Hongera mkuu kwa kuamua kujikwamua. Ila pole pia kwa mihangaiko.
Kotokana na kipato ulichoweka hapo juu, ningekushauri utafute gari isiyozidi 1500cc kwa sababu zifuatazo.
1) Ushuru wa TRA (Road License) ni nafuu kwa gari ndogo < 1500cc
2) Uta-save pia kwenye mafuta. Matumizi makubwa ya gari yapo kwenye mafuta, na sio service wala spea.
3) Service ya engine ndogo ni bei ndogo sana, tofauti na engine kubwa.
Kwa collora Premio, sijawahi ona yenye engine ya 1500cc, ila nafahamu ipo ya 1600cc na ulaji wake wa mafuta ni mzuri sana. Spea pia zipo na bei ni nafuu sana. Ila kuna Premio za 2000cc, hizo sifahamu utumiaji wake wa mafuta ukoje, labda mdau mwingine atufahamishe.
Ila pia, unaweza jaribu Toyota Raum, ni 1500cc na utumiaji wa mafuta ni mzuri. Spea pia zipo nyingi na bei ni nafuu. (In fact, Raum inatumia spea za corrolla, na engine yake ni ile ile ya Toyota Starlet)
Mambo mengine ya jinsi ya kupata mkopo, ngoja tusubiri wadau tuone wanalipi la kuchangia.