Ushauri kwa Dr. Steven Ulimboka: Usifanye kosa la "Kukuingiza kaburini"

Naamini Dk Uli hataki kuweka maisha yake rehani hana wafuasi katika sekta ya udaktari anapigana peke yake mwacheni apumzike .... ukienda kaburini haurudi.
 
Sio kweli, ULIMBOKA kaa kimya. Tena tamka kuwa huna haja ya kuwasema waliokuteka ikiwa tu huna uhakika na kuwatambua kwao. Usihisi wala usilishwe maneno kuwa waliofanya hivyo ni fulani. Kama unauhakika unawajua waseme lkn hapo utakuwa unajiweka katika hatari zaidi maana hao wanaokushauri hawatakupa ulinzi wowote watakuwa pembeni kama wanavyoficha majina yao kwenye JF. Minaona kusamehe na kuachana na yote yaliyopita ni salama kwako na familia yako kuliko kutaka kufanya vita na adui usio jua idadi yao.
 
mkuu! ndo imetoka hiyo, hakuna usemi tena hapo!

Weweeee...Wanyakyusa wa Kyela huwajui! Hii ngoma bado mbichi sana; ipo juani inakaushwa saa hizi. Ikishakauka lazima utasikia mlio tu! Nipo hapa....
 
Mimi namshauri dr.Ulimboka hivi kila jambo unaloliona zuri lina "risks" zake. Mambo yaliyokupata ni wazi kabisa kwa mtu anayejiuliza ataendelea kujiuliza!-"all that night, What kind of negotiation was that". Nadhani ulikuwa motivated kwenda kupata mshiko. Lkn ndio hivyo, dili likasanuka. kubali yaishe.
 
[h=2]21 August 2012[/h] [h=3]Ulimboka aibukia kanisani Ubungo *Atoa sadaka maalumu, awashukuru Watanzania *Adai unyama aliofanyiwa anamuachia Mungu[/h]

Stella Aron na Rehema Maigala

HATIMAYE Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt.Steven Ulimboka, ameibuka na kusema kitendo cha kinyama alichofanyiwa na watu waliomteka anamuachia Mungu.

Dkt.Ulimboka aliyasema hayo Dar es Salaam juzi alipokwenda kutoa sadaka ya shukrani na familia yake kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo.

Katika ibada hiyo, Dkt.Ulimboka ambaye pia alisindikizwa na ndugu zake wa karibu, alimshukuru Mungu kwa kumpigania maisha yake na kurudi salama, madaktari wenzake na Watanzania wote kwa maombi yao ambayo yamemwezesha apone haraka.

Kabla ya kutoa sadaka maalumu, Dkt. Ulimboka aliomba kusomewa kitabu cha Zaburi 124 isemayo; “Kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, Israel na aseme sasa, kama si Bwana aliyekuwa pamoja nasi, wanadamu walipotushambulia, wangalitumeza hai”

“Hasira yao ilipowaka juu yetu, papo hapo maji yangalitugharikisha, mto ungalipita juu ya roho zetu, papo hapo yangalipita juu ya nafasi zetu yafurikayo”

“Na ahimidiwe Bwana, asiyetutoa kuwa mawindo kwa meno yao, nafasi yetu imeokoka kama ndege katika mtego wa wawindaji, mtego umevunjika nasi tumeokoka, msaada wetu u katika jina la Bwana aliyezifanya mbingu na nchi”

Baada ya kusomwa ujumbe huo, Mchungaji wa kanisa hilo Godlizen Nkya Mkaya, alimwongezea sura nyingine ya Zaburi 44, kuanzia mstari wa kwanza hadi wa saba na kusomwa kanisani hapo.

Baadhi ya maneno ya sura hiyo yalisema; “Ee Mungu tumesikia kwa masikio yetu, Baba zetu wametuambia matendo uliyoyatenda siku za kale, wewe kwa mkono wako uliwafukuza mataifa ukawakalisha wao”

“Maana si kwa mkono wao walivyoimiliki nchi wala si mkono wao uliowaokoa, bali mkono wako wa kuume, Mungu wewe ndiwe mfalme wangu, uagize mambo ya wokovu kwa Yakobo”

“Kwa nguvu zako tutawaangusha watesi wetu, kwa nguvu zako tutawakanyaga watupingao, maana sitautumaini upinde wangu wala upanga wangu hautaniokoa bali wewe ndiye uliyetuokoa na watesi wenu na watuchukiao umewaaibisha,”

Baada ya ujumbe huo, Dkt. Ulimboka alisema yeye anamshukuru Mungu kwa kumponya na hana neno lingine zaidi ya hilo.

