Ushauri kwa Kamishna Mkuu wa TRA (Kiuongozi)

Tabutupu

JF-Expert Member
Nov 26, 2010
13,109
18,326
Naamini kabisa sina nafasi ya kukushauri kwa kuwa wewe ni mtu mkuu sana lakini kama ukipenda hapa chini nimeweka mawazo yangu ya kitoto ambayo kama yakikupendeza unaweza yasoma walau mara moja.

Kiongozi bora ni yule ambaye husikiliza wengine na kuchuja lipi ni jema.

Kiongozi mbaya ni yule asiyesikiliza .

Sasa kwa jinsi ninavyo iona TRA nimeona baadhi ya mambo yanaweza kukusaidia.

1. Hakikisha unapata update zote za nchi nzima kila siku juu ya operation zote ambazo maofisa wako wamezifanya. Hapa naongelea kubwa na ndogo kutoka kukamata mtu asite toa EFD resit hadi container zilizo zuiliwa bandarini.
Mfano : unatakiwa kujua kila siku biashara ngapi zimefungwa au zimepata mgogoro na TRA kwa nchi nzima. Na ikiwezekana afisa yoyote ambaye hata fikisha taarifa za operation ambazo amezifanya within 24 ni kufutwa kazi.

Kilicho mkukuza kichere ni yeye kutojua aliye ufungia mzigo kwa miaka 4 kwa sababu hajatoa rushwa.

2. Hakikisha unantaarifa zote za mizigo ambayo imezuiliwa au biashara ambazo zimezuiliwa ma maafisa wa TRA na updates uzipate on daily basis. Hii ni kwenye yadi zote za TRA. Sasa ivi utakuata kuna yadi ambazo zimejaa malori mengine yana miaka 10 na waliyo yakamata wamesha toka TRA.

3. Hakikisha unapata updates zote zinazo fanya na thirdparty kama Majembe Yono etc wanao kamata wakwepa kodi ya niaba ya TRA. Huko kuna uchafu mwingi sana. Sio tuu kupata updates ila pia kuhakikisha kesi zote umezielewa na zinatatuliwa kwa sababu hakuna kesi isiyo na jawabu.

4. Hakikisha vision na strategy yako yamemfikia kila mfanyakazi wa TRA kwa kukutana nao au kwa kufanya assessment mwenyewe ili ujiridhishe kama wazaidizi wako mpo njia moja au la.

5. Hakikisha vision na strategy yako IGP ameielewa na ameifikisha kwa jeshi la policy vizuri kwa sababu jeshi la policy ni moja ya taasisi inayo saidia kuipaka matope TRA.

6. Weka vigezo vya maamuzi .. mfano biashara yoyote au mzigo unaozidi kiasi fulani ili kufungiwa au kuwekwa kwenye mgogoro lazima kibali kitoke kwako au kwa mtu ambaye utamteua.

7. Hakikisha mabadiliko yote ya makadirio yanakufikia on time. Au weka sheria zako za ndani kwamba biashara yoyote ambayo kodi yake imebadilika let say kuanzia 20% lazima ipate kibali chako la sivyo mfanyakazi aliye kadiria akose kazi. Na mfanyakazi yoyote ambaye makadiri yake ya mwanzo na yale yaliyo kubalika na mlipaji yakizidi 30% akose kazi.

8. Swala la makadirio lifanyiwe kazi ili kwenye baadhi ya iashara kodi iwe inajulikana.

Mfano biashara ya mabasi.

9. Muombe Mungu akupe ujasiri wa kufanya kazi na hao wazee wa TRA.

10. Usihofu tunakuombea ufanikiwe sana hata tupate tr 2 kwa mwezi ifikapo 2020.

Mungu akubariki CG TRA.
 
Bila kusahau

Kuonana na wafanya biashara mara kwa mara ili kujifunza namna wanavyo shirikiana na TRA kwa lengo la kutejeleza matakwa ya sheria ya kodi au kwa lengo la kutaka kukwepa kodi.
 
Kabisa na hili ndilo linalo toa mwanya wa upigaji.

Unakuta mzigo wa aina moja kwa ukubwa ule ule ila kodi tofauti.
Pia ili kuepusha upigwaji weka utaratibu wa mlipa kodi awe anajua fika huu mzigo wangu wa kitu nilicholeta kutokana na ushuru wa serikali ni kiasi fulani badala ya kuwa na kodi tofauti kwa mzigo wa sina moja wenye thamani moja
 
Kabisa na hili ndilo linalo toa mwanya wa upigaji.

Unakuta mzigo wa aina moja kwa ukubwa ule ule ila kodi tofauti.

Hapana !
Nazani ni zaidi ya inavyosemwa kama kishabiki vile!

Siyo kweli kuwa mzigo ni sawa ktk aspects zote,

Mfano mzigo waweza kuwa ni sawa kwamba ni 1. “Tiles labda from China, lakini tiles hizo mwingine kaleta za ubora tofauti,
Aloleta tiles materials ya Ceramic hawezi lipa kodi sawa na aloleta materials ya Spanish,
Na size pia kuna ndogo na kubwa,

Ni kweli zote zaweza kuwa tiles toka nchi moja mfano toka China n.k lakini ubora wa hizo tiles na size huwa ni tofauti,

Kwa hiyo tusidanganyike na kujaribu kupotosha watu.

