Ushauri kuhusu ku-apply vyuo vikuu 2016/2017

God'sBeliever

JF-Expert Member
Sep 1, 2015
5,788
3,028
Habari ndugu na wana JF kwa ujumla.

Nimeona nianzishe huu uzi mahususi kabisa kwa wale wanaoomba vyuo vikuu kozi mbali mbali tuwape elimu na ujanja ili waweze ingia vyuo wavipendavyo.

Pia huu uzi utashauri ubora wa chuo husika kuhusu baadhi ya kozi kwani kuna baadhi ya vyuo vina sifa kadhaa katika fani wanazofundisha.

Unachopaswa kufanya ewe unaeomba chuo utaleta matokeo yako yote ili tuyachambue ndio tukupe ushauri, pia kwa vyuo vyenye ushindani kwa kozi fulani hawa hadi matokeo ya form four wanaangalia so usiwe na hofu relax tutakushauri na hakika utashinda mapema wala hutapoteza kitu na pia uwashauri na wenzio walio karibu wapitie huu uzi ili wajifunze zaidi.

Kumbuka ufaulu wako ndo unaamua yote unapoomba kozi angalia ufaulu wako na ushindani kama idadi ni kubwa sana ya waliiomba na wewe una matokeo hafifu badilisha haraka.

Pia ni vyema kufanya maamuzi sahihi ukitegemea eti utahama chuo ni ngumu na hizi habari zinaingiliana na mkopo hivyo basi utaweza kuja kupata mkopo mwaka wa pili.

Hivyo basi jandae vizuri usiwe mbishi sikiliza ushauri wetu vizuri na sisi tumepita huko.

Pia wenzetu mliosoma diploma tunaweza wasaidia mawili matatu.
Karibuni sana.
 
CIV - 'D' HIST - 'D' GEO - 'C' E/D/KIISLAMU - 'D' KISW - 'C' ENGL - 'C' PHY - 'D' CHEM - 'C' BIO - 'C' B/MATH - 'D
Division 3 ya 23
Alafu sikupangiwa popote hebu nishauri nifanye nn malengo yangu ni kuwa daktari

Mkuu Kwani Kichwa Cha Habari si Kiko Hivi "Ushauri Kuhusu Ku apply Vyuo Vikuu 2016/2017".

Sasa Hujajua tu Kuwa Huu Uzi unawahusu Wale WaitList Wanaosubiri Kuingia Vyuo Viku?? au nawewe unataka kwenda Chuo?
 
nina ufauru wa DEE kwa combination ya CBG respectively naweza kwenda wap naitaj msaada wen kmawazo ili nijiongeze mapema
 
CIV - 'D' HIST - 'D' GEO - 'C' E/D/KIISLAMU - 'D' KISW - 'C' ENGL - 'C' PHY - 'D' CHEM - 'C' BIO - 'C' B/MATH - 'D
Division 3 ya 23
Alafu sikupangiwa popote hebu nishauri nifanye nn malengo yangu ni kuwa daktari
hayo ni matokeo ya form four tena bora umekutana na mimi nikushauri, kwa ukweli wewe una uwezo wa kawaida. sikushauri uende form six kule ni kupoteza mda tuu ila kama una amin utapata division one basi nenda na iwe ya PCB hapo utaweza kujikinga kifua na kuomba kozi ya udaktari vyuo vya serikali kama muhasi, udsm na udom. ila kwa vyuo vya private pcb za division 2 hadi 3 unaenda iwe unataka udaktari, ufamasia au maabara. ila kwenu muwe mna pesa ada ni zaidi ya million 6. kwa vyuo vya imtu, hku, kairuki huko. kampala. ila vyuo kama archibishop james songea ada ni million 3 na ushee ivi, st francis morogoro ada ni million 3 kasoro. na jua kadri miaka ivavyozidi kwenda ada nayo inapata.
kcmc na bugando ata inakaribia million 3 ila lazima uwe umefaulu vizur pcb, ushindani upo man,

ushauri wangu achana na mambo ya advance sababu unautaka udaktari. kwan zinahitajika pcb za one ila unaweza kwenda kama utakuja kusoma vyuo vya private na hela yako juu. serikali inatoa mkopo kwa hela isiyozidi million 3.1 na hapo hiyo milliom3.1 ni full yan asilimia 100% sasa wewe kubata hiyo asimilia 100% inategemea kama umekidhi mahitaji na vigezo vyao, mfano kama umesoma serikalini kuanzia msingi, olevel na advance na vipengele vyao vingine unaweza pata asilimia 100% au usipate kabisa kama seriikali haina pesa hili ni swala la bahati ndugu. kuna mayatima waliambatanisha vyeti vyao na ulemavu wa wazazi wao lakini wapi hawakupata nawengine wakafunga safari hadi hadi bodi ya mkopo na hawakusaidiwa,
so ndugu we apply chuo cha diploma tena vya serikali wewe matokeo yakmo yanaruhusu kabisa na utapata nina imani.
nimejitahidi nimekuambia yote. ukiwa na tatizo zaid nicheki usiwe na hofu
 