“Sina cha kusema kwa jinsi ambavyo Mungu amenitendea wema wake hivyo yote namuachia Bwana,” alisema Dkt.Ulimboka ambaye hakupenda kuzungumzia zaidi tukio lililomkuta.

Katika ibada hiyo, pia kulikuwa na uzinduzi wa CD ya kwaya ya Uinjilisti Kanani ambapo Dkt.Ulimboka, alinunua CD hiyo yenye nyimbo 10 kwa sh. 300,000.
 
[h=2]21 August 2012[/h] [h=3]Ulimboka aibukia kanisani Ubungo *Atoa sadaka maalumu, awashukuru Watanzania *Adai unyama aliofanyiwa anamuachia Mungu[/h]

Stella Aron na Rehema Maigala

HATIMAYE Mwenyekiti wa Jumuiya ya Madaktari nchini, Dkt.Steven Ulimboka, ameibuka na kusema kitendo cha kinyama alichofanyiwa na watu waliomteka anamuachia Mungu.

Dkt.Ulimboka aliyasema hayo Dar es Salaam juzi alipokwenda kutoa sadaka ya shukrani na familia yake kwenye Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Usharika wa Ubungo.

Katika ibada hiyo, Dkt.Ulimboka ambaye pia alisindikizwa na ndugu zake wa karibu, alimshukuru Mungu kwa kumpigania maisha yake na kurudi salama, madaktari wenzake na Watanzania wote kwa maombi yao ambayo yamemwezesha apone haraka.
 
Wakishapona sijui wanasahau? nakumbuka jinsi Mwakyembe alivyoahidi "kuyasema yalo moyoni mwake" hadi leo kimya, ameishia kupanda treni Dar- Dom na kuwaita waandishi wa habari wampige picha akiwa safarini. Tz ni zaidi ya tuijuavyo!
 
nahisi kama ashaahidiwa mijisenti ya kumfunga mdomo vile
afu hatazila amalize kabla ya kumaliziwa kabisa
tumwache atafakari kama atazichukua ama la.
msiposikia kauli mjue mambo tayari keshazikamata

Unajua usifikiri kila mtu anafikiri kama wewe lazima ulitambue hili kwanza wakati unaandika na si ku generalize mambo pasi na sababu za msingi

UNAFIKIRI KAMA ANGEKUWA NA TAMAA KAMA ZENU NYIE WENGI CHEAP BEING YALIYOMPATA YANGEMKUTA?

KWA FIKRA ZANGU FUPI SUALA LA KUPEWA PESA LILIPITA KITAMBO NA BAADA YA KUSHINDIKANA NDIO MAJAMAA YAKACHANGANYIKIWA HADI YAKASHINDWA KU EXECUTE ORDERS CALMNESSLY...
UNAFIKIRI HAO JAMAA UNASEMA WANATOA PESA WANGEFANYA WALIYOYAFANYA? THINKKKK....
 
Dr Ulimboka ni heri aeme maana hata asiposema haisadii kitu. Ni bora akasema maana kutokusema wale jamaa wa TISS watakuwa wanamtafuta!
Hahaha mmeashaanza kumkana ULIMBOKA? hahaha ngoja akifunguka ndio mtamkana zaidi hahaha
 
Weweeee...Wanyakyusa wa Kyela huwajui! Hii ngoma bado mbichi sana; ipo juani inakaushwa saa hizi. Ikishakauka lazima utasikia mlio tu! Nipo hapa....

mwakyembe ni mnyakyusa wa china? wewe ndounasema ivyo kwakuwa hayajakukuta! kwa kifupi dr hatosema tena kuhusu ishu yake, zaidi ya kuishia kanisani na kumuachia mungu tu. sema kwa kuwa wabongo nyinyi ni washabiki na mnataka hbr za kuuzia magazeti bila kuangalia upande wa pili wa shilingi kipi kinaweza kumkuta mwenzenu, basi ndo maneno yenu tu hayo.hata yeye anaakili anajua kipi kinaendelea mpaka sasa, awezi kufanya kama mnavyotaka nyinyi, alivyotupwa mabwepande mlisaidia nini zaidi ya kuishia kupiga kelele tu humu jf, acha wewe asikwambie mtu, haya yaliomkuta dr ni mazito, sema kwa kuwa wewe ni mtoto mdogo huwezi kujua haya!
 
