Ushauri kuhusu mkopo wa gari

Kwa ushauri tafuta Collora XE/SE 110 au Collora Filieder ZNE Vvt i ni gari zinatumia mafuta kidogo (CC 1500) kulinganisha na gari kama Premio (CC 1800- 2000). Spea zake zinapatikana kwa wingi bila shida kifupi Nairobi haitakuhusu kabisa.
Taratibu za Exemption ni hizi:-

  • Mshahara wako uaanzie TGSD (kwa wewe ume qualify)
  • Kodi zinazo samehewa ni Import Duty (25% ya CIF) na Execise dut(5% kwa gari zenye CC (0-1500) na 10% kwa gari zenye (CC 1501- ). Uchakavu hausamehewi na ni 20% kabla ya VAT(18%). Uchakavu ni kwa magari yote yalitengenezwa zaidi ya miaka kumi, hivyo ukiagiza gari la mwaka 2001 kwa saizi hadi lifike litakuwa tayari limeshamaliza miaka kumi toka kutengenezwa hivyo uchakavu ni lazima ukuhusu.
  • Unaandika barua kupitia mwajiri wako kwenda Sub Treasury baada ya kujazwa fomu toka TRA ambayo inajieleza. Viambatanisho katika barua hiyo ni Salary Slip (Current), barua ya kupandishwa cheo kama ulikuwa hujafikia daraja hilo, TIN namba.
  • Gari liwe kwa matumizi ya kawaida na siyo biashara.
Kifupi huo ndiyo utaratibu lakini unahitaji ufatiliaji kidogo.
Kama unataka kukopa ni bora ukakope kwenye bank/ SACCOS (kama mnayo kwa minajili ya riba) kuliko kwenda kwenye makampuni yanayouza magari watakupiga riba kubwa sana.
Ushauri wa mwisho, kabla ya kukopa hakikisha umesave angalau 1.6m -2.0m ili ujazie hicho kiasi kingine na ubakie hata na salio kidogo la kulihidumia gari hilo kwa kuweza kulipa motorvehicles license na mingeneyo ya barabarani.
Kila la kheri katika safari yako ya kutaka kutembea huku UMEKAA.
 
Daladala ni shida wazee, unyunyu wote unaisha ukitoka unanuka mchanganyiko wa pafyumu na vikwapa
me nakushauri uchukue ka-starlet ndugu yangu kanaserve the purpose, na hako kampunga kalivyo kaduchu utamudu tu.
SWALI KWA WANAJF: kati ya CAMI(TOYOTA) na TERRIOS(DAIHATSU) ipi bora coz naona zinafanana ila sijajua ki-maintenance na spares ziko vipi, naomba msaada wenu kabla sijaangukia pua.
 
Mimi nakushauri ukope pesa bank ya wanawake, kukopa gari si rahisi itakugharimu sana afadhali kukopa fedha..
 

mkuu una uhakika ?mbona huu mkopo unaonekana rahisi sana!
 

nimeupenda sana ushauri wako, umejaa busara , hekima na weledi wa hali ya juu sana.
 

Kamata tuktuk tu mwisho wa matatizo. Itaendana na kipato chako.
Ukiweka wese la buku 5 unazunguka round 4
Gari kwa sasa mafuta bei juu lt1=2000 ambapo kwa wiki utatumia mafuta si chini ya 80,000 pamoja na misele yako ya hapa na pale kwa mwezi piga hesabu hapo na kipato chako ni hiyo kilo 4 + na makato ya kwenye mkopo utajikuta unapokea take home chini ya laki 4 aangalia usije ukalipaki ukawa unatembelea week end tu kwa ajili ya maumivu ya mafuta.
 

Hapo kwenye red ndo huwa nachanganyikiwa nashindwa kuelewa which is which. Kama raum, corrola na starlet zinatumia engine aina moja iweje ziwe na cc tofauti? Mfano raum zina cc 1500 na starlet cc 1300. ufafanuzi please
 
we bado uko very naive aisee, aliyekwambia ukilipwa laki nne ndo huwezi kuendesha gari mjini nani? hizo laki nne ni zinazoingia benki kila mwezi kama mshahara uliowekwa na serikali lakini in reality watu wana link za pesa nyingi tu huko serikalini kuliko huku private, unakuta ndani ya mwezi ana semina ya wiki mbili nje ya mkoa, mara kaenda swaziland training kwa miezi 2, marra sitting allowence, so usiogope mkuu, pesa ipo ndo maana akasema anawezakatwa hata laki tatu out of laki nne, au labda ana miradi yake inamlipa zaidi kuliko kazi.
 
Hata mimi nasubiria jibu. Ila CAMI naona bei juu.. Tusubiri wataalam
 
Huyu anahitaji mkopo wa Gari...

Hivi kuna huduma hizo hapa TZ? Nahisi hilo gari by the tym unamaliza kulilipia inakuwa kama umenunua magari mawili

Nenda Conti-cars opposite na holiday inn mpya, walishawahi kuniambia wanafanya mikopo ya aina hiyo ila ni lazima wamshirikishe mwajiri na pia unasettle down payment hiyo nyingine ndio wanachanja taratibu...of course with high interest.
 
nitafute nikupe carina ya 2002 bei ni milioni nane unatoa asilimia 60 ya hiyo pesa alafu kila mwezi utakuwa unanipa laki tano
 
nitafute nikupe carina ya 2002 bei ni milioni nane unatoa asilimia 60 ya hiyo pesa alafu kila mwezi utakuwa unanipa laki tano

hii nimeipenda sana je umeinunua lini na umeanguka/kugongwa mara ngapi?
 

mkuu namie nisaidie hapa; gari 1500cc ya mwaka 2000, FOB 2600USD, Je nikitaka kuinunua itani cost tsh ngapi mpa inaingia barabarani?
 
kweli bana. muerezee
 

Impressive!
Inafurahisha mtu anayeelewa jambo anapochangia.Being a professional in my own field niko impressed mzee.
Thanks.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…