pocha2
JF-Expert Member
- Sep 23, 2014
- 890
- 396
Nikiangalia juhudi za huyu kijana anaitwa Ruge Mtahabwa katika kuunganisha Taifa na hasa baada ya uchaguzi uliokuwa na vishindo na ambao haujawahi kushuhudiwa hapa nchini, na zaidi, juhudi zake katika kuwajenga vijana kwenye mambo ya ujasiliamali na ukweli kwamba wana beef (kama watoto wa Siku hizi wanavyosema) na mwenzake Paul Makonda (Bashite), Nashawishika kumshauri Mh Rais (kama Raia na Mtanzania Mwema) amteue huyu kijana (Ruge) kuwa mkuu wa mkoa na ikibidi amuweke hapo Pwani ili washindane katika kuwaletea watanzania Maendeleo badala ya hizi purukushani ambazo hazina maana.