kutokuhongeka mara ya kwanza hakuzuii second attempt
dau laweza kuwa kubwa zaidi
na atapewa option 2 kupokea au kukaa kimya
lets wait and see kama ataongea
then you will prove me wrong
Unajua usifikiri kila mtu anafikiri kama wewe lazima ulitambue hili kwanza wakati unaandika na si ku generalize mambo pasi na sababu za msingi

UNAFIKIRI KAMA ANGEKUWA NA TAMAA KAMA ZENU NYIE WENGI CHEAP BEING YALIYOMPATA YANGEMKUTA?

KWA FIKRA ZANGU FUPI SUALA LA KUPEWA PESA LILIPITA KITAMBO NA BAADA YA KUSHINDIKANA NDIO MAJAMAA YAKACHANGANYIKIWA HADI YAKASHINDWA KU EXECUTE ORDERS CALMNESSLY...
UNAFIKIRI HAO JAMAA UNASEMA WANATOA PESA WANGEFANYA WALIYOYAFANYA? THINKKKK....
 
Sijafuatilia sana ya Mwakyembe ndugu. ILA maandiko yako yanaonesha wewe ni mtu mwenye huruma sana. Na katika kuona huruma nakuunga mkono. Ila tu bahati nzuri au mbaya ni kwamba habari za Ulimboka zipo zaidi ya sehemu moja. Kwa hiyo hata kama angetaka yaishe, siasa za Tanzania hazitaruhusu yaishe. Habari zitakuja kutoka tu. TISS na Zoka wao wamelikoroga hili watalinywa tu... ingawa nionavyo mimi victim mkubwa katika hili atakuwa CCM kwenye uchaguzi. They are going to pay a very high price kule Kyela.

mwakyembe ni mnyakyusa wa china? wewe ndounasema ivyo kwakuwa hayajakukuta! kwa kifupi dr hatosema tena kuhusu ishu yake, zaidi ya kuishia kanisani na kumuachia mungu tu. sema kwa kuwa wabongo nyinyi ni washabiki na mnataka hbr za kuuzia magazeti bila kuangalia upande wa pili wa shilingi kipi kinaweza kumkuta mwenzenu, basi ndo maneno yenu tu hayo.hata yeye anaakili anajua kipi kinaendelea mpaka sasa, awezi kufanya kama mnavyotaka nyinyi, alivyotupwa mabwepande mlisaidia nini zaidi ya kuishia kupiga kelele tu humu jf, acha wewe asikwambie mtu, haya yaliomkuta dr ni mazito, sema kwa kuwa wewe ni mtoto mdogo huwezi kujua haya!
 
Sijafuatilia sana ya Mwakyembe ndugu. ILA maandiko yako yanaonesha wewe ni mtu mwenye huruma sana. Na katika kuona huruma nakuunga mkono. Ila tu bahati nzuri au mbaya ni kwamba habari za Ulimboka zipo zaidi ya sehemu moja. Kwa hiyo hata kama angetaka yaishe, siasa za Tanzania hazitaruhusu yaishe. Habari zitakuja kutoka tu. TISS na Zoka wao wamelikoroga hili watalinywa tu... ingawa nionavyo mimi victim mkubwa katika hili atakuwa CCM kwenye uchaguzi. They are going to pay a very high price kule Kyela.

mkuu! asikwambie mtu, uhai unatafutwa sana skuizi, we uoni watu wanavyojazana mahosptalini! alafu isitoshe huyu dr alishalibeep kaburi, siri za dr haziwezi kuvuja tena kwakuwa tayari zilishavuja na watu wanatambua wazi kipi kiliendelea na kinaendelea kumuhusu dr na yaliomkuta,sasa hata yakiwekwa wazi ni kwamba watakuwa kama wanahalalisha tu habari lakini si kutujuza watu gani wahusika! ki ukweli dr hawezi litamka hilo ng'o nae anakawoga, yale maneno ya sikuile airport yalikuwa ni ujasiri na furaha ya kurudi nyumbani akiwa mzima na afya, kama angekuwa ni msemaji, angelisha sema zamani sana na tungekuwa tumeshasahau kuwa kasema humu jf!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom