Ushauri kwa IGP Sirro

Ushauri kwa IGP Sirro

Tunasikia tetesi na kelele za maandamano kwenye mitandao ya kijamii,bila kuelewa kamanda Sirro ameshaanza kuweweseka na kuanza kutoa matamko na makaripio kwa atakaeandamana kinyume cha sheria atakiona.

Ushauri kamanda Sirro wape kibali waache hao watu wenye kutaka kuandamana waende watakako cha msingi wape ulinzi na uwaeleze kabisa viongozi na waratibu wa hayo maandamano suala lolote litakalotekea kinyume na kusudio la maandamano basi wao ndio watawajibika,najua watanzania kama wataachia waende walikokusudia bila bughudha yeyote sidhani kama kutakua na uvunjifu wa amani.

Na tunawataka nanyi waandamanaji maana maandamano hubeba vibaka wa kupora basi kweli muwe na nia moja ya kufikisha ujumbe wenu sehemu husika na sio kuanza kuwachokoza polisi.

Angalizo kamanda Sirro ukiingiza intelejensia tu umeshaharibu najua askari wa kutosha unao na wanaweza kuwatuliza watu na amani ikarejea kama ilipotea

Wape kibali wajione wapo huru katika huru,utaandikwa kwenye vitabu vya kumbukumbu na historia!

Ni maandamano bila kikomo mpaka dikteta uchwara atoke
 
Magufuli anaogopa maandamano,mabomu ya machozi yatarindima kilakona kabla watu hawajajitokeza barabarani.
Hilo sio la kuuliza na ndio stahili yenu. Miguu itakayovunjwa isipungue 2000
 
Bila akishatoa hicho Kibali na akifukuzwa Kazi utakuwa unamkaribisha hapo Kwako kunywa nae Chai, chakula cha mchana na cha usiku pia Yeye pamoja na Familia yake nzima Mkuu.
Anaweza kufukuzwa hata bila ya kutoa hicho kibali inategemeana na mkulu kaamka vipi!
 
tapatalk_1519828232571.jpeg
tapatalk_1519828240205.jpeg
IMG-20180228-WA0008.jpeg
 
Hapa kipara kwa mara kwanza umetoa ushauri maridhawa kabisa. Tatizo ninaloliona kwa viongozi ni ile hali ya kukwepa ukweli ambao kwa sasa umeanza kukosa majibu na walitarajia na kuaminisha mambo makubwa sana. Mambo kama ya ajira, uminywaji wa demokrasia, uhuru wa vyombo vya habari, kudondoka kwa uchumi na biashara za watu. Haya mambo serekali haiko tayari kuona inaambiwa hadharani. Nashauri siku ya maandamano viongozi wa kisiasa wasiongee ili kuepusha kuonekana ni maandamano ya kisiasa kwani hapa pana shida kidogo. Bali viongozi wa dini na asasi za kiraia ndio waongee ili kufikisha ujumbe. Kwwnye maandamano hayo kusivaliwe sare za vyama, bali waandamanaji wabebe matawi ya miti na vitambaa vyeupe. Hapo serekali itajionea yenyewe ni kiasi gani inachofanya kinawagusa wananchi.
Kama kelele zimezidi kuna haja ya kutafakari na kuchukua maamuzi sahihi yenye maslahi kwa wote!
 
Tunasikia tetesi na kelele za maandamano kwenye mitandao ya kijamii,bila kuelewa kamanda Sirro ameshaanza kuweweseka na kuanza kutoa matamko na makaripio kwa atakaeandamana kinyume cha sheria atakiona.

Ushauri kamanda Sirro wape kibali waache hao watu wenye kutaka kuandamana waende watakako cha msingi wape ulinzi na uwaeleze kabisa viongozi na waratibu wa hayo maandamano suala lolote litakalotekea kinyume na kusudio la maandamano basi wao ndio watawajibika,najua watanzania kama wataachia waende walikokusudia bila bughudha yeyote sidhani kama kutakua na uvunjifu wa amani.

Na tunawataka nanyi waandamanaji maana maandamano hubeba vibaka wa kupora basi kweli muwe na nia moja ya kufikisha ujumbe wenu sehemu husika na sio kuanza kuwachokoza polisi.

Angalizo kamanda Sirro ukiingiza intelejensia tu umeshaharibu najua askari wa kutosha unao na wanaweza kuwatuliza watu na amani ikarejea kama ilipotea

Wape kibali wajione wapo huru katika huru,utaandikwa kwenye vitabu vya kumbukumbu na historia!
Yule aliyejipa(Siro ni figure head tu) kuwa IGP hawezi kukubali.

Ref; I wish I could be IGP, kilichofata ni Mangu kuwa out of office
 
Mkuu tindo mambo mengine muache siasa ,hatulisaidii taifa ,hapa unaeleza mawazo yako na hisia zako zote ,kwa maana unajieleza ,uhuru upi unaoutaka ?, wa kutukana na kudhalilisha wengine ?
Au tuwape uhuru kama wa libya ?, kwasasa wanasherekea uhuru walioutaka kwa raha zao mpaka basi.

Mkuu tindo uhuru huendana na ustaarabu wa jamii,watanzania ustaarabu hatuna
Huyo Tindo na wahuni wenzake ni watu wa hovyo sana katika jamii ya Watanzania mkuu.
Wana nia Ovu na mama Tanzania. Hawa Wahuni kutwa kupiga kelele katika mitandao ya kijamii na kuhamasisha uvunjifu wa Sheria na kanuni za nchi. Wanachochea machafuko wakati wao na familia zao wako Ughaibuni tuliii....sisi na familia zetu tutakuwa wageni wa nani azma ya hawa Wahuni itakapotimia!?

Hakika Libya wanasheherekea uhuru kwa sasa!
 
Ni rahisi jua kuchomozea magharibi kuliko huu ushauri wako kuzingatiwa. Period.
 
Kipara kashanywea hahahaha raia kazeni uzi
Mlipiga kelele sana mitandaoni ya kwamba mtakinukisha siku ya HUKUMU ya Sugu. Sugu amehukumiwa kwenda JELA miezi mitano na HAPAKUCHIMBIKA wala Kubonyea! Bladibastaadi.
 
Back
Top Bottom