Ushauri juu ya kukaa hostel au kupanga mtaani

mkomb

Member
Aug 31, 2023
21
31
Wanajukwaa poleni na majukumu ya kulijenga taifa letu.

Husika na kichwa hapo juu mimi ni mwanafunzi wa bachelor mwaka wa kwanza katika mwaka wa masomo 2023/2024 naombeni Ushauri wenu kati ya kukaa hostel au kupanga mtaani kipi Bora.

Naomba kuwasilisha
 
Wakati na mimi kipindi hicho naenda chuo nilikuwa na mawazo kama yako, ushauri wangu nenda kakae hostel za chuo na wenzako huko mtaani unapotaka kwenda kupanga kutakupotezea sana hela na muda wako, na usipokuwa makini unaweza ukajuta sana.
Umeona takwimu za afya za wanachuo ??
 
Wanajukwaa poleni na majukumu ya kulijenga taifa letu. Husika na kichwa hapo juu mimi ni mwanafunzi wa bachelor mwaka wa kwanza katika mwaka wa masomo 2023/2024 naombeni Ushauri wenu kati ya kukaa hostel au kupanga mtaani kipi Bora. Naomba kuwasilisha
Kwa mwaka wa kwanza kaa hostel ujenge urafiki na masomo bila kash kash nyingine za maisha. Pia inakusaidia kunetwork vizuri na wanafunzi wenzako.
 
Kaa hostel mwaka wa kwanza, mwaka wa pili upange.

Ama kama wewe ni mwenyeji wa mkoa unaosoma basi panga kama ni mgeni kaa hostel mwaka wa kwanza huku ukiusoma mchezo mwaka wa pili upange.

Mwisho, angalia wewe unataka nini na kama unaweza kukipata basi kifanye.
 
Nashukuru Kwa ushauri wako
Usifuate makundi ,mimi nimekaa miaka yote mwanzo mwisho getto la kupanga na msela kwa sabbu chuo chetu hapana hostel za kutosha zipo chache hta kwa wanafunzi wa mwaka wa kwanza wanapata 50% tu....Kama umefuata kusoma kaa hostel safi na usalama kama upo uhakika tulia .

Fanya kusoma mambo ya kupanga ni uzushi na hovyo.
 
Back
Top Bottom