Ushauri juu ya mabati imara ya kuezeka nyumba

Ushauri juu ya mabati imara ya kuezeka nyumba

Habari zenu wadau.

Kwa muda sasa tangu haya mabati ya rangi tofauti yameingia (maarufu kama mabati ya south) makampuni mengi yamewekeza kwenye biashara hii.

Changamoto niliyokutana nayo ni kwenye uimara wa hizi rangi za mabati na mabati yenyewe. kwa utafiti wangu wa kawaida usiotumia utaalamu wowote, karibu kila nyumba tano ninazoona zenye mabati ya rangi moja kati ya hizo rangi yake imeanza kufifia na bati kupauka na kupoteza ule muonekano wa awali.

Ukienda madukani wanakwambia mabati yao ni origino, jeshini nako nasikia si kuzuri.

Nimepita kwenye baadhi ya thread kipindi cha nyuma nikakuta watu wanasema alaf ndo kinara wa mabati imara. ila nimeongea nao, kwa kweli bei imechangamka sana. ila wanasema mabati yao yako imara na ni ya uhakika.

Kuna mabati mengine yanatoka china na mengine yanatoka nadhani korea, bei zao kidogo ni nafuu ila naogopa sasa nisije nikaingia choo cha kike wakati nimeshaona changamoto iliyopo.

Naomba kwa wenye uzoefu wa mabati yatokayo nje ya nchi au haya ya alaf na mengineyo pamoja na bei zake na pia mafundi wa kuezeka mipe ushirikiano wenu kujua;

  • Aina ya mabati
  • Bei zake
  • Upatikanaji
  • Usafirishaji wake
  • Ufundi na gharama za kuezeka wastani wa ukubwa wanyumba ni 148sm
Napenda vitu imara origino na genuine. ila pia bei iwe relative.

Natanguliza shukrani kwa wote watakaokuwa tayari kutoa ushauri na uzoefu wao.

Ahsanteni sana.

Nawasilisha.
Nenda Aluminium Africa wao ndio wana mabati bora huuza kutokana na vipimo vya nyumba yako na kwa meter ,kwa mikoani wana viwanda vyao vidogo ambavyo hukata hizo metal ream ambazo zina rangi tayari sio za kupaka ,mimi nilitumia kama milioni 7 kwa nyumba yangu kubwa na zimebaki bati 25 hizo za mgongo,lakini ukitaka za kawaida za rangi kwa bundle ni kama laki 3 hivi mimi nilitumia bati hizo za kawaida kwa kuzikunja kuwa kofia ,na zinapendeza kweli.Kama ungekuwa Mbeya nenda pale kwenye kiwanda Mwanjelwa na kama upo Dar nenda kiwandani Pugu road.Na kidogo bati nyingine nzuri ni za Korea na India,tahadhari usiende kununua za dezo jeshini,ikija mvua ya masika utaisahau nyumba yako
 
Hata mimi nilipata shiida sana kuamua ninunue mabati aina gani na kutoka kiwanda gani. Nilianzia kiboko hadi viwanda vya Wachina. Bei zao zinashawishi sana .
Mwisowe nilipiga moyo konde nikaingia Alaf japo nei yao ni kubwa lakini unapata value for money .
Nakushauri kama unataka kutumia bati hizi xa Msouth tumia bati za Alaf nenda pale kiwandani kwao watakuonyesha tofauti ya bati zao na hizo za wachina.Pia kuhusu bati za Alaf zinakuja zikiwa na rangi tayari wanachofanya wao ni kuweka migongo kutegemea aina unayotaka. Wachina wanaweka mogongo halafu wanapuliza rangi.
Ukikosea kwenye bati ni vigumu na gharama kufanya marekebisho.Chezea ukuta na sio paa. Usifanye majaribio kwenye nyumba kwani yawezekana baadaye usiwe na uwezo wa kujenga nyumba nyingine
Unayosema nikweli kabisa,ukiwa Mbeya nenda pale Mwanjela Aluminium Africa wana kiwanda chao cha kuyaweka migongo hayo mabati wao huleta metal ream ambazo zina rangi tayari na si kupuliza wao hukuwekea migongo au kufanya ya kawaida kwa vipimo vyao ni expensive lakini ni thamani nzuri ya pesa,na kwa Dar nenda kwenye kiwanda pale Pugu rd,baada ya kufanya utafiti wa mabati niliamua niingie gharama ninunue hayo mabati ya AA na sijajutia uamuzi wangu kuna mwenzangu alipenda unafuu pamoja na kuwa na fweza ,tayari nyumba yake inaonekana ya mwaka 47,anajuta.
 