Mkuu Ushauri Wako Ni Muhimu Sana Kwangu Na Ninakuomba uzingatie Nyanja Zifuatazo wakati wa Kunishauri:-

1) Ushindani Wa Kupata Chuo kwa Kozi Husika ili Nijue Ni Vyuo gani Naweza Kupata, Na Vyuo Gani siwezi Kupata
2) Ada Za Kozi Husika
3) Ubora wa Kozi

Mimi Ni Diploma Holder Wa "Pharmaceutical Technician" na nina GPA ya 3.7

Sasa iwapo Nitapata Chuo & Mkopo, Ninataka Kusoma "PHARMACY" au "MD" sasa kwa Kuzingatia Vipengele Vitatu Nilivyo Vitaja Hapo Juu Naomba Ushauri wako nisome ipi Kati ya Hizi mbili??
 
Napenda kufanya marketing kaka!
pitia guide book ya tcu 2016/2017 kuna kozi kibao za biashara kuhusu marketing yako. unachopaswa kuangalia ni ushindani maana point zako ni za kawaida. ukiona watu wengi wameomba sana hiyo kozi we badilisha omba chuo kingine. saut, udom na imani utapata
 
Asante. Nisaidie kaka nitawezaje kujua kama wengi wameomba sana kozi hiyo? Udsm siwezi kupata bro?
 
yap nakukubali sababu uko vizuri na umeyaelewa maelezo yangu. pia nikupongeze kwa GPA kali hapo omba UDOM MD ya kwanza, halafu sababu kuna intake maalumu imetengewa kwa ajili ya diploma omba UDSM, MUHAS, KCMC, CUHAS/BUGANDO au ST FRANCIS morogoro
unapewa slot 5 za kujaza fata mtiririko nliokupa nakwambia hukosi ndugu amini nakuambia. ada vyuo vyya serikali ni million1.8 halaf kcmc ada ni milion 3.1 na 3.7 cuhac st francis ni 2.6m hizi takwimu zangu ni za mwaka jana sijajua kama wamepandisha,
karibu sana ukiwa na tatizo jingine
 
pitia guide book ya tcu 2016/2017 kuna kozi kibao za biashara kuhusu marketing yako. unachopaswa kuangalia ni ushindani maana point zako ni za kawaida. ukiona watu wengi wameomba sana hiyo kozi we badilisha omba chuo kingine. saut, udom na imani utapata
wewe guide book umeiona wap???
 
Asante. Nisaidie kaka nitawezaje kujua kama wengi wameomba sana kozi hiyo? Udsm siwezi kupata bro?
mkuu wewe hayo matokeo yako si ya form four wewe utasoma diploma, utaaply kupitia nacte ila sijajua proces zao kama walishafunga au wanaendelea kuomba,
utaona ushindani sababu unaona idadi ya watu waliiomba. unatengenezewa profile kabisa wala usiwe na hofu uki apply utaona system inavyokua
 
pitia guide book ya tcu 2016/2017 kuna kozi kibao za biashara kuhusu marketing yako. unachopaswa kuangalia ni ushindani maana point zako ni za kawaida. ukiona watu wengi wameomba sana hiyo kozi we badilisha omba chuo kingine. saut, udom na imani utapata

Kwani imeshatoka?
 
Asante. Nisaidie kaka nitawezaje kujua kama wengi wameomba sana kozi hiyo? Udsm siwezi kupata bro?
mkuu samahani kuna sehemu nimekosea nika sema ufaulu wako hafifu nilichanganya. hongera upefanya vizuri omba chuo chochote unapata im sure, marketing hukosi
 
mkuu wewe hayo matokeo yako si ya form four wewe utasoma diploma, utaaply kupitia nacte ila sijajua proces zao kama walishafunga au wanaendelea kuomba,
utaona ushindani sababu unaona idadi ya watu waliiomba. unatengenezewa profile kabisa wala usiwe na hofu uki apply utaona system inavyokua
Asante kaka kwa uvumilivu katika kunishauri, Mungu akubariki sana. Matokeo yangu ni ya kidato cha sita ambayo ni div 1 ya pointi 9 HGE nina C zote, nilikwambia ninapenda kufanya marketing, ila nilikuwa natafuta ushauri kwenu wakubwa zangu kama ninaweza kufanya kozi nyingine yenye mwelekeo mzuri huko mbeleni. Na mwisho nilikuuliza kama ninaweza kujiunga na udsm kwa matokeo hayo.
 
unaweza mkuu samahani sana nilikosea kukujibu, umefanya vizuri, kozi zipo nzuri sababu marketi ndo kila kitu kinachohitajika ni competence yako, yani skills zako na kusaka madili ndo zitawashawishi waajiri wakupe kibarua, usiangalie tuu GPA kubwa bali angalia na ushawishi wako kwenye nyanja husika. kuna kozi kama agrobusiness hii kwa maono yanu ina futute nzuri ipo sua na ukiomba unapata hata udsm ipo
 
Back
Top Bottom