Ushauri kuhusu bestman

msakapesa

Member
Sep 19, 2013
26
17
Habari wanajamvi. mie natarajia kufunga ndoa mwezi wa 10 mwaka huu, sasa naomba ushauri wa kumpata bestman, msimamizi wa ndoa yangu aweje awe na sifa zipi, maana even ukiwa kanisani wapo watu ambao wanafake relationship kati ya mume na mkewe lakini maisha ya ndani ni vurugu mwanzo mwisho, naomba kuwakilisha.
 
weka picha ili tuweze kukupa sifa za bestman wako awe vipi..bila kukuona wewe ukoje inakuwa ngumu kusema awe vipi..
 
embu funguka

unataka sifa za muonekano..like unene?sura?umbo or

unataka kujua yale ya ndani ya tabiaza upendo na amani ndan ya ndoa zao

je unajua kwenye ndoa kuna kipindi cha kutofautina??sio kila siku ni sikukuu tuuuu ...kikubwa ni jinsi ya kumaliza tofuti zao
kama wwe unafikiri eti unawaona kanisani wazuri ila ndani ya ndoa zao kuna matatizo jua hizo ndoa
jiapange kukutana na mengi
 
hapo mambo kwenye best man ngumu kushauri ungefunguka vya kutosha ingekuwa bora sana....
 
hapana kuhusu unene au wembamba. Je ni kigezo gani nitumie ili niweze kumpata bestman mzuri, mfano, je bestman wangu ni lazima awe rafiki yangu, tuwe tunaendana umri, au awe na tofauti kubwa kiumri kati yangu mwanandoa mpya na yeye au inakuwaje katika mila na desturi( kabila liwe sawa??) je kuna haja ya kuchukua mume na mke wa ndoa moja wawe walezi wa ndoa yetu, au mie best man wangu na mke wangu matroni wake anayempenda yeye?/maana kuna haja ya kumshirikisha mpenzi wangu kuhusu swala la bestman, na wat if akiwa hamtaki????
 
Kuhusu umri ni vyema mkaendana mkuu bestman hatakiwi akuzidi sana.
Kuhusu mahusiano ya ndoa zao, hiyo haikuhusu sana maana kazi yao ni ya siku moja tu, hayo ya kuwa walezi wenu sio lazima ma best wawe walezi wenu!, mwaweza tafuta watu wazima sana na waliokaa kwenye ndoa muda wa kutosha, itasaidia sana!
Kuhusu uchaguzi wa ma best inabidi wote mkubaliane!
 
Post kule jukwaa la matangazo utawapata walio tayari kwa malipo. siku hizi kila kitu ukiwa na hela kinawezekana hata wa kulia kwenye misiba wapo, wewe tu
 
Back
Top Bottom