ushauri kwa madada zangu, wake, wapenzi na mama zetu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

ushauri kwa madada zangu, wake, wapenzi na mama zetu.

Discussion in 'Mahusiano, mapenzi, urafiki' started by OGOPASANA, May 22, 2012.

 1. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #1
  May 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  heshima kwenu wakuu, ushauri wangu ni kuhusu mapishi na mapochopocho mnayotupikia hasa kwa sisi watu wa hali ya kati na chini. wanawake wengi hawana ubunifu katika sekta nyeti ya mambo ya jikoni kitu kinachopelekea tuzoee vyakula vinavyopikwa majumbani mwetu kwani ni vile vile tu vinajirudiarudia.. mfano asubuhi unaweza kupikiwa chai na vitafunwa (vitumbua,mikate, chapati,maandazi nk) ambazo kwa asilimia kubwa ni vyakula vya aina moja (starch)... mchana utapikiwa ugali / wali na mboga ambavyo navyo ni starch na usiku utakuta unaweza kupikiwa wali / ugali (starch) ukibadilishiwa sana viazi, ndizi, makande hali inayopelekea afya zetu hasa nguvu za kiumeni kuwa DUNI na kusababisha kutufaya kuwa wazito na kuota vitambi.

  USHAURI:
  1 - kuna makabila zaidi ya 120 hapa nchini ambayo kila kabila lina chakula chake kikuu that we might be interested kula vyakula hivyo + vyakula mbali mbali kutoka makabila ya nchi za nje na huko dunia ya kwanza bila kusahau vile vya mahotelini kwa wenye kipato cha kati. Hivyo kama mwanamke akiwa mbunifu na akafahamu kuwa chakula ni basic need na sekta muhimu katika ndoa au maisha yao na mwenzake anaweza kufanya kila njia akajifunza namna ya uaandaaji wa kupika vyakula mbali kutoka sehemu nyingi duniani kama nilivyoeleza hapo juu, hali itakayopelekea kutorudia kupika chakula cha aina moja kila siku.

  2 - ni muhimu wanawake wetu wa tanzania wakajifunza si tu kipa na kuandaa chakula bali CHAKULA BORA na MILO KAMILI kwani ni muhimu sana sana katika kuwa na AFYA BORA. Kumbuka kuwa kula mlo kamili si gharama kama wengi wanavyofikiri bali ni kupangilia tu bajeti yako. Mfano: badala ya kununua nyama nusu kilo kwa ajili ya kupika mboga, unaweza ukanunua nyama robo , mboga za majani na matunda kwani kiasi kinachohitajika tumboni ni kiasi kidogo (vipande 2 hadi 4) vya nyama kuliko kumuandalia mumeo mchuzi jaa na vipande 10 vya nyama.

  Nawasilisha.
   
 2. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #2
  May 22, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Wanawake wangapi wanajishughulisha wenyewe jikoni?

  Sema wawatafutie wadada wanaowasaidia kazi sehemu ya kujifunza maana wao hata wakijua haitosaidia.
   
 3. Taz

  Taz JF-Expert Member

  #3
  May 22, 2012
  Joined: Feb 14, 2012
  Messages: 305
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Wewe mwenyewe unapika mara ngapi kwa wiki? mbona unataka kuwafanya wadada,wapenzi, wamama zetu kua wapishi tuu? Yani wanakupikia as a favor (because they have other things to attend as well) wewe unafanya kama ni job yao kabisa na unataka increased performance.
   
 4. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #4
  May 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  ukitaka kula vizuri ujue kutoa hela vizuri......

  Kama unatoa sh 5,000
  vitumbua/chapati 100*4*2=800
  nazi shilingi 800
  mchele kilo 2400
  maharage nusu 900
  kitunguu sh 100
  mafuta ya wali sh 200 kipimo
  mkaa sh 1800
  majani ya chai 100(ya kupima)
  sukari robo sh 500

  jumla sh 7,600 hapo mama lazima auze ubuyu karanga ili ajaze gap..........

  Kuna kubadili msosi hapo? Lazima mtoke vitambi. Unless kipindi cha msimu wa mihogo na viazi ndo mnabadili mlo
   
 5. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #5
  May 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  Lizzy nimewashauri wale wadada zetu wenye mazingira ya kuwapikia waume na wapenzi wao kila siku na si kama wale wazungu women types ambao kila kila kitu huwaachia housegirls wakati kiafrika ni kazi na majukumu ya mwanamke.
   
 6. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #6
  May 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280

  usiombe kuolewa na mwanaume ambaye ameoa ili wapate JIKO.
  Ili wapate DOBI
  ili wapate WATOTO
  ili wapate MLINZI wa nyumba
  ili apate mtu wa kumtunzia WAZAZI wake...
  Ili apate mtu wa kusimamia MIFUGO.....
  Ili apate wa KUMSAFISHIA nyumba

  Usitarajie kupikiwa wala kusaidiwa kazi za nyumbani, usitarajiwe kusaidiwa kubembeleza mtoto...