Nenda Aluminium Africa wao ndio wana mabati bora huuza kutokana na vipimo vya nyumba yako na kwa meter ,kwa mikoani wana viwanda vyao vidogo ambavyo hukata hizo metal ream ambazo zina rangi tayari sio za kupaka ,mimi nilitumia kama milioni 7 kwa nyumba yangu kubwa na zimebaki bati 25 hizo za mgongo,lakini ukitaka za kawaida za rangi kwa bundle ni kama laki 3 hivi mimi nilitumia bati hizo za kawaida kwa kuzikunja kuwa kofia ,na zinapendeza kweli.Kama ungekuwa Mbeya nenda pale kwenye kiwanda Mwanjelwa na kama upo Dar nenda kiwandani Pugu road.Na kidogo bati nyingine nzuri ni za Korea na India,tahadhari usiende kununua za dezo jeshini,ikija mvua ya masika utaisahau nyumba yako
Mkuu unaweza kuweka bei zao kwa haya mabati ya migongo mipana?
 
Mm nimeulizia bei ya ya kigae nabaki afrika pc moja sh alf 20 yenye sm 120 hiyo ndio ya chin kuna mpaka sh 27 alf kwa pc ya sm 160 bei ni kunwa balaa
 
alaf ndio bati sahihi nyingine yote ni mizoga tu, jua miaka mitatu utaona kila aina ya rangi
 
alafu mita moja ya migongo mipana wanauza tshs 12 mpaka upate futi tatu ambalo ndio bora ni 36 kila bati, kama nyumba yako ni kubwa ambayo ni square meta 500 utachukua bati 135 x 36 = calculate mwenyewe hapo, hapo utapata gutters 50 na cofia 60 hapo umemaliza paa
 
Duh mabati ni stress sana tatizo product feki kibao sometime nawaza kuishi kikushi nitoe kitu changu cha makuti maisha yaendelee
 
Unayosema nikweli kabisa,ukiwa Mbeya nenda pale Mwanjela Aluminium Africa wana kiwanda chao cha kuyaweka migongo hayo mabati wao huleta metal ream ambazo zina rangi tayari na si kupuliza wao hukuwekea migongo au kufanya ya kawaida kwa vipimo vyao ni expensive lakini ni thamani nzuri ya pesa,na kwa Dar nenda kwenye kiwanda pale Pugu rd,baada ya kufanya utafiti wa mabati niliamua niingie gharama ninunue hayo mabati ya AA na sijajutia uamuzi wangu kuna mwenzangu alipenda unafuu pamoja na kuwa na fweza ,tayari nyumba yake inaonekana ya mwaka 47,anajuta.
Sasa Mfianchi kwa vipimo vya mita au futi na kama kwa mita, mita moja bei gani na kama futi, futi moja bei gani pia
 
alafu mita moja ya migongo mipana wanauza tshs 12 mpaka upate futi tatu ambalo ndio bora ni 36 kila bati, kama nyumba yako ni kubwa ambayo ni square meta 500 utachukua bati 135 x 36 = calculate mwenyewe hapo, hapo utapata gutters 50 na cofia 60 hapo umemaliza paa
Mkuu software hizi calculation zako kama nataka kuzijua vizuri zaidi

Kuna uhusiano gani kati ya Eneo la Mraba(square metres) na Idadi ya bati?

Je? Mtindo wa paa lako nalo hauta determine Idadi kamili ya bati
 
Sasa Mfianchi kwa vipimo vya mita au futi na kama kwa mita, mita moja bei gani na kama futi, futi moja bei gani pia
Bei za mita zinatofautiana na aina ya bati utakalochagua ila bei zinanzia 14,000 mpkaka 20,000
 
Je,kwa wastani wa siku ngapi order inakuwa imekamilika let say but 160?usafiri kutoka kiwandani ni mnunuzi au kuna ofa ya kiwanda?
 
Kwa Wastani ni masaa 72 ya kazi , Usafiri unajitegemea boss
Sawa mzee, nitakuja ila sijajua ni lini, hizi bati za siku hizi ni madoido, uangalifu ukiepukwa mtu unachukua urembo machoni lakini ubora sifuri.
 
Back
Top Bottom