uzeebusara
JF-Expert Member
- Apr 15, 2013
- 657
- 514
Habari wanajamii
Naomba ushauri wa kiroho au kisaikolojia kuna masuala yananitokea sielewi namna gani kuyakabili
Kwa kifupi ni hivi, kuna baadhi ya nyakati huwa natokewa hali ambayo inaweza kuwa
1. Mhemko "tension"
2. Furaha
3. Huzuni
4. Bumbuwazi
Hali hizi hutokea katika nyakati tofauti tofauti na zimekuwa zenye kudumu zaidi ya miaka 15 kwn nakumbuka zilianza kutokea wakati nasoma "O level"
1. Mhemko "tension"
Hali hii inaweza kutokea tu inakuwa kama kuna habari na subiri kwa hamu sana utadhani kama vile mtu ameniambia atanipa habari fulani muhimu sana hivyo naweza kukaa kutwa nzima na hali ya tension ya juu sana. Na ikitokea hivyo lazima ntapata habari au ntajuzwa jambo muhimu anaweza kuwa jamaa, rafiki au ndugu au mtu yoyote tu. Sasa nashindwa kuelewa hisia hii au mhemko huu unakuja vipi. Ubaya wake hali hii inaniumiza sana inapotokea. Je hii hali ni athari za kisaikolojia au kiroho?
2. Furaha
Hali hii naweza kuta labda nimeamka kawaida tu. Lkn moyo waweza kupasuka kwa furaha nisiyojua nini nafsi yangu yafurahia. Na ikitokea hivi ndani ya siku hiyo ntapata tu habari za furaha au za kheri sana. Sasa ikitokea nayo hali hii tatizo lake mpaka niijue ndiyo nafsi au roho yangu inatulia vinginevyo nabaki namna hiyo tu hata kama siku nzima. Je yaweza kuwa tatizo la kisaikolojia au kiroho?
3. Huzuni
Hali hii ni kama hapo juu nilivyoelezea. Yaani naweza kuwa na unyonge hasa nafsini mwangu, japo mtu au rafiki yangu huwezi kugundua ila Mimi nakuwa nalihisi hili tena kwa nguvu sana. Hali hii ikitokea huishia kupata habari si nzuri. Sasa nashindwa kujua nini hasa
4. Bumbuwazi
Hali hii hunitokea nyakati nakuwa na uzubavu au akili fikirishi nayokuwa nabaki na mshangao Wa kutopata jibu au njia ya kutatua jambo japo sijui ni jambo gani linalonipa ubumbuwazi. Lakini mwisho Wa siku utakuta napata taarifa fulani au shida fulani ambayo naitatua bila hata kujua njia ipi nimepita kufika katika jibu
Sasa hali hii mwanzo nilikuwa naona ni ya kawaida. Lakini kadiri umri wangu unavyozidi naona hii hali inazidi kukomaa sana. Nishajaribu kuwauliza watu wengi wa fani ya udaktari na saikolojia na tiba mbadala sijapata jibu zaidi ya kuambiwa ni hali ya kawaida tu. Lakini labda jambo limekaa kihisia sana, Mimi naliona si kawaida. Karibuni kwa ushauri