Ushauri: Kesi ya mirathi ya nyumba Dar es Salaam

cacashian01

Member
Mar 3, 2016
76
62
habari zenu wadau,

naomba ushauri wenu kwa wale wenye utaalamu wa kisheria,

mzee wangu alinunua Ghorofa kwa mzungu(mzawa) japo alikua hajamalizia hela kidogo ila mzungu alisamehe ila hati alikuahajakabidhi.,miaka ya 80’s,tukampangisha mpangaji mzungu,akakaa kwa miaka kadhaa,wazazi wakafariki kwa ajali,sisi tupo watatu,baada ya hapo mirathi akaachiwa asimamie kaka yetu,kwakauwa tulikua wadogo sana,kwenye miaka ya 97 kaka akafoji hati akamuuzia Yule mpangaji mzungu bila sisi kujua,tulipo gundua kaka alikimbilia ulaya,Yule mzungu aliye tuuzia nyumba anasema yuko tayari kutukabidhi hati tukiwa wote na tusaini,ila Yule mpangaji anasema nyumba yake,na hilo eneo limekuwa kama pori,tulipo fanya search ardhi,majibu yansema eneo lilirudishwa na likakbidhiwa kwa raisi,ila muuzaji(mzungu)anasema hajalirudisha eneo,wala hanabarua yoyote ya wizara ya ardhi wala tangazo,na eneo linasoma jina lake,mpaka atukabidhi tubadilishe.

Ushauri nifanyaje kulipata eneo,
 
Mkuu kabla sijakusaidia lolote labda unisaidie kujibu yafuatayo:

1. Unaposema eneo limekuwa kama pori ina maana gani, je kuna nyumba au ni kiwanja kitupu?

Swali lina maana kwa kuwa ili eneo lirudishwe kwa Mh. Rais ni lazima kulikuwa na ukiukaji wa masharti ya umiliki wa eneo. Masharti ni mengi ila la uendelezaji hasa ndio limekuwa likipewa uzito.

2. Hilo eneo liko mahala gani, title search ulifanya lini na uliambiwa limepelekwa kurudishwa kwa rais lini? (Kama limesharudishwa kwa rais lilirudishwa na kutangazwa lini kuwa limerudishwa kwa rais?) Maake waweza kulipata tena kama halitakuwa limetolewa upya.

3. Hati ya Mzungu wa kwanza aliyemuuzia baba yenu ilikuwa inaexpire lini?

Mkuu kama utajibu maswala haya labda ninaweza kukupa ushauri.

NB: Hati feki achana nayo haina uzito wowote japo mazingira ya uuzji yanaweza kumpa uhalali mnunuzi.
 
Nashukuru kwakujali

1.eneo limekuwa pori,maana ni hekari 5,na ndani yake kuna gorofa ambalo anakaa huyo mzungu,ila hekari nyingine kama 3,hashughuliki nazo huwa anapunguza majani mara moja moja tu kwa hiyo linaonekana kama pori flani,ila eneo limezungushiwa uzio lote.na watu wa ardhi wakaomba wachukue kipande ili kuendeleza mji kwa makubaliano ya manunuzi,
2.eneo liko makongo juu,title search nilifanya mwaka jana mwezi wa sita,ikasema eneo limekabidhiwa kwa raisi mwaka 2011 mwezi wa 11,ila hakuna tangazo lililomfikia huyo mzungu wala barua na anasema kama walituma au yeye alilikabidhisha wampe ushahidi,na commissioner hajatuthibitishia hilo tangazo kama walitangaza lini wala kutuonyesha nakala.
3.hati ya mzungu wa kwanza ni ya miaka 99,haija expire bado.mzungu wa pili hana hati yoyote na sio raia,sema kuna watu anashirikiana nao ili kupata hilo eneo,ndio maana hadi ardhi ushirikiano unakuwa mdogo.
Note.ila eneo la makongo juu kuna mradi ulikua unapita wakuendeleza mji ndio maana kufika kwenye hilo eneo wakamkuta mzungu akawa hana ushirikiano na watu wa Ardhi,ndo tukatafutwa wahusika maana walikua hawatujui,ndo kesi ikaanza hapo kufuatilia,ila kwenye huo mradi commissioner alisema kama unavyosema kukabidhiwa eneo Mh.Rahisi haimaanishi kama halirudi,tukifuata taratibu linarudi,ila watu wamaeneo hayo walirudisha hati zote nakuomba upya kwa ajili ya mji mpya huo-commisioner.
 
