Ushauri kwa kijana mwenzetu

Miaka 29 unahangaika na jimama ambalo lilikwishaolewa na kuwa-widowed WHY?

Kama ni tamaa ya mali za marehemu mwambie aendelee; kama ni kutaka mke wa kuoa mwambie tamaa itampeleka pabaya!

........Mleta topic hakusema umri wa huyo mama, inakuwaje wewe unasema ni mama mwenye umri mkubwa kuliko huyo muoaji? Inawezekana huyo mama ana umri mdogo kuliko jamaa ndio maana jamaa anaona anamfaaa.
Vilevile huyo mama hakutaka kuwa mjane ila ni mipango ya Mungu tu kumchukua mumewe, inawezekana bado msichana tu.Ana haki ya kuolewa tena.
 

Kwani umeambiwa huyo mdada ni mkubwa?
 
Baba_Enock mgane mwanaume anaweza chukua binti ambaye bado hajaolewa?
 
mjadala unakwenda vizuri sana.
N:B mnahimizwa kuchunga matumizi ya spelling sahihi katika post zenu

yours faithfully
klorokwini a.k.a spare mod.
:focus:
 

Sio kawaida na ndio maana hata huyo mama yake ameshangaa! Hata ningalikuwa mimi kama mdogo wangu ananijia kwa ushauri katika situation hiyo pengine ningemuuliza au angalau kujiuliza 'hujaona ambaye anafanana na wewe'?

Naona kuna mambo mengi yanajitokeza hapa ambayo kwa kweli ni muhimu kwa kijana kuyatazama kabla hajafanya maamuzi mazito: Umri, mtoto, haki ya kuwa na mwenza.

Umri: Imejibiwa kabla kwamba wote wana miaka 29. Kwangu mimi naona ingependeza kama kijana angepata msichana mwenye umri wa chini kidogo. Najua wengi wanasema umri sio zaidi ya namba!

Mtoto: Kama ataamua kuendelea na huyo mama, ni vema wakakubaliana mapema jinsi watakavyo handle malezi ya huyo mtoto. Kuwepo kwa mtoto huyo kunaongeza complications ambazo pengine zisingekuwapo kama mwanamke angekuwa hana mtoto. Matatizo yanayotokana na kuwepo kwa watoto/mtoto wa kambo yamekuwa yakitishi ustawi wa ndoa nyingi tu. Kuna hata social pressure zinaweza kuleta taabu - utani kutoka kwa watu na kadhalika. Nakumbuka kuna rafiki yangu mmoja alikuwa anatatizo la kuona na mara nyingi watani zake walipenda sana kumtania ati 'anapenda kutembea na wanawake wazee'! Lakini ni vema nikasisitiza sio ndoa zote zenye watoto wa kambo zina matatizo!

Haki ya kuwa na mwenza: Ni kweli huyo mama anayo haki ya kupata mwenza kama mwanamke/msichana yeyote mwingine. Kuwepo kwa mtoto hakupaswi kumwondolea haki yake ya kuwa na mwenza. Hata hivyo kijana pia hapaswi kuingia kwenye ndoa kwa kumwonea huruma mtu. Kwanza ni yeye mwenyewe anatakiwa kuridhika nafsi yake na kisha ndio angalie mtu mwingine.
 
wanawake wengi ambao wanaoolewa kwa mara ya 2 wanakuwa wanaziheshimu sana ndoa zao,na wanakuwa wanyenyekevu sana katika ndoa zao.
 
kama mwanamama umri unaruhusu bado hana haki?...may b 25-29....mtoa thread hebu tuambie mwanamama ana age gani...au shida hapa ni kwamba kashaitwa mama?

Inawezekana mwanamke aliolewa mdogo labda hata sasa hajafikisha miaka hiyo 29 ya muoaji,pia izingatiwe alikuwa mkweli toka mwanzo kuna wengine wanapeleka mtoto kwa wazazi unakuja gundua baada ya miaka.
 

