tamimusalim
JF-Expert Member
- Jun 17, 2014
- 1,822
- 499
Jamani mimi nina mke wangu nampenda sana toka tumeowana ni miaka 7 sasa ,tulianza na maisha magumu sana tunamshukuru mungu amefungua riziki leo tuna maisha mazuri sana.
Tumefanikiwa kujenga nyumba 4 na kupata watoto 3 ukweli tuna mshukuru mungu,pia tumefungua biashara nyingi tu ingawa bado ni wafanyakazi wa serikali ya Tanzania.
Licha ya gari ya ofisini kwa upande wangu namiliki toyota landcruser v8 mali yangu binafsi hapo ndipo nae mke wangu nilipoamua kumnunulia gari yake ya kutembelea sasa toka nimemnunulia iyo gari aina ya toyota RAV4, amelisusa na halitaki kabisa yeye anataka SUBARU FORESTAR TURBO STI ambayo iyo juu pichani mimi nimemkatalia hii gari kwanza inakimbia sana pia linakula mafuta sana hebu nisaidieni maana hata unyumba sipati nina wiki sasa.