Kwa maelezo yaliyotolewa hapo juu si rahisi eneo kuwa limetwaliwa na rais kwa maana ya acquisition maake ingekuwa hivyo serikali ingetoa taarifa ya kusudio la kufanya hivyo, uthamini ungefanyika na mngelipwa fidia (hii ni kama lingechukuliwa kuendeleza mji).

Lakini ipo namna nyingine ambayo rahisi anaweza kulichukua eneo ambalo hati imetolewa na masharti yaliyotolewa kwenye hati hayakutimizwa hii inaitwa Revocation of the Title.

Njia hii ya pili ya utwaaji ardhi kwa Ardhi ina mlolongo mrefu ili kuhakikisha haki ya mmiliki wa Ardhi inalindwa dhidi ya uonevu au watumishi wasiokuwa waaminifu.

Hatua ni pamoja na mmiliki kutumiwa notisi ya kusudio la kutoa mapendekezo kwa Mh. Rais kuwa miliki yake ifutwe. Notisi itaeleza mmiliki amekiuka masharti yapi na atatakiwa kujitetea kwa nini Commissioner asimshauri rais afute milki. (Notisi hutolewa na kutakiwa kujibiwa ndani ya siku 90)

Iwapo Commissioner hakuridhika na sababu ulizotoa au iwapo hukutoa sababu zozote basi atapendekeza kwa Mh. Rais kuwa miliki ifutwe.

Kimsingi utwaaji wa ardhi kwa staili hii ya pili sio kawaida labda kama kuna mgogoro au eneo ni prime. Kitu ambacho kwa mujibu wa maelezo yako sidhani kama vipo.

Ushauri wangu kama kweli eneo lilirejeshwa kwa Mh. Rais ni lazima uwepo ushahidi ikiwamo kutumiwa notisi ya kusudio la kufuta milki. (hii ni lazima ipo kwenye faili maake bila hiyo milki haifutwi)

Nakushauri uende Kinondoni wakupatie ushahidi wa hiyo notisi maana kila kiwanja kina file lake na nyaraka zote ikiwamo barua n.k huwekwa kwenye faili husika. Vikikosekana nachelea kusema hakuna kitu kama Mh. Rais ametwaa eneo lako.

NB; Mkuu ilikuwaje mkamilikishwa eneo lote hilo kwa mtu mmoja. Ni vema ukaangalie kwenye hati kama lilitolewa kama Housing Estate au Shamba. Maana haiwezekani kuwa lilitoka kama kiwanja cha kawaida.

Pili kwa kumbukumbu zangu sidhani kama Mh. Kikwete alirevoke hati yoyote DSM 2011 nakumbuka amefanya hivyo 2015.

Nakutakia ufuatiliaji mwema na karibu tena
 
Nashukuru sana kwa ufafanuzi wako Mkuu,umenifungua sana na kunipa mwanga na mwongozo mzuri,

Kama ulivyosema eneo nikubwa sana maana hati yake iliyotoka ni ya shamba,maana kwakipindi kile eneo la makongo juu lilikua linatambulika kama KISARAWE,ila pia nyumba hiyo ya gorofa ilikuwepo ndani yake.
 
Kama hati iliyotoka ni ya shamba sioni ni kwa namna gani mnyanganywe kwa njia ya revocation. Kwa sababu kama halikuwa eneo lililotolewa kwa uwekezaji bali ni maombi ya mtu kupewa milki ya shamba lake, binafsi sioni mnapokonywa vipi? ( Maake ni rahisi kumbana mwekezaji kuwa hajatimiza masharti ila sio kwa raia wa kawaida aliyeomba apewe milki ya shamba)

Fuatilia kama kuna ushahidi wa vile nilivyokueleza. Kama hakuna mafanikio kalalamike kwa Makonda straight au kwa Lukuvi. Ukishindwa hilo lalamika ikulu moja kwa moja ili wakuthibitishie lini na kwa amri ipi Mh. Rais alitwaa eneo lako
 
Halafu huyo mzungu alikuwa RAIA wa wapi? Maana mojawapo ya sababu ya Rais kurevoke yaweza kuwa kuwauzia ardhi non citizen rejea sheria ya ardhi kifungu cha 45
 
Za jioni.nilifuatilia wilayani na kwa mkuu wa mkoa,ila nikaambiwa nianzie katika baraza la ardhi la wilaya au kwa mtendaji,ila mtendaji ameniambia inabidi kuandika (msimamizi wa mirathi) barua ya kisheria ya notice kuondoka katika nyumba hiyo.alafu kuanzia hapo ndo kama nikesi au atatii tuendelee.unaonaje?
NAHITAJI MSAADA WAKO WA USHAURI
 
Nashukuru sana kwa ufafanuzi wako Mkuu,umenifungua sana na kunipa mwanga na mwongozo mzuri,

Kama ulivyosema eneo nikubwa sana maana hati yake iliyotoka ni ya shamba,maana kwakipindi kile eneo la makongo juu lilikua linatambulika kama KISARAWE,ila pia nyumba hiyo ya gorofa ilikuwepo ndani yake.
Shukuru umesaidiwa. Kwanza wew ni tajiri hadi muda huu ila hujajijua tu. Pili mambo kama haya hatua inayofuatia ni kulipa kahela kidogo tu kwa huyo mshikaji mdadavuji hapo juu na kumkabidhi hili jukumu yeye wew unatoa ushirikiano tu pale inapohitajika. Shamba hilo utalipata kwa haraka tu. Nyongeza mshikaji wangu ndiye anayeshughulika na eneo lote la makongo juu kwenye huo mradi. Ukiondoa ubahili kidogo tu utatiririka vizuri sana.
 
Kwa maelezo yaliyotolewa hapo juu si rahisi eneo kuwa limetwaliwa na rais kwa maana ya acquisition maake ingekuwa hivyo serikali ingetoa taarifa ya kusudio la kufanya hivyo, uthamini ungefanyika na mngelipwa fidia (hii ni kama lingechukuliwa kuendeleza mji).

Lakini ipo namna nyingine ambayo rahisi anaweza kulichukua eneo ambalo hati imetolewa na masharti yaliyotolewa kwenye hati hayakutimizwa hii inaitwa Revocation of the Title.

Njia hii ya pili ya utwaaji ardhi kwa Ardhi ina mlolongo mrefu ili kuhakikisha haki ya mmiliki wa Ardhi inalindwa dhidi ya uonevu au watumishi wasiokuwa waaminifu.

Hatua ni pamoja na mmiliki kutumiwa notisi ya kusudio la kutoa mapendekezo kwa Mh. Rais kuwa miliki yake ifutwe. Notisi itaeleza mmiliki amekiuka masharti yapi na atatakiwa kujitetea kwa nini Commissioner asimshauri rais afute milki. (Notisi hutolewa na kutakiwa kujibiwa ndani ya siku 90)

Iwapo Commissioner hakuridhika na sababu ulizotoa au iwapo hukutoa sababu zozote basi atapendekeza kwa Mh. Rais kuwa miliki ifutwe.

Kimsingi utwaaji wa ardhi kwa staili hii ya pili sio kawaida labda kama kuna mgogoro au eneo ni prime. Kitu ambacho kwa mujibu wa maelezo yako sidhani kama vipo.

Ushauri wangu kama kweli eneo lilirejeshwa kwa Mh. Rais ni lazima uwepo ushahidi ikiwamo kutumiwa notisi ya kusudio la kufuta milki. (hii ni lazima ipo kwenye faili maake bila hiyo milki haifutwi)

Nakushauri uende Kinondoni wakupatie ushahidi wa hiyo notisi maana kila kiwanja kina file lake na nyaraka zote ikiwamo barua n.k huwekwa kwenye faili husika. Vikikosekana nachelea kusema hakuna kitu kama Mh. Rais ametwaa eneo lako.

NB; Mkuu ilikuwaje mkamilikishwa eneo lote hilo kwa mtu mmoja. Ni vema ukaangalie kwenye hati kama lilitolewa kama Housing Estate au Shamba. Maana haiwezekani kuwa lilitoka kama kiwanja cha kawaida.

Pili kwa kumbukumbu zangu sidhani kama Mh. Kikwete alirevoke hati yoyote DSM 2011 nakumbuka amefanya hivyo 2015.

Nakutakia ufuatiliaji mwema na karibu tena
Fee kidogo tu akulipe. Halafu utaendelea na kazi yake mkuu. Ardhi ni utajiri
 
Mkuu kabla sijakusaidia lolote labda unisaidie kujibu yafuatayo:

1. Unaposema eneo limekuwa kama pori ina maana gani, je kuna nyumba au ni kiwanja kitupu?

Swali lina maana kwa kuwa ili eneo lirudishwe kwa Mh. Rais ni lazima kulikuwa na ukiukaji wa masharti ya umiliki wa eneo. Masharti ni mengi ila la uendelezaji hasa ndio limekuwa likipewa uzito.

2. Hilo eneo liko mahala gani, title search ulifanya lini na uliambiwa limepelekwa kurudishwa kwa rais lini? (Kama limesharudishwa kwa rais lilirudishwa na kutangazwa lini kuwa limerudishwa kwa rais?) Maake waweza kulipata tena kama halitakuwa limetolewa upya.

3. Hati ya Mzungu wa kwanza aliyemuuzia baba yenu ilikuwa inaexpire lini?

Mkuu kama utajibu maswala haya labda ninaweza kukupa ushauri.

NB: Hati feki achana nayo haina uzito wowote japo mazingira ya uuzji yanaweza kumpa uhalali mnunuzi.

Kwa maelezo yaliyotolewa hapo juu si rahisi eneo kuwa limetwaliwa na rais kwa maana ya acquisition maake ingekuwa hivyo serikali ingetoa taarifa ya kusudio la kufanya hivyo, uthamini ungefanyika na mngelipwa fidia (hii ni kama lingechukuliwa kuendeleza mji).

Lakini ipo namna nyingine ambayo rahisi anaweza kulichukua eneo ambalo hati imetolewa na masharti yaliyotolewa kwenye hati hayakutimizwa hii inaitwa Revocation of the Title.

Njia hii ya pili ya utwaaji ardhi kwa Ardhi ina mlolongo mrefu ili kuhakikisha haki ya mmiliki wa Ardhi inalindwa dhidi ya uonevu au watumishi wasiokuwa waaminifu.

Hatua ni pamoja na mmiliki kutumiwa notisi ya kusudio la kutoa mapendekezo kwa Mh. Rais kuwa miliki yake ifutwe. Notisi itaeleza mmiliki amekiuka masharti yapi na atatakiwa kujitetea kwa nini Commissioner asimshauri rais afute milki. (Notisi hutolewa na kutakiwa kujibiwa ndani ya siku 90)

Iwapo Commissioner hakuridhika na sababu ulizotoa au iwapo hukutoa sababu zozote basi atapendekeza kwa Mh. Rais kuwa miliki ifutwe.

Kimsingi utwaaji wa ardhi kwa staili hii ya pili sio kawaida labda kama kuna mgogoro au eneo ni prime. Kitu ambacho kwa mujibu wa maelezo yako sidhani kama vipo.

Ushauri wangu kama kweli eneo lilirejeshwa kwa Mh. Rais ni lazima uwepo ushahidi ikiwamo kutumiwa notisi ya kusudio la kufuta milki. (hii ni lazima ipo kwenye faili maake bila hiyo milki haifutwi)

Nakushauri uende Kinondoni wakupatie ushahidi wa hiyo notisi maana kila kiwanja kina file lake na nyaraka zote ikiwamo barua n.k huwekwa kwenye faili husika. Vikikosekana nachelea kusema hakuna kitu kama Mh. Rais ametwaa eneo lako.

NB; Mkuu ilikuwaje mkamilikishwa eneo lote hilo kwa mtu mmoja. Ni vema ukaangalie kwenye hati kama lilitolewa kama Housing Estate au Shamba. Maana haiwezekani kuwa lilitoka kama kiwanja cha kawaida.

Pili kwa kumbukumbu zangu sidhani kama Mh. Kikwete alirevoke hati yoyote DSM 2011 nakumbuka amefanya hivyo 2015.

Nakutakia ufuatiliaji mwema na karibu tena
Habari yako,unahusika na sheria za ardhi?Ningependa kujuwa kama mirathi ilifunguliwa mwaka 72,na warithi wakagawana mirathi yao,wakafariki.Je yawezekana tena,mtoto wa miongoni wa waliogawana akafunguwa mirathi ya mali hiyo hiyo,akadai nyumba iliyopewa warithi wengine?Wakati wao walishapewa nyumba na shamba,lililopimwa viwanja karibia arubaini na kuviuza hivyo viwanja.
Kwa maana amefunguwa kesi,lakini hakuoredhesha nyumba na shamba,walilipewa wao,ila ameoredhesha nyumba waliopewa wengine tu.Je hapo ni sawa,kwa kuorodhesha nyumba moja,na kuacha mali nyingine waliopewa wao?
 
Mkuu Kikwajuni One kwanza nikukaribishe katika uzi huu kuhusu masuala ardhi.

Kuhusu swali la mimi kuhusika na masuala ya Ardhi jibu lake ni ndiyo, kwani ndio profession yangu.

Pili kuhusu hoja uliyoiweka mezani, naomba nieleze machache.

Swala la mirathi ni swala pana na linaongozwa name sheria nyingi kutegemeana uwapo wa wosia na dini na mila za marehemu. Hivyo katika kutoa ushauri haya yote huzingatiwa. Labda nieleze yafuatayo;

1. Mali iliyogawanywa kama mirathi huhesabika kama mali ya mrithi au mtu aliyeteuliwa kuwa msimamizi wa mali za marehemu kwa mujibu wa sheria. Kwa hiyo kuhusu mirathi hiyo ya marehemu wa kwanza ni dhahiri ilikuwa mali halali ya wale warithi wa mwanzo.