:thumb:
 
umeongea (sijui umeandika) vizuri sana ni kweli tatizo lipo ambalo ni kuoa mtu ambaye alishafunga pingu za maisha na kuingia mkataba wa ndoa na mtu mwingine lakini kwa kuwa amefariki huyo aliyefunga nae ndoa acha jamaa ajaribu tu haina tofauti sana na kuoa mtu ambaye hajaolewa kabisa maana wote hamjuani background zenu cha msingi ni kumwomba Mungu akupe hekima na mwongozo katika ili (kama alivyosema mama mzazi wa jamaa)
 

Poa mkuu, Hakuna mtu anayeweza kumzuia, isipokuwa yeye mwenyewe. Hapa tunajaribu kumuweka katika mazingira ya kufanya informed decision. Hebu jaribu pia kusoma ushauri wa SMU. Tatizo lipo ila kijana ndiye mwenye maamuzi ya mwisho.
 
Umri: Imejibiwa kabla kwamba wote wana miaka 29. Kwangu mimi naona ingependeza kama kijana angepata msichana mwenye umri wa chini kidogo. Najua wengi wanasema umri sio zaidi ya namba!

haaaa haaaaa........watu wabaya sana! Sasa mnataka wanawake wenye umri huo wachukuliwe na nani jamani? Kuna jamaa yangu formula yake hachukui kitu zaidi ya miaka 23, anasema ngoma ikishapita umri huo hailiki vizuri.........inakuwa ngumu kama shimo la panya!
 

Mkuu sisemi mwanamke mwenye umri wa miaka 29 ni 'mzee'! Kama ningalikuwa mimi ndio muoaji (say nina miaka 40:confused2:!), msichana/mwanamke wa miaka 29 bado ni 'mbichi' sana! Ila kwa kijana wa miaka 29 kuoa mwanamke mwenye miaka 29, mimi kwa upande wangu naona kuna walakini (najua hii ni opinion zaidi na sio hoja!)!
 

Kweli mkuu. Hili suala linatakiwa kuangalia kwa kulinganisha. Kama wote wanalingana umri si jambo zuri kwa kijana. Kwani wanawake wana biological limitations zinazohusiana na umri. Kuna mwanasayansi mmoja wa UK alishauri kuwa ingekuwa vizuri wanawake wakarudi kwenye uasili unaotaka binti kuanza kupata watoto walau kati ya miaka 15-30 kwani kipindi hicho hakina risk nyingi tofauti na sasa ambapo wanawake wengi huko Ulaya wanaanza kutafuta watoto baada ya kufikisha miaka 30.
 

SMU What if you are dating a woman who is older than you is there a problem on that as well, I know watu watasema mwanamke atawahi kuzeeka kuliko wewe.
 
SMU What if you are dating a woman who is older than you is there a problem on that as well, I know watu watasema mwanamke atawahi kuzeeka kuliko wewe.

I hope you are not implying 'dating' is synonymous to 'marrying'! Ninachosema ni kuwa sio kawaida! Hata kwenye kudate (kwa maana ya short term relationship) pia inategemea na hilo gap la umri. Kwa mfano nisingeweza kuwa comfortable kudate mwanamke alienizidi miaka kumi! Linapokuja suala la lifelong commitment, kwa kweli ushauri wangu ni kuwa mwanaume awe mkubwa kwa umri kulinganisha na mkewe!
 
Hapo Mama mzazi ameweka question MARK. Je hakuna ambaye hajawahi kuolewa? Mimi ninafikiri anachowaza huyo kilana ni lile swali! Ni heri Mama angesema neno moja tu kwamba simtaki huyu Mwanamke. Sasa kijana yuko njia panda. Anawaza je akioa itakuwaje?

Kuna laana zingine haziwezi kumpata mtoto hata iweje.. Cha muhimu je ni kweli huyo binti Mume wake alikufa kwa ajali? Maana USANII ni mwingi sana siku hizi ili mradi mdada aolewe.
 
Miaka 29 unahangaika na jimama ambalo lilikwishaolewa na kuwa-widowed WHY?

Kama ni tamaa ya mali za marehemu mwambie aendelee; kama ni kutaka mke wa kuoa mwambie tamaa itampeleka pabaya!
Mods nadhani inabidi kuwe na batani ya dislike. Wat kind of comment is this???!!!!!!!!!!!!
:mad2::mad2::mad2::mad2::mad2::mad2::mad2::mad2:
 
Mods nadhani inabidi kuwe na batani ya dislike. Wat kind of comment is this???!!!!!!!!!!!!
:mad2::mad2::mad2::mad2::mad2::mad2::mad2::mad2:
naona umekuja ''KIVINGINE''...
we know you so far
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…