2. Batteries
Huwa zinatofautiana ktk capacity zao, nchi zilikotoka n.k

3. Tv
Tv zipo za size mbali mbali na bei huwa ni tofauti, tv kubwa bei kubwa n.k

Kwa hiyo tuache siasa kwenye mambo ya msingi yenye maslahi ya umma
 
I mean ;
1. Tiles zaweza kuwa ceramic au Porcelain

Wote wameingiza bidhaa moja ya tiles lakini ubora tofauti,
Kwa hiyo kusema kodi wanalipishwa tofauti ni sawa sababu ubora wa bidhaa waloleta unatofautiana ijapokuwa ni aina moja ya bidhaa!

Hata magari Yani mlipakodi ajilinganishe kati ya Toyota na Benzi walipe sawa kwa kuwa yote magari?
 
Nami niongezee kamoja. Usianze kazi na mentality ya kufukuza watu kazi. Akili za kuambiwa changanya na zako (Kwa hisani ya JK).
 
Kuna jamaa nilimsoma mahali akisema ili kuleta uwiano wa mizania ingekuwa vyema jamaa awaite na wale awasikilize
 
Kwanini unasema hivyo?
Hebu dadavua
Mashataka yaliyo semwa na wafanya biashara yana uhalisia na yanajulikana. Itakua vigumu sana kwa TRA kuyakana hata waje na mada nyingine .

Inawezekana kuna mabaya ambayo wafanya biashara wanayafanya lakini ukilinganisha na mabaya wanayo yafanya TRA wafanya biashara lazima waondoke washindi.
 
you can't have it both ways, as long as wafanya biashara ni haohao wachache ili afikie malengo anayowekewa lazima awakamue kisawasawa na hivyo kupelekea mazingira ya biashara yawe magumu zaidi na biashara nyingi kufungwa zaidi.
tukitaka kukusanya kodi zaidi ni lazima tukubali kupoteza kidogo katika kipindi cha mpito ili kuzipa nafasi biashara changa zikue na kuwavutia watu wengi zaidi kwenye biashara, lazima JPM akubali kurudisha pesa nyingi mtaani!
 
Pia
I mean ;
1. Tiles zaweza kuwa ceramic au Porcelain

Wote wameingiza bidhaa moja ya tiles lakini ubora tofauti,
Kwa hiyo kusema kodi wanalipishwa tofauti ni sawa sababu ubora wa bidhaa waloleta unatofautiana ijapokuwa ni aina moja ya bidhaa!

Hata magari Yani mlipakodi ajilinganishe kati ya Toyota na Benzi walipe sawa kwa kuwa yote magari?
Pia aangalie kwa makini kitengo kinachohusika na utoaji wa leseni za udereva pananuka kama siyo kuna uozo wa rushwa mbaya sana
 
Nami niongezee kamoja. Usianze kazi na mentality ya kufukuza watu kazi. Akili za kuambiwa changanya na zako (Kwa hisani ya JK).
Siyo mentality ya kufukaza watu kazi ila afukuze pale mtu anapofanya uzembe. Moja ya mambo yanayosababisha uendaji mbovu kwenye ofisi za serikali ni kulea uzembe. Anatakiwa awe mkali kweli kweli ila ukali wake uendane na haki! Mfanyakazi akifanya kosa kubwa kama la kushirikiana na waagiza mizigo kuhujumu mapato ya serikali afukuzwe mara moja. Kama kosa ni dogo ndio pale na onyo. Na la muhimu zaidi ni kuwafanya wafanyakazi kufanya kazi bila kuogopa na kwa kujiamini!
 
Huyu in mcha Mungu msomi industrious na muadilifu mwenye msimamo sina wasiwasi naye .

Kikubwa awe makini na madudu yanapoibuliwa na wanasiasa ayafanyie kazi fasta.mwenyewe nilishangaa PM aonyeshwe dhurumaile kwa mfanyabiashara alafu hakuna displinary action yoyote kwa wahusika hadi rais aseme!!
 
Pia

Pia aangalie kwa makini kitengo kinachohusika na utoaji wa leseni za udereva pananuka kama siyo kuna uozo wa rushwa mbaya sana
Hivi jamani hili la leseni za udereva kwa nini liwe na utata wakati ndipo sehemu ambayo naona ilitakiwa iwe clear kabisa? Sijui utaratibu wake lakini siyo kwamba kuna wahusika wawili wakuu 1. Polisi 2. TRA. POLISI anapopitisha kuwa fulani ana ujuzi wa kuendasha gari X kwa nini leseni isitolewe mara moja? Au utaratibu ukoje? Au pengine wangeachiwa polisi kufanya hii kazi na fedha inayopatika waipeleke TRA!
 
30. Fungua common email address, ambayo watu wenye malalamiko yao yaweze kukufikia moja kwa moja, maana wakati mwingine inakua taabu kukufikia, na uwe na deaturi ya kuipitia hiyo email au mpe mtu kazi awe anaingalia daily
 
Tatizo hawa wakubwa huwa wanakua na uboss sana. Anaagiza hafuatilii..

Nilisikitika sana kwamba kichere na msaidizi wake walikua wamesahau jina la yule kijana ambaye ameuzuia mzigo kwa miaka 3.

Back
Top Bottom