Ushauri kati ya biashara ya hardware au pharmacy wholesale

Ushauri kati ya biashara ya hardware au pharmacy wholesale

Habari wandugu
Je kwa mtaji wa 50-65 ml ni biashara gani nzuri kufanya kati ya pharmacy na hardware. Natakuliza shukrani
Pharmacy je wewe una taaluma yoyote inayohusu famasi ama unategemea kulipa na kuajiri?
Hio pesa inatosha kwa kuanzia maana around 10-20m itaisha kwenye premises ukaguzi na vibali
 
Unaweza kujitutumua kumshauri mtu, kumbe yupo kwa shemeji ameshiba ugali akaona achangamshe jukwaa !

Kama hujui ufanye nini na hio 65m uliiokota ama ulibeti ukala ?
Shida ndio hio . Mawazo negative. Usitafutee sijaomba kuulizwa nilipoitoa . Ukiona una cha kushauri kaa kimwa . Na zaidi unawezafanya fanya biashara fulani ukapata mpungu na ukatafuta income source zingine . Try be positive
 
Pharmacy je wewe una taaluma yoyote inayohusu famasi ama unategemea kulipa na kuajiri?
Hio pesa inatosha kwa kuanzia maana around 10-20m itaisha kwenye premises ukaguzi na vibali
Hapana. Natarajia kutafuta waatalamu . Mm nikaset mifumo ya stock record na monitoring. Kama tally
 
Habari wandugu
Je kwa mtaji wa 50-65 ml ni biashara gani nzuri kufanya kati ya pharmacy na hardware. Natakuliza shukrani
Fanya utafiti wako binafsi sehemu ulipo. Ukishagundua nini kinalipa zaidi na unaweza kukisimamia fanya hicho. Hata muuza majeneza anaona biashara yake ndo nzuri na inalipa zaidi.
 
Punguza uongo mkuu. 10m iishie kwenye vibali? Kama hujui kitu kaa kimya.
Nime generalize vibali na kuandaa premises bro, mbona comment ipo wazi hapo? Kuita wakaguzi na logistics zingine inaweza fika huko boss hujalipa pharmacist superintendent huyo pekee kuweka cheti ana demand kwanzia 1m, busness permit bado mambo ya kodi
 
Unaweza kujitutumua kumshauri mtu, kumbe yupo kwa shemeji ameshiba ugali akaona achangamshe jukwaa !

Kama hujui ufanye nini na hio 65m uliiokota ama ulibeti ukala ?
Yaani wewe kupanga geto la elfu 40 ndo unaona ushamaliza maisha. Don't be too negative
 
Muhimu ni location ....
Hardware kama utapata sehemu ndio mji unaanza kujengeka, utapiga sana pesa.
Kwa dsm hardware inalipa kila mahali, kipindi hiki mji wa dsm uko katika reform, maeneo mengi nyumba zinavunjwa na kujengwa upya kisasa, maeneo kama msasani, hardware zinafanya vizuri mnoo
Mwenge hardware zinafanya vizuri sana
Kinondoni hardware zinafanya vizuri sana
 
Back
Top Bottom