Ushauri kuhusu elimu bure

Ushauri kuhusu elimu bure

Koryo2

JF-Expert Member
Joined
Nov 28, 2016
Posts
2,056
Reaction score
2,523
Kwanza kabisa naipongeza sana Serikali kuhusu dhana ya Elimu Bure kuanzia elimu ya msingi mpaka Sekondari LAKINI kuna changamoto zinazotakiwa kuangaliwa kwa umaakini sana.

Kwanza fedha inayotolewa kwenye shule ni kidogo sana. Leo asubuhi nimesikia kule Shinyanga katika Shule mmojawapo wanapewa Tshs.182,000 kwa mwezi na shulei na wakati watoto wengi. Pili, Kwa kawaida shule zote ni mali ya Wazazi lakini sasa hivi kwa kiasi kikubwa Wazazi wamejiweka mbali kama vile hawauhusiki.

Mfano Mzazi akiambiwa achangie fedha ya uji kwa ajili ya watoto wao wanasema Serikali iliishapiga marufuku michango ya aina yoyote. Tatu, tunajua kwamba shule za Sekondari zina upungufu mkubwa wa walimu wa masomo ya sayansi hasa fizikia,hesabu, kemia na bayoljia na hapo mwanzo wazazi walikuwa wanachanga kwa ajili ya upungufu wa walimu hawa, lakini sasa wazazi wamegoma kabisa kuchangia wakati shule nyingi zina upungufu wa walimu hawa.

Kwa hili nani anapata hasara ni Mzazi au Serikali. Tunaiomba Serikali aidha iangalie kwa undani changamoto zinazoikabili dhana ya elimu bure na kuzifanyia kazi.
 
Mkuu mpaka serikali iteng'anishe elimu na siasa.....sivyo elimu yetu ndo inakufa hivi hivi...huyu professor ilio pewa dhamana ya wizara kasha kua mwanasisa sio academician tena unamsikia bungeni anakana mambo hadharani wakati mwenyewe aliyaratibu mitaala ya darasa la 1-6. Anawaza kugobea jimbo kwao kigoma....Sio elimu tena.
 
Sisi kama Wazazi tunaishukuru sana Serikali kwa kutoa elimu bure tangu Shule za msingi mpaka Sekondari. Serikali imekuwa ikitumia takriban bilioni 24 kwa mwezi kwa ajili ya elimu bure. Ili mwanafunzi awe na maendeleo mazuri na uelewa katika masomo yake anatakiwa pate mlo/chakula cha mchana.

Familia nyingi ni duni na hawana uwezo wa kutoa chakula hata uji tu kwa watoto wao na hivyo mwanafunzi anashinda kutwa kwa njaa na matokeo yake ni kutoelewa masomo anayofundishwa na hatimaye kupata matokeo mabaya katika mitihani yake.

Ni vema sasa Serikali kwa nia njema kabisa kuongeza fedha zinazotolewa kwa ajili ya elimu bure ili zijumuishe pia na fedha za chakula cha mchana kwa ajili ya wanafunzi wa Shule za msingi na Sekondari. Ongezeko la Tshs. bilioni 5 nafikiri itatosha. Najua Serikali ya awamu ya tano ni sikivu na mtalifanyia kazi ushauri wangu huu.
 
Katika hii 24 b hata hii shule yetu hapa kijijini imo kwenye mgao? Sijawahi kuona wala kusikia eti mwezi fulani shule imepata daftari au vitabu au rangi.
 
Kawaulize kama wanapokea fedha za elimu bila malipo? na mgawanyo wa matumizi yake ukoje? yaani hata daftari hutaki mnunulia mwanao unataka serikali inunue?
 
Back
Top Bottom