Ushauri kwa serikali kuhusu SALARY SLIP

Ushauri kwa serikali kuhusu SALARY SLIP

Mr. Django

JF-Expert Member
Joined
Jul 25, 2014
Posts
1,830
Reaction score
2,434
Habari za asubuhi ndugu wanajukwaa?

Kwa wafanyakazi wa serikali mtafahamu kuwa imekuwa ni muda mrefu sasa wafanyakazi wa serikali hatupati haki yetu ya hati za malipo ya mshahara - salary slip. Hapa ofisini mara ya mwisho kupata salary slip ilikuwa mwezi wa 5, 2016.

Tumekuwa pia tukiskia mambo mengi kuhusu hili, ikiwemo serikali kukosa karatasi za kuprint hizo slips na mengine wanayoyajua wao.

Nitoe wito kwa HAZINA kuwa kama suala ni kukosa karatasi basi iachane na kusubiri bajeti ya serikali kwenye karatasi ianzishe mfumo wa kieletronic ambapo kila mtumishi wa serikali kupitia "check number" yake ataweza kuaccess system na kuona e-slip yake na kama atapenda aprint mwenyewe kwa gharama zake.

System hiyo ipatikane kama webpage au mobile app au hata kwa wasio na uwezo wa kupata internet iwepo namba maalum ya mtu kurequest hiyo slip kupitia simu yake (Nokia torch).

Nawasilisha.
 
Mkuu mbona ukienda ofisi za utumishi unaweza ku printiwa
Ofisi za utumishi zipi? Sidhani kama kila mmojawetu na access na ofisi za utumishi kirahisi! Kuna watu wapo vijijini sana, na wengine hata wakienda ofisi zile wanaambiwa wanaondaa slips ni hazina na hazijaletwa!!
 
Wafowadi kwenye email zenu tu
Naam, hiyo pia ni njia nyingine bora kuongezea nilichoandika! Kimsingi slips ziwe electronic, namna ya kuzisambaza ni kama nilivyoelezea ukijumlisha na hii ya kwako, mabenk yanafanya hii njia yako!
 
Habari za asubuhi ndugu wanajukwaa?

Kwa wafanyakazi wa serikali mtafahamu kuwa imekuwa ni muda mrefu sasa wafanyakazi wa serikali hatupati haki yetu ya hati za malipo ya mshahara - salary slip. Hapa ofisini mara ya mwisho kupata salary slip ilikuwa mwezi wa 5, 2016.

Tumekuwa pia tukiskia mambo mengi kuhusu hili, ikiwemo serikali kukosa karatasi za kuprint hizo slips na mengine wanayoyajua wao.

Nitoe wito kwa HAZINA kuwa kama suala ni kukosa karatasi basi iachane na kusubiri bajeti ya serikali kwenye karatasi ianzishe mfumo wa kieletronic ambapo kila mtumishi wa serikali kupitia "check number" yake ataweza kuaccess system na kuona e-slip yake na kama atapenda aprint mwenyewe kwa gharama zake.

System hiyo ipatikane kama webpage au mobile app au hata kwa wasio na uwezo wa kupata internet iwepo namba maalum ya mtu kurequest hiyo slip kupitia simu yake (Nokia torch).

Nawasilisha.
Mbona huku Private tunatumiwa Kwenye e mail mpunga ukishaingia? Aisee kumbe serikalini mnapelekwa kishamba hivyo?


Poleni na Endeleeni kuisoma namba
 
Mbona zipo hazina ,ukienda tuu dakika tano unapewa,labda kama ni wa mkoani.
Nyie watu wa Dar es salaam huwa mnajiona ndo nchi inaooishia!! Mbadilike, Tanzania siyo Dar es salaam pekee!! Mnadhalilisha watu wenye akili zao timamu huko mnaifanya jamii iwaone wote kama "wanaume wa daresalama"
 
Kishamba!! Ha ahaaaaaaa... Hii ndo serikali yako mkuu!
Kuna kampuni fulani nilikuwa nafanya kabla sijahama yaani tulikuwa tuna account Kwenye HRM system.. Unaingia unapakuwa fasta...


Nilikuwa natamani kuhamia serikalini Lakini kama mambo ndo yako Local hivyo... Aisee mmmh!!!
 
Nyie watu wa Dar es salaam huwa mnajiona ndo nchi inaooishia!! Mbadilike, Tanzania siyo Dar es salaam pekee!! Mnadhalilisha watu wenye akili zao timamu huko mnaifanya jamii iwaone wote kama "wanaume wa daresalama"
Povu la nini ndugu,nimesema ukienda hazina unapewa,mbona unakyrupukaaa?
 
Back
Top Bottom