Ushauri kuhusu mkopo wa gari

Uda

JF-Expert Member
Nov 27, 2010
811
624
Habari wanajf;
mimi ni mtumishi wa umma na kipato changu ni Tsh 400000/=(take home)
nataka kukopa mojawapo ya gari hizi forester/ suzuki escudo/corona premio.
Naomba ushauri kama kuna sehemu naweza kupata mkopo wa aina hiyo(achilia mbali kukopa fedha taslimu kutoka bank)
msaada jamani nshachoka kupanda dala dala.
 
mimi naomba nikushauri kwenye gari.....kamata corona premio.....forester mmmmmh...no...suzuki sina uhakika
 
Tafuta corola limited itaendana sana na kipato chako hasa katika fuel consuption and spare parts zake ni nafuu sana. Achana na Escudo maana spare ziko juu na kupata ambayo iko order kwa sasa si chini ya Mill 6..
 
Ahsante kwa kuomba ushauri wa jambo hili, mimi nami nasubiri ushauri huo niufanyie kazi kwani nina shida hiyo na pia hata kwa vipato twafanana, naomba pia wana forum wenye uzoefu wa process za kupata exception ya kodi kwa watumishi wa umma atusaidie ushauri tafadhali.
 
mimi naomba nikushauri kwenye gari.....kamata corona premio.....forester mmmmmh...no...suzuki sina uhakika

hapo kwenye forester mbona umeguna,tatizo ni bei,spea au unywaji wa fuel?
 
Tafuta corola limited itaendana sana na kipato chako hasa katika fuel consuption and spare parts zake ni nafuu sana. Achana na Escudo maana spare ziko juu na kupata ambayo iko order kwa sasa si chini ya Mill 6..

thanks kwa ushauri .
 
May be we should ask a fundamental question.
Out of your take home salary of Tshs 400,000/= how much are you ready to spend on the car?
you can then split the sum onto 3 parts; loan re-payment, services and maintenance; insurance, road tax, etc. and fuel
 
nina uwezo wa kulipa 300000/=
kwa mwezi.
 
Habari wanajf;
mimi ni mtumishi wa umma na kipato changu ni Tsh 400000/=(take home)
nataka kukopa mojawapo ya gari hizi forester/ suzuki escudo/corona premio.
Naomba ushauri kama kuna sehemu naweza kupata mkopo wa aina hiyo(achilia mbali kukopa fedha taslimu kutoka bank)
msaada jamani nshachoka kupanda dala dala.

duh ebana yaani we unaingiza 400000 na unataka kulipa laki 3 kila mwezi kwa ajili ya gari au we ni kafisadi flani hv kuna sehemu unataka kuwa unachota fwedha,maana haingii akilini kubaki na matumizi ya laki 100000 kwa mwezi,otherwise utuambie kipato chako halisi,kama ni laki 4 ni bora uvumilie na daladala mpaka uwezo utaporuhusu la sivyo lazima ije kula kwako tu
 
Usipate tabu nenda nabarua kutoka kwa mwajiri wako ipeleke benki ya wanawake utapewa mkopo bila rongorongo!!
 
Usipate tabu nenda nabarua kutoka kwa mwajiri wako ipeleke benki ya wanawake utapewa mkopo bila rongorongo!!

Huyu anahitaji mkopo wa Gari...

Hivi kuna huduma hizo hapa TZ? Nahisi hilo gari by the tym unamaliza kulilipia inakuwa kama umenunua magari mawili
 
hivi hii bank ya wanawake inakopesha wanaume?afu mikopo yao si inahusiana na ujasiliamali.

Wanatoa mkuu kama nikuhusu mikopo ya gari aende ACB Banki wanatoa mikopo ya magari,nyumba ila kwa maelezo yakina aende huko watampatia zaidi terms nizile lazima uwe na granta,hasa mwajiri!!
Namkopo wowote ujue unalipa mara moja nanusu!!kwani kunakitukinaitwa risk loan insurace!!
 
duh ebana yaani we unaingiza 400000 na unataka kulipa laki 3 kila mwezi kwa ajili ya gari au we ni kafisadi flani hv kuna sehemu unataka kuwa unachota fwedha,maana haingii akilini kubaki na matumizi ya laki 100000 kwa mwezi,otherwise utuambie kipato chako halisi,kama ni laki 4 ni bora uvumilie na daladala mpaka uwezo utaporuhusu la sivyo lazima ije kula kwako tu

ikiwezekana hata kula nyasi lakini gari lipatikane.sio kila kitu ufisadi jamani.
 
Hongera mkuu kwa kuamua kujikwamua. Ila pole pia kwa mihangaiko.

Kotokana na kipato ulichoweka hapo juu, ningekushauri utafute gari isiyozidi 1500cc kwa sababu zifuatazo.

1) Ushuru wa TRA (Road License) ni nafuu kwa gari ndogo < 1500cc
2) Uta-save pia kwenye mafuta. Matumizi makubwa ya gari yapo kwenye mafuta, na sio service wala spea.
3) Service ya engine ndogo ni bei ndogo sana, tofauti na engine kubwa.

Kwa collora Premio, sijawahi ona yenye engine ya 1500cc, ila nafahamu ipo ya 1600cc na ulaji wake wa mafuta ni mzuri sana. Spea pia zipo na bei ni nafuu sana. Ila kuna Premio za 2000cc, hizo sifahamu utumiaji wake wa mafuta ukoje, labda mdau mwingine atufahamishe.

Ila pia, unaweza jaribu Toyota Raum, ni 1500cc na utumiaji wa mafuta ni mzuri. Spea pia zipo nyingi na bei ni nafuu. (In fact, Raum inatumia spea za corrolla, na engine yake ni ile ile ya Toyota Starlet)

Mambo mengine ya jinsi ya kupata mkopo, ngoja tusubiri wadau tuone wanalipi la kuchangia.
 
tafuta toyota starlet au vitz.ndio gari za vipato vyetu vya level hiyo.tena sisitiza upate yenye engine aina ya v.v.t-i. ni nzuri sana hizi engine kwa power na fuel consumption.ukubwa wa vitz au starlet ni kati ya cc 900 na 1200.ni ndogo lakini utaenjoy kua na gari kuliko escudo au forrester ambayo utajikuta unalazimika kuizima kwenye foleni ili kuokoa mafuta
 
duh ebana yaani we unaingiza 400000 na unataka kulipa laki 3 kila mwezi kwa ajili ya gari au we ni kafisadi flani hv kuna sehemu unataka kuwa unachota fwedha,maana haingii akilini kubaki na matumizi ya laki 100000 kwa mwezi,otherwise utuambie kipato chako halisi,kama ni laki 4 ni bora uvumilie na daladala mpaka uwezo utaporuhusu la sivyo lazima ije kula kwako tu
acha fujo unauliza ufisadi nchi hiii! ni sawa na anaeuliza eeeti kwani Dr Slaa aliibiwa kura wakati inaonekana live!
 
Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom