ANGUKO LA CHADEMA Linapozidi Kuonekana – CCM yazidi Kuimarika kwa Wapiga Kura.
Katika mchakato wa uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji, na vijiji, CHADEMA imeonyesha kushindwa kusimamisha wagombea katika sehemu kubwa ya nchi. Wakati ambapo Watanzania wanahitaji viongozi wa kuwajibika, ambao watawatetea na kuboresha hali za maisha, CHADEMA inabaki kutokuwa na nguvu za kisiasa za kuleta mabadiliko hayo.
Udhaifu wa CHADEMA unaonekana wazi na kuibua maswali muhimu. Inakuwaje chama kinachodai kuwa na ushawishi mkubwa, hakina uwezo wa kusimamisha wagombea nchi nzima? Hii ni ishara kwamba wanachama wa CHADEMA wanakata tamaa, hawana tena imani na chama chao, na wanatafuta uongozi bora wa kweli - ambao wanaupata katika vyama vingine vyenye ushawishi na nguvu kama CCM.
Takribani idadi ya wanachama wa CHADEMA nchi nzima inaonekana kuwa ndogo kiasi kwamba hata hawatoshi kuwania nafasi mbalimbali katika chaguzi hizi. Ni nani basi atawapigia kura? Inaonekana wazi kuwa hawana watu wa kutosha kuwawakilisha, na hivyo kupoteza ushawishi katika jamii.
CCM, Wanaona umuhimu wa kuwa na wagombea wenye nia ya dhati ya kuleta mabadiliko na ambao wapo tayari kuwatumikia wananchi kwa moyo mmoja. Uwezo wa kusimamisha wagombea kila kona ya nchi, CCM imedhihirisha uimara wake, na kutoa mwanga wa matumaini kwa Watanzania wanaotaka maendeleo.
Kwa mara nyingine tena, CHADEMA inaanguka na kuachia nafasi kwa CCM kuendelea kuimarika. Wakati wao unakaribia kwisha, na wanachama wao wanashindwa kuona mwelekeo wa matumaini ndani ya CHADEMA. Wanachama hawa sasa wanajiondoa na kujiunga na chama chenye ushawishi wa kweli (CCM) Hii ni ishara kuwa CCM bado ni kimbilio na tumaini la kweli kwa Watanzania wote.
Watanzania wote wanashuhudia, siku hadi siku, anguko la CHADEMA na nguvu ya CCM inayozidi kuimarika. Ni wakati wa CCM, chama chenye uwezo na dhamira ya dhati ya kujenga Taifa linaloendelea. Watanzania sasa wanapaswa kujiunga, kwa sababu kwa CCM, maendeleo ni uhakika!