Ushauri kwa Mdau Wadada wa Kisonjo

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,606
1,956
Wakuu habarini.
Juzi nilitembelewa na Mshkaji ambae ndio Amepata Uhamisho kuja pande Hizi za Arusha. Nilzungumza nae mengi ila kubwa aliniomba Ushauri kuhusu Wanawake wa Kisonjo.Alifunguka Kuwa Yupo Mbioni Kufanya Maamuzi na Huyo Mdada wa Kisonjo is one of Candidate hivyo Angependa Kupata Maoni Yangu.
Wadau Tafadhali Sana Mpeni Ushauri Mwenzetu Mapema ili Aweze Fanya Maamuzi.
Karibuni
 
Yupo mbioni kufanya maamuzi sasa unataka tumpe maoni gani?

Aende Wasso au Loliondo au Samunge akawaona wanayoishi ndiyo atawajua vizuri hao wadada wa kisonjo
 
Duuh we jamaa unafanya utafiti nini kila siku na makabila juzijuzi wahaya na wajita, ukaja wanyiramba na wanyaturu leo uko na Wasonjo...mmmh


Mwambie aende kwao akaulizueulizue mila za huko atapata cha kujifunza
 
Wakuu habarini.
Juzi nilitembelewa na Mshkaji ambae ndio Amepata Uhamisho kuja pande Hizi za Arusha. Nilzungumza nae mengi ila kubwa aliniomba Ushauri kuhusu Wanawake wa Kisonjo.Alifunguka Kuwa Yupo Mbioni Kufanya Maamuzi na Huyo Mdada wa Kisonjo is one of Candidate hivyo Angependa Kupata Maoni Yangu.
Wadau Tafadhali Sana Mpeni Ushauri Mwenzetu Mapema ili Aweze Fanya Maamuzi.
Karibuni
Wasonjo ni moja ya makabila yanayopatikana mkoani arusha, wilaya ya ngorongoro kijiji cha sale karibu na maeneo ya loliondo na samunge.
Ni kabila linalokaribiana na tamaduni za kimasai ila tofauti yao ni kwamba wasonjo wanalima sana na pia wanajenga nyumba za kudumu za kisasa tofauti na masai wanaoishi kwenye maboma.
Kabila la wasonjo hasa wanawake ni waaminifu sana wanapoolewa hii inatokana na tamaduni zao jinsi walivyokuzwa.
Ila wanaume wa kisonjo ni wana wivu sana kwa wanawake wao hasa wakiona mtu wa kabila lingine anamendea.
Silaha kubwa ya wasonjo ni mishale ya sumu ambayo huitumia hata kuwapiga wanaume wakwale.
Wasonjo ni kabila dogo sana, ila ni kabila linaloogopwa sana na masai ukanda wa loliondo sababu ya kutumia silaha zenye sumu ikiwemo mishale.
Mara nyingi kumekuwa kunatokea vita ya masai na wasonjo maeneo ya samunge na loliondo hasa kunapotokea kuibiana mifugo kati yao, watu hupoteza maisha na mwamuzi wa hiyo vita huwa FFU na Polisi kutoka Loliondo au arusha.
Nimejisikia tu kuelezea kwa kifupi hili kabila sababu ni moja kati ya makabila madogo nchini Tanzania yasiyofahamika.
Ila namshauri huyo rafiki yako amuoe huyo binti wa kisonjo sababu hao mabinti huwa na nidhamu sana kwa waume zao na hiyo inatokana na tamaduni zao na ni kama nidhamu aliyonayo mwanamke wa kimasai
 
Back
Top Bottom