Ushauri katika kadhia hii ya kifamilia

Pili, kule ofisini kazi hajaacha je uhusiano na huyo bosi aliemuweka hautakuwa unaendelea?
Tatu, nini hasaa kinachomrudisha kwangu na kujiliza usiku na mchana kubembeleza turudiane au tuendelee na maisha kama zamani?

Huu msimu wa Magufuli mabosi wamepunguza michepuko, hela ya kuhudumia familia 2 hakuna, huyo anarudi kwako kwa sababu hiyo mkuu.
 
Ushauri wangu kwa mjibu wa dini mtoto wa kwanza wako maana kazaliwa ndani ya ndoa ila kama ushampa talaka na EDA ishapita Huyo c mkeo tena tafuta mwingine uoe Wabillahi taufiq
 
Umri wenu bado mdogo sana katika ndoa. Mshukuru Mungu kwanza kwa kuonyeshwa kucha mapema. kuwepo kazini na kutokuwepo hakutakuhakikishia wao na mubosi kuachana.
  1. Pima vinasaba lea wanao kama itakuwa ni wako na kama la chapa mwendo
  2. Hata kama ni wako talaka umeshatoa achana nae
  3. pia kumbuka maisha ni watu na mahusiano yenu mpaka kwa wake yamkini sio shwari tena
 
Potezea bwana na malaya huyo...mie ndio maana nasema wanawake ni kugegeda tuu ata mambo ya kusema familia kwa sasa ni kupotezzea tuu.
 
Suala la DNA ntaleta mrejesho hapa vile vile. Ila nahitaji kujipanga sana kupata majibu sahihi yasiyo na shaka ndani yake. Nipo tayari kuyakubali majibu yoyote yatakayokuja kwa mazingira sahihi na yasiyo na mashaka ndani yake kwani huyu mwanamke ni mjanja mjanja sana
 
Ushauri wangu kwa mjibu wa dini mtoto wa kwanza wako maana kazaliwa ndani ya ndoa ila kama ushampa talaka na EDA ishapita Huyo c mkeo tena tafuta mwingine uoe Wabillahi taufiq
Hili suala linahitaji ufafanuzi wa kidini zaid.
 
Pima DNA kwa mtoto wa pili tu kwenye hospitali tofauti tofauti ambayo umeyapanga wewe ili kuepusha kupanga matokeo. Kuwa makini zaidi ya unavyofikiria maana Ibilisi anakuchekea chekea ili akunase.
 
Ulikosea sana ulipomwambia mkapime DNA....inaudhi sana eti kisa mtoto hajafanana nanyi....kwani lazima mtoto afanane na baba tu jamani??

Hata ningekuwa mimi ningesema mtoto si wako wakati ni wako

ni kuvunjiana sana heshima!!

Mama yake inawezekana nae ilimkera sana ndio maana akakujibu vibaya...inawezeka a hana kabisa uhusiano na huyo bosi.

hebu vaa viatu vyake ungekuwz weee ungejisikiaje??

Ulitakiwa kumpima dna kimyakimya kisha majibu kama hasi ndipo ungemwambia.

Anyway
kapime mtoto sidhani sana kama huwa kuna kupindisha majibu.

kama watoto ni wako jitahidi uwapende tu kwani hawana makosa.
 
sipotezi muda wangu kukushauri.

Elimu yako inatosha kukusaidia what to do
 
Pima dna watoto wote 2

Inawezekana alikujibu kua sio wako.kwa hasira

Ingawa mkweo hakutumia busara

Dna ndio suluhisho
 
Ulikosea sana ulipomwambia mkapime DNA....inaudhi sana eti kisa mtoto hajafanana nanyi....kwani lazima mtoto afanane na baba tu jamani??

Hata ningekuwa mimi ningesema mtoto si wako wakati ni wako

ni kuvunjiana sana heshima!!

Mama yake inawezekana nae ilimkera sana ndio maana akakujibu vibaya...inawezeka a hana kabisa uhusiano na huyo bosi.

hebu vaa viatu vyake ungekuwz weee ungejisikiaje??

Ulitakiwa kumpima dna kimyakimya kisha majibu kama hasi ndipo ungemwambia.

Anyway
kapime mtoto sidhani sana kama huwa kuna kupindisha majibu.

kama watoto ni wako jitahidi uwapende tu kwani hawana makosa.
Mkuu asante kwa ulivyosema. Hapo sijamwaga mambi mengi ya ajabu aliyokuwa akiyafanya baada ya kupata kazi hiyo. Kwani ndoa iligeuka ndoano na mimi sasa nikageuka kuwa mama na yeye ndiyo baba wa nyumba mwenye sauti na maamuzi na sauti
Ukiona hadi mshenga kanyoosha mikono na kuna watu waliokuwa wanamlingania kusema "asiyefunzwa na mamaye hufunzwa na ulimwengu" ndo hayo yaliyomkuta. Masuala mengine ya ndani ni aibu kuyaweka hadharani mkuu. Ila ukiona hadi mwanaume kakubali kukuachia kila kitu na kusema acha akaanze maisha mapya ujue mwanamke amevuka mipaka ya uvumilivu. Maana unaweza kushindwa kujizuia na kuishia kumpa kichapo ambacho unaweza kuishia gerezani tu
 
