Nyakwaratony
JF-Expert Member
- Dec 21, 2011
- 573
- 140
Hi all
Rafiki yangu anatarajia kufunga ndoa mwishoni mwa mwaka huu, na ndoa hiyo itafungwa kwao mwanaume (uhayani - Bukoba) tatizo ni kwamba huko Bukoba hana hata ndugu wa kuvuta na kamba wala rafiki.
Swali je inawezekana kufikia na kutokea hotelini?
Au anaweza kufikia hapo hapo ukweni? Vipi utaratibu unaotakiwa kufuatwa katika situation kama hii?
Mila za kihaya zinasemaje maana rafiki yangu sio muhaya?
Contradiction.
Kwani hasindikizwi hata na mama yake, baba ama kaka? Hauwezi kutokea ukweni kwenda kuolewa bwana! Japo zamani uncle wangu akioa tulienda sendoff kijijini kwao aunt, tukasepa na mwali wetu. Kwa bibi wakawa wamepewa room akalala na maids na dada zake.
Kwa dunia ya leo waweza pewa sehemu ukweni mkala (hali imeguwa jiwe sana) ila kama yuko fiti achukue flight afikie hoteli then harusini ila ni bora kuwapa wakwe heshima ya kuwahifadhini.
Hivi ndoa huwa inamfuata bibi au bwana? Au huyo mwanaume ndio anaolewa? Hata hivyo haya yamekua mageni sana kwa upande wangu kiasi cha kushindwa kuchangia.
Shemeji " mume mtarajiwa' wa shogaangu ndio kang'ang'ania kuwa lazima harusi ifanyikie kwao.
Sasa huyo binti (Shoga yako) hana wazazi? au anakwenda yeye kama muolewaji na mzazi! Kama hamna ndugu sio mbaya hata akitokea Gest maana hamna jinsi.
ndoa hiyo mbona ina utata,kidogo au mwandishi ndo sjamuelewa
Huyo rafiki yako mdada aongee na mumuwewe mtarajiwa, awafanyie arrangement ya guest house, hotel au lodge kutegemeana na uwezo wao, ambapo atafikia yeye [bi harusi mtarajiwa] pamoja na troop yake [wazazi, kakazake, rafiki, matron n.k]. Huyo mume mtarajiwa amtafutie na salon. Wanafike Bukoba Alhamisi, washinde Ijumaa kuweka mambo sawa na kuondoa uchovu, na Jumamosi iwe harusi. Jumapili wapambe watageuza kurudi, na maharusi watajiju, kutegemea na honeymoon plan
"Amandla!" .... "Awethu"! Power!" .... "to the People!"
Samahani dada naona kama sijakuelewa vile, hapo umesema wakwe (kwao mume mtarajiwa ) wanaweza kutoa chumba kwa ajili ya wazazi, madada/makaka, maids na bibi harusi mtarajiwa?