Nilijua tu , haraka haraka zile za makundi mbalimbali wengine wakijiita wanaharakati alikuwa ni CDM tu. Afadhali sasa mmejitokeza wazi na kuonesha hizia zenu kuwa Dr Ulikuwa alikuwa akiyafanya hayo kwa Maslahi ya Chama. Hivi watanzania wajinga kiasi gani watakaochagua chama cha siasa kinachopandikiza chuki miongoni mwa wananchi wake kama CDM?Wana JF,
Nimefikiria sana juu ya mustakabali wa Dr. Ulimboka mara Mungu atakapomjalia afya njema na akarejea nyumbani.
Japo sijui msimamo wake binafsi na familia yake, reaction ya serikali (badala ya kujibu hoja) ya KULIFUNGIA KWA MUDA USIOJULIKANA GAZETI LA MWANAHALISI lililofichua mpango mzima (na wahusika wakuu) wa kukamatwa kwake,kuteswa na hatimaye kutupwa katika msitu wa pande wakidhani angekufa tu kunadhihirisha mambo mawili makubwa.
Mosi serikali ndiyo iliyohusika na unyama aliofanyiwa Ulimboka;
La pili, kwakuwa hajafa till now,hayuko salama.
Ushauri:
Hukohuko aliko,arejee maelezo yake juu ya unyama aliofanyiwa kwa undani na ufasaha na yahifadhiwe kwenye formats mbalimbali na yasambazwe kwenye vyombo vyote vya habari (vya ndani na nje) kwa ajili ya kumbukumbu. Na mara tu atakaporejea nyumbani afanye press conference juu ya tukio lake na pia kutangaza kuacha kazi serikalini.
Kama anaweza siasa ajiunge na chama cha upinzani. Kwenye uchaguzi ujao atapata kura za kishujaa.
Wana JF mnasemaje?