Habari zenu
Baada ya salamu tupeane pole wote kwa kuisoma namba hasa pasina matarajio ya lini hali za kiuchumi zitaka sawa
Ama baada ya hilo, ndugu zangu naombeni ushauri muhimu sana katika kadhia ambayo imetokea katika ndoa yangu
Kwa kifupi ni kuwa kuna binti tulioana kwa muda kama miaka mitatu hivi na kidogo katika muda huo wote tulijaaliwa kupata mtoto mmoja kwanza ila ukawepo utata kuhusiana na baba halisi wa huyu mtoto kwani mienendo ya huyu aliekuwa mke wangu ilibadilika sana kabla ya kupata mimba hasa baada ya kupata kazi shirika moja hivi la hifadhi jina kapuni na kwa bahati nzuri alipata cheo. Kielimu yeye ana shahada na mimi vile vile ni shahada tofauti zetu ni kuwa mimi niliachana na masuala ya kuajiriwa na kujikita katika kujiajiri. Alhamdulillaah biashara hazikunitupa mkono kwani kama kula, nyumba na usafiri havikuwa tatizo kwangu
Na vilevile japo mshahara wake alikuwa anapata mkubwa tu lakini hata siku moja sikuwahi kumwambia anisaidie katika majukumu kama mume ila akijisikia alikuwa anasaidia. Na hili nililifanya hasa kwa misingi ya dini yetu.
Turejee katika suala la mtoto. Huyu mtoto alivyozaliwa wazazi na ndugu walipomuona walisema kuwa makini mtoto huyu sio asili yetu kwa watu wa Visiwani hasa mnatujua. Hakuwa kabisa na uasilia wowote na kinasaba na jamaa yoyote na kwetu lakini nikajipa matumaini huenda anafanana na upande wa kwao. Ila kuna siku nikamweleza mwenzangu kuwa kuna haja ya kumpima DNA mtoto yule mwanzo alikataa lakini baadae akakubali kwa shingo upande. Kabla ya kwenda kumpima nilipata safari ya dharula kwenda nje ya nchi basi nilivyorejea kumkumbusha tu suala la DNA ikawa shida. Maana alimwaga matusi na maneno vibaya sana na mwisho akanitamkia kua yule mtoto mimi sio baba yake. Baba yake yupo bosi aliempa nafasi kule kazini. Mwanzo niliona mas'khara. Lakini aliendelea kushikilia msimamo huo na kurudia zaidi ya mara 5.
Kiukweli niliumia sana na pamoja na maneno na kero zoote sikuwahi hata siku moja kumjibu vibaya. Kuificha aibu ile ilibidi niende kwa mama yake mzazi yaani mkwe wangu wa kike. Nikamweleza a to z ya yote. Ajabu yule mama kwa lugha lainiii kabisa akaniambia sawa kama ishatokea sasa tatizo lako ni nini. Ulitaka mtoto wetu akose kazi sehemu nzuri? Daah nikakubali matokeo na kusema alhamdulillaah na kuondoka zangu. Basi baada ya hapo nikaamua niachane nae. Nikampa talaka na kuendelea na maisha yangu
Sasa wiki kama mbili zilizopita alinipigia simu kuniambia kuwa amejifungua na huyu mtoto ni wa kwangu. Yaani kanishangaza sana na bahati mbaya sikumbuki lini tulishirikiana tendo la ndoa wakati ule wa sekeseke la talaka kwani sikuwa na hamu kabisaaa na mapenzi tena. Na mbaya zaidi ananisistiza kuwa hata yule mtoto wa kwanza ni wangu pia kwani zile zilikuwa hasira tu kuniambia maneno yale na pamoja kuwa alinihakikishia mbele ya mama yake kuwa yule mtoto si wangu
Wanajamii hebu nipeni ushauri huyu mwanamke ni mkweli kweli au ni muongo? Maana navyojua ukweli wa baba wa mtoto anaujua mama mwenyewe! Na pili, moyo wangu kimahabba kwake na mtoto ulishakufa kabisaaaaa sina hata chembe ya upendo nao japo sina chuki nao. Hivyo ukisema tukapime DNA naona hata kama itaonyesha nina uhusiano nao lakini siwezi tena kuwa na upendo kama wa mwanzo
Pili, kule ofisini kazi hajaacha je uhusiano na huyo bosi aliemuweka hautakuwa unaendelea?
Tatu, nini hasaa kinachomrudisha kwangu na kujiliza usiku na mchana kubembeleza turudiane au tuendelee na maisha kama zamani? Kwa sababu kwa mtazamo wangu aliamini ukiwa na pesa basi ndo maisha umeyaweza?
Naishia hapa labda na wenzangu mna neno la ushauri
Ukiamua kupima hiyo dna... usipime hospitali yeyote nchini.. vuka mipaka
 
Back
Top Bottom