Ushauri kwa Diamond: Mpe Mji Harmonize, Kashapevuka

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
2,475
2,000
Habarini za muda huu wana jf.

Imefika wakati sasa wa nyumba ya WCB kupata miji mingine, watoto wameshakua vya kutosha haifai waendelee kuishi na baba yao wakati wote wananyoa ndevu. Diamond nakushauri tuu wape wanao miji na wao waweze kuendeleza kizazi ulichoanzisha wewe. Au hutaki kupata wajukuu? Jitahidi sana wape hao wanao miji ili uweze kupata wajukuu, ikiwezekana hata vitukuu kabisa.

Sote tunafahamu kwamba nyumba siku zote inacompose baba, mama na watoto. Baada ya muda hawa watoto wakishakomaa basi na wao huwa wanaanzisha familia zao (miji). Lakini haimaanishi kwamba hawa watoto ndo wamejitenga na baba na mama zao bali ni nature tuu iliyopo.

Siku zote unapokuwa kiongozi wa label ya muziki itafika mida kuna watakaofika level zako ww kama kiongozi, na endapo utajifanya kuwang'ang'ania basi jua umeshika bomu ambalo linaweza kukulipukia muda wowote.

Usifanye makosa waliyofanya viongozi wako kina Babu Tale na Mkubwa Fela kipindi wako na makundi ya Tiptop Connection na TMK Wanaume Family respectively.

Hawa majamaa waliwalea wasanii wao vzr san kimuziki enzi hizo na kuwapeleka kileleni, lakini kosa walilofanyaga ni kutotaka kuwe na muendelezo wa vizazi. Walitaka wao ndo wawe kizazi cha mwisho wakati wasanii wao walishapevuka na kufika level za kuwa na miji yao.

Kwa hiyo usirudie kosa, wape uhuru vijana wako waliokomaa hasa Harmonize wakajitengenezee miji yao. Haimaniishi uwavunjie mikataba, la hasha. Endelea kuwa close nao. Wewe ni babu wa watoto wao i.e wajukuu zako. Hivyo hao wajukuu pia watakuwa faraja kwako pindi watakapokuwa wanakuja kukutembelea hapa na pale.

Ni hayo tuu kwa sasa.
 

Joseverest

Verified Member
Sep 25, 2013
42,826
2,000
Jamaa sijui kama atakusikia kwa maana ule msemo wa pata pesa tujue tabia zako umewakaa sana


Sent from my iPhone using JamiiForums
 

Mapensho star

JF-Expert Member
Jun 30, 2016
2,240
2,000
Aongeze chipukizi hao wakubwa awatoe inje

Sent using Jamii Forums mobile app
Kila biashara inataratibu zake ngumu kupata vijana waaminifu mfano rich mavoko kajitoa kabla hata kampuni haijatengeneza faida na kiukweli diamond anatake risk sana anaangalia faida mbeleni uwekezaji wa harmonize pengine haujarudisha faida sababu bado hajafanikiwa kuwa balozi wa kampuni yoyote na pesa ipo kule
 

Dong Jin

JF-Expert Member
Jun 4, 2018
338
1,000
harmorapa aaah sory harmonize bila mond namwona huyo kule chitoholi analima mikorosho
 

Viol

JF-Expert Member
Dec 15, 2009
22,080
2,000
Harmoze hawezi bila wasafi hasa Diamond,hata tour za kimataifa itakuwa ngumu kuzifanya, kuna mwenye vision na pesa,Harmonize hata kama ana pesa bila vision kama ya diamond hatafika mbali.
 

MoudyBoka

JF-Expert Member
Dec 31, 2011
906
1,000
Harmoze hawezi bila wasafi hasa Diamond,hata tour za kimataifa itakuwa ngumu kuzifanya, kuna mwenye vision na pesa,Harmonize hata kama ana pesa bila vision kama ya diamond hatafika mbali.
Comments kama hizi ndo zitakazomfanya Harmonize atoke wasafi ili kuthibitisha sasa amekua na anaweza kusimama mwenyewe
 

Kingsmann

JF-Expert Member
Oct 4, 2018
2,475
2,000
Hatimaye kijana kaamua kujitengenezea mji wake baada ya dingi kugoma kumpa uhuru kabisa.

Developmental milestones.


 
Top Bottom