
Usihame .ni bora uwe private ubanwe lkn mwisho wa siku unalimpunga la maanaa..
 
Nyie watu wa Dar es salaam huwa mnajiona ndo nchi inaooishia!! Mbadilike, Tanzania siyo Dar es salaam pekee!! Mnadhalilisha watu wenye akili zao timamu huko mnaifanya jamii iwaone wote kama "wanaume wa daresalama"
wanaume wa dar walikugegeda nn? acha hoja za kingese
 
Kuna wengine pesa zetu zinakatwa hatujui. Tatzo liko wapi
Na mimi hasa ndicho kimenisukuma kushauri namna nyingine ya kurahisisha upatikanaji wa hizo slips! Kuna makato hayajulikani, mtu unashangaa mshahara unapungua tu na kwa vile hakuna salary slip basi huna pa kuanzia.
 
Back
Top Bottom