  Tarajia kumwandalia hadi maji ya kuoga....
  Tarajia kumnawisha hadi mikono......
  Tarajia kumvua hadi soksi
  tarajia kupelekwa kijijini ukaangalie wazee wake
  tarajia kusemwa huna ubunifu........
   
 7. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #7
  May 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  BD...haya ndo mapungufu ninayozungumzia mimi, wanawake wengi hamjui food cost... huo mfano uliotoa utakushinda kwa sababu inaonekana unafanya manunuzi ya vyakula kila siku, wakati ungeweza kunua mwisho wa wiki au mwisho wa mwezi ili uweze kutumia kiasi kidogo kidogo katika vyakula tofauti ulivyonunua...ndo maana mnafanya mishahara yetu kuishia katika majukumu ya nyumbani na kutufanya watumwa wa kazi.
   
 8. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #8
  May 22, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Haya basi. . .
  Hao wachache waojitahidi wanapata yepi toka kwa waume/wapenzi/kaka na baba zao? Hata ASANTE tu wanapewa? Wanaonekana na kujulishwa kuwa wana bidii? Kazi ya mikono yao inasifiwa au ndo watu wanajaza matumbo na kuona 'ahhhhh asante ya nini wakati bibie ni kazi yake?!"
   
 9. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #9
  May 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  BD...acheni mambo ya kuiga wadungu, hizo ndo mila zetu na ni mambo yanayowezekana kama ukiweza kumanage muda na mumeo akikusaidia hayo majukumu na wewe ukamsaidia ya kwake...sasa we umeolewa ili mtoke outing?? akupe hela ya kwenda salon? akununulie gari? akununulie nguo mpya aliyokilingisjia mwenzio?... ndo maana siku hizi hakuna mapenzi, leo mmeolewa kesho mmeachana.
   
 10. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #10
  May 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  huo ni upande wa pili na ni maada nyingine hiyo, na ni wajibu wenu kuwajulisha waume zenu mnayohitaji kwao kama mlivyoanza kipindi mnatongozana ndo mapenzi mama, msifanye revenge.. sumu ya mwanaume ni mwanamke, na silaha ya mwanamke ni mwanaume.
   
 11. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #11
  May 22, 2012
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,876
  Likes Received: 6,231
  Trophy Points: 280
  hivi unadhani wewe ulivyo na uwezo wa kununua jumla kila mtu anao? Hujui wengine riziki yake iko mguuni? Akipata ndo mle...... Na mtakula kutokana na kinachopatikana? Unajua kuna watu tunashindia uji? Maisha magumu oooh....ndo maana nikasema utoavyo ndivyo utakavyokula....
   
 12. Lizzy

  Lizzy JF-Expert Member

  #12
  May 22, 2012
  Joined: May 25, 2009
  Messages: 22,224
  Likes Received: 244
  Trophy Points: 160
  Sasa wewe utamwambiaje tu mtu fanya hivi au vile bila kugusia atakachopata out of it?
   
 13. CUTE

  CUTE JF-Expert Member

  #13
  May 22, 2012
  Joined: Mar 5, 2012
  Messages: 1,237
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  tena na kipigo juu sa ingine
   
 14. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #14
  May 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  Lizzy ni ukweli usiopingika kuwa mapenzi na mahusiano mengi yanakufa ama kupoa kutokana na changes zinazojitokeza kadiri wanavyoishi na kwa kadiri unavyozidi kwenda katika mahusiano hayo,,,hivyo nina kila imani huu ni ushauri mmoja kati ya yale wanayoweza kuboresha ILI WAPENZI WAO WAWAPENDE KAMA MWANZO.
   
 15. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #15
  May 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  kwa hesabu za haraka haraka...anayenunua mahitaji na kutumia kila siku hutumia kiasi kikubwa kuliko yule anayenunua jumla na kutumia kidogo kidogo, kipato ni kidogo lakini lazima tuwe na nidhamu na hela tunazopata (kuweka kiasi kidogo katika kile tunachopata)..mbona kwenye harusi, kitcheni parties tunachangia 50,000?? hazitoshi kununua mchele kilo 10, maharage kilo 5, unga kilo kadhaa nk??
   
 16. OGOPASANA

  OGOPASANA JF-Expert Member

  #16
  May 22, 2012
  Joined: Apr 30, 2009
  Messages: 265
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 35
  Lizzy...kwa niaba ya wanaume wengine wanaojali, ASANTENI SANA kwa yale mnayotupa, mnayotufanyia na mnayotusaidia..you're appreciated..!! ndo maana tumewawekea siku ya wanawake duniani kuonesha tunawashukuru kwa yote mnayotufanyia.
   
Loading...