Ushauri kuhusu ku-apply vyuo vikuu 2016/2017

yaa labaratory kadhaa zipo muhasi, IT ni information technology, mambo ya kutengeneza application kibao unazoziona app store n.k, graphics design na websit creation ya ina mambo mengi for more info andika google IT carrier utaona application zake
Tofauti na MUHAS medical labaratory inapatkana chuo gan kingne?
 
nashukuru kwa ushirikiano wako
poa God bless kwa kua umefaulu usipaniki relax halaf angalia upepo unavyovuma sasa ukiona watu wengi sana wameomba chuo unachoomba wewe usijali sikilizia utaweza pata bahati yako.
pia ukiona idadi imekua kubwa tafuta chuo ambacho unajua huwezi kosa idadi ya waombaji ni wachache na nina kkuhakikishia utapata
 
ndio huwezi omba kozi moja mara mbili kwa chuo kimoja hiyo haifai. unaweza omba kozi mbili kwa vyuo viwili tuu na usizidishe.
pia unaruhusiwa kuomba sii chini ya vyuo vitatu na pia si zaidi ya vyuo vitano
lakini koz moja kwa vyuo vi2 tofauti naruhusiwa!
NB usinichoke kwa maswali yangu.
 
Yeah. Unashangaa nn wakati ma profesa karibu wote wanafanya kazi za siasa. Sasa mentors watakuwa nani?! Wakati salim said bakhresa hana class na ana drive life atakavyo. Ndio tulivyo kama nchi!

Pamoja na makosa ya hao waliotutangulia sio suala la kulifurahia hata kidogo kwa kijana wa kidato cha sita kua hajui aende wapi. Hili suala la kwenda kusoma chuo kikuu sio la ghafla, tangu akiwa kidato cha tano anatakiwa awe anajua ni nini atasoma na awe na options zaidi ya moja endapo ya kwanza ikifeli (kutokana na matokeo kuja kinyume na matarajio pengine) inayofuata inapandishwa daraja. Mtu anaweka matokeo yake tu hapo anasubiri ushauri, hasemi anapenda nini, alitaka kuwa nani au kufanya kazi gani au kujiajiri katika nini...... Ingekua na tija zaidi mtu akisema jamani ni nini potential ya mtu kusoma kozi fulani na vitu kama hivyo.
 
Mbona hamnijibu nishaurin chuo cha kuomba Math C phyE ChemE point 4 zimefika mnashauri kozi na chuo gani?
 
Mkuu sijaelewa
ishu ya utapeli. usijekuwa ni tapel ukaliza watoto maana mtz akishasikia kwenda nje ya nchi huwa anapagawa. sasa usjetumia mwanya huo kutapeli watu!!
 
unawezaje kujua watu waliomba kozi flan kwenye chuo flan n wengi? au wachache?
 
Tofauti na MUHAS medical labaratory inapatkana chuo gan kingne?
naweza kukwambia UDSM ila sina uhakika suburia hiyo guide book wakiitoa utaangalia, udsm nahis kama wanatoa ila sina uhakika. na kwa cbg yako hupati wala usipoteze mda boy fanya plan b. kuwa confident mambo ya kawaida haya. PCB ndo habari ya mjini.
ila sababu wewe unapenda labu jaribu kuomba imtu au kampala huko unaweza pata ila kampata kuna ukakasi ila sababu magufuli yupo na imani mambo yatakua shwari tuu
kampala ina mgogoro mingi sana na unaweza toka hapo kapa na baraza la ufamasia, udaktar na maabara naskia walikua hawakitambui so graduates kibao walivyomaliza hwakuajiriwa na ada ni kubwa saa miliion 6 na pesa kadhaa so kabla ya kufanya maamuzi fanya uchunguzi kwanza ujiridhishe.
 
yaan ushauri ume exhaust wote kuhusu huyu mtoto. hakuna nyongeza hapo. yeye atekeleze tu
 
NIT hiyo kozi inaushindani sana, yani hapo hadi pcb, pcm, pgb, cbg, egm, hge na kombi zote kavu wanaruhissiwa kuomba na si unajua tena science inapewa kipaumbele. atleast ungekua umesoma hge na una divsin two ningeweza kukushauri omba. ila kweli transpot and logistic huipati kwa kozi yako.
fanya plan b
 
hapana ndio nakuambia wanaifanyia marekebisho, kama wanavyofanyaga hii tumeiona miaka ya nyuma

Haya mkuu, sasa sio sawa kusema WAMESHATOA au kumwambia mtu akasome kwenye guidebook ya mwaka 2016/2017 ilhali unajua bado haijatoka.
 
Hivi inamaana wengi wa wasomi wetu hawa waliohitimu kidato cha sita ni kweli hawajui ni nini wasome katika ngazi ya chuo kikuu ?
Nikweli hawajui,inawezekana kabisa vipaumbele vyao wameona hawatovifikia kulingana na point zao.
 
Vp kwa upande wa IT na forest ajira zake?
 
Vetenary MD Sua.
mkuu uko serious kweli au wamanisha veterinary ni dude zaid ya MD?
labda ajaribu anaweza pata ila wasiwasi wangu ni ushindani maana kwa point zake chache sijui kama atapumua maana anaenda kushindana na pcb hapo
 
mkuu huwezi kwenda chuo kikuu sababu huna point 4 kwa masomo mawili hapo. pole sana ila fanya njia mbadala, kuna kurudia somo upate hizo maks n.k

Mkuu, niombe radhi kwa kunionea. E =1, C =3. Point 4 hizo. Rejea tena post yangu, halafu unipe maoni yako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn moreโ€ฆ