MWANASIASA HURU
Senior Member
- Oct 4, 2012
- 180
- 240
Habari zenu wadau.
Kwa muda sasa tangu haya mabati ya rangi tofauti yameingia (maarufu kama mabati ya south) makampuni mengi yamewekeza kwenye biashara hii.
Changamoto niliyokutana nayo ni kwenye uimara wa hizi rangi za mabati na mabati yenyewe. kwa utafiti wangu wa kawaida usiotumia utaalamu wowote, karibu kila nyumba tano ninazoona zenye mabati ya rangi moja kati ya hizo rangi yake imeanza kufifia na bati kupauka na kupoteza ule muonekano wa awali.
Ukienda madukani wanakwambia mabati yao ni origino, jeshini nako nasikia si kuzuri.
Nimepita kwenye baadhi ya thread kipindi cha nyuma nikakuta watu wanasema alaf ndo kinara wa mabati imara. ila nimeongea nao, kwa kweli bei imechangamka sana. ila wanasema mabati yao yako imara na ni ya uhakika.
Kuna mabati mengine yanatoka china na mengine yanatoka nadhani korea, bei zao kidogo ni nafuu ila naogopa sasa nisije nikaingia choo cha kike wakati nimeshaona changamoto iliyopo.
Naomba kwa wenye uzoefu wa mabati yatokayo nje ya nchi au haya ya alaf na mengineyo pamoja na bei zake na pia mafundi wa kuezeka mnipe ushirikiano wenu kujua;
Natanguliza shukrani kwa wote watakaokuwa tayari kutoa ushauri na uzoefu wao.
Ahsanteni sana.
Nawasilisha.

- Aina ya mabati
- Bei zake
- Upatikanaji
- Usafirishaji wake
- Ufundi na gharama za kuezeka wastani wa ukubwa wanyumba ni 148sm