2. Kuhusu hoja ya pili juu ya uhalali wa watoto wa marehemu aliyepewa urithi kudai urithi wa marehemu wengine.
Uhalali wa madai hayo kisheria unategemea mambo mawili; LA kwanza iwapo haki ya urithi wanayoidai imetamkwa kwenye wosia wa marehemu hao (kwa maana kwamba marehemu waliwataja hao wadai kama warithi wa mali zao) au iwapo marehemu walikuwa Wakristo na hawakuacha mke/mme na watoto au wajukuu basi iwapo hao ndugu ndio ndugu wa karibu zaidi wa marehemu basi watakuwa na haki ya kurithi mali za marehemu hao.

Kwa kuwa hoja hii ya pili inategemeana zaidi na dini na mila husika za marehemu nashauri ni vema ukatujulisha iwapo sharti la kwanza hawakutimiza (kwa maana hawakutajwa kwenye wosia) basi tuambie iwapo marehemu waliacha watoto au la na vile vile dini na mila za marehemu.
 
Asante kwa maelezo yako.
Marehemu wote ni waislamu,na walipofunguwa mirathi,kwa mujibu wa muhtasari wa vikao vya ndugu vya kuchaguwa msimamizi wa mirathi,walitaka mirathi yao iendeshwe kiislamu.
Na vile vile,hawakuacha wasia wowote ,wa mtu yoyote kurithi.Na waliofunguwa mirathi mingine ni wajukuu wawili wa watoto wa mwanamke wa marehemu aliyeacha hizo nyumba na mashamba yaliyopimwa viwanja.
Marehemu aliacha watoto,na hao watoto ndio waliofunguwa mirathi miaka ya 70,hao watoto wakagawana mali zao katika vikao mbali mbali,walivyokaa na pia mke wa marehemu alipewa,na karatasi za mahakamani za kupewa zipo.Hawa watoto wa marehemu walifariki wote.Waliofunguwa mirathi ni wajukuu wa marehemu,ambao wazazi wao walishafariki,baada ya kufunguwa mirathi na kugawana mirathi.
Je baada ya kugawana watoto wa marehemu na wao pia kufariki,inawezekana wajukuu wa marehemu kufunguwa mirathi ile ile,ambayo warithi walishagawana?
Na pia imengundulikana mahakamani mirarhi waliyofunguwa kuna njia zisizo halali wamepitia mojawapo ni yakutaja jalanda namba,ambalo ni la marehemu mwingine kabisa sio lao.
 
Pole sana Comrade ila naamini JF ni bahari isiyo na beach kwa vipaji na weledi utasaidiwa tu!
 
Shukuru umesaidiwa. Kwanza wew ni tajiri hadi muda huu ila hujajijua tu. Pili mambo kama haya hatua inayofuatia ni kulipa kahela kidogo tu kwa huyo mshikaji mdadavuji hapo juu na kumkabidhi hili jukumu yeye wew unatoa ushirikiano tu pale inapohitajika. Shamba hilo utalipata kwa haraka tu. Nyongeza mshikaji wangu ndiye anayeshughulika na eneo lote la makongo juu kwenye huo mradi. Ukiondoa ubahili kidogo tu utatiririka vizuri sana.
hata siku moja usitumie tatizo la mwenzako kujinufaisha mkuu, hii ni laana mbaya sana ambayo itakula kizazi na kizazi chako
 
Kama hati iliyotoka ni ya shamba sioni ni kwa namna gani mnyanganywe kwa njia ya revocation. Kwa sababu kama halikuwa eneo lililotolewa kwa uwekezaji bali ni maombi ya mtu kupewa milki ya shamba lake, binafsi sioni mnapokonywa vipi? ( Maake ni rahisi kumbana mwekezaji kuwa hajatimiza masharti ila sio kwa raia wa kawaida aliyeomba apewe milki ya shamba)

Fuatilia kama kuna ushahidi wa vile nilivyokueleza. Kama hakuna mafanikio kalalamike kwa Makonda straight au kwa Lukuvi. Ukishindwa hilo lalamika ikulu moja kwa moja ili wakuthibitishie lini na kwa amri ipi Mh. Rais alitwaa eneo lako

hata siku moja usitumie tatizo la mwenzako kujinufaisha mkuu, hii ni laana mbaya sana ambayo itakula kizazi na kizazi chako

king kan nisaidie no.yako ya simu
 
Back
Top Bottom