Naombeni ufahamu kuhusu kozi ya Bachelor in Wildlife and Management Tourism

mkomb

Member
Aug 31, 2023
21
31
Habarizenu wanajukwaa,

Naombeni ufafanuzii kuhusu course tajwa hapo juu kuhusiana na kazi zakufanya baada ya kumaliza masomo chuona, chuo kipi Bora hapa Tanzania katika utoaji wa course tajwa hapo juu, upatikanaji wa ajira na je ninawezaje kujiajiri katika hyo course. Naomba kuwasilisha.
 
Bsc wildlife management/conservation not confused with a bachelor of tourism.
 
Iyo kazi nzuri ukiajiriwa serikalin mana ndo kuna maisha huko si mchezo ndo matanapa huko ila kuajiriwa serikalin ndo ishu kujiajir labda uwe tour guide kinyume na hapo sijui utajiajir vp yaan na chuo kizur n mwika au hata sua sio mbaya
Chuo kizuri ni MWEKA kipo Moshi Kilimanjaro
Ada yake itakua shughuli sana kama kipato chenu ni mnaamka na kuwaza mkanunue mkaa wa buku ndio mpike ..
 
Main employers Tanapa, ngorongoro, tawiri, Tawa. Mashirika kama WWF, FRANKFURT, NABU, WCC, na taasisi nyinine zilizobase kwenye masuala ya tafiti mbalimbali za wanyama pori.
 
Ikitokea ukapata nafasi kwenye hizo taasisi hapo juu basi we umasikini umeuaga na shida ndogo ndogo utazisikia kwa jirani tu. Changamoto ni kwenye kupata sasa.
 
Kwenye swala la ajira MWEKA ipo more favourable than SUA sababu jamaa wamespecialize sana kwenye field practical rather than SUA ambao wamebobea sana kwenye management (managerial positions) na kucheza na data.
 
Kwenye ajira battle kubwa ni MWEKA vs SUA hapa UDSM huwa anabaki kuwa mpenzi mtazamaji tu. anakosa muscles ya kucompete na hata waajiri ni mara chache sana kuopt wahitimu wa UD over hao rivals kwa upande wa hiyo course. So utaangalia where to go kama mfuko upo vizuri au una ufadhili basi nenda mweka, otherwise sua inakuhusu.
 
Kutokana na changamoto za ajira na nafasi kuwa finyu, wahitimu wengi (hasa mweka) wamejiajiri sana kwenye game ya utalii na kuwa madereva cruser/matour guide na kupiga pesa za mzungu, wengine wameenda mbali na kufungua makampuni yao binafsi (tour company) hapa sua wamekuwa wazito sana, nadhani mweka ile location ya kuwa karibu na exposed kwenye vivutio vya utalii na wageni wengi imewapa msukumo zaidi.
 
Apart from utalii kuna namna ukijiongeza zaidi unaweza liajiri kwenye shughuli za uhifadhi, hapa wengi bado wazito ila ukichanga karata zako vizuri basi unakuwa umehit jackpot. Hii nitakuja kuuanzishia uzi wake special kabisa, ngoja nimalizie hii chupa ya safari lager kwanza.
 
Apart from utalii kuna namna ukijiongeza zaidi unaweza liajiri kwenye shughuli za uhifadhi, hapa wengi bado wazito ila ukichanga karata zako vizuri basi unakuwa umehit jackpot. Hii nitakuja kuuanzishia uzi wake special kabisa, ngoja nimalizie hii chupa ya safari lager kwanza.
Kivip broh naomba madini hayo
 
Kivip broh naomba madini hayo
hahah kasome kwanza mkuu kwa sasa haitakusaidia kitu, unless ungekuwa graduant wa hii course ingekuwa inamatter kidogo. Kiufupi wenzetu rangi nyeupe linapokuja swala la uhifadhi wa mazingira, natural resources, climate change etc. currently kuna individuls na mashirika wana hela ambazo wanahitaji kufanya jambo katika hizo area so ni kwa namna gani unaweza kuzipata hizo pesa ndio ninachokizungumza, you get my point? Mimi nimeinvest muda na rasilimali nyingine katika kuhakikisha naconnect huo mrija wa pesa kwangu and it pay me off. Inahitaji nguvu, akili na uvumilivu though.
 
Habarizenu wanajukwaa,

Naombeni ufafanuzii kuhusu course tajwa hapo juu kuhusiana na kazi zakufanya baada ya kumaliza masomo chuona, chuo kipi Bora hapa Tanzania katika utoaji wa course tajwa hapo juu, upatikanaji wa ajira na je ninawezaje kujiajiri katika hyo course. Naomba kuwasilisha.
Management tourism ndiyo kozi gani boss?
 
Samahani mkuu mleta uzii kama ntakua navuruga mada. Wadau mimi pia nahitaji uelewa zaidi kuhusiana na upana wa ajira kwenye kozi ya Bachelor of environmental health
science au kujiajiri kwake maana nilileta uzi humu lakini sikupata ushirikiano
naomba kuwasilisha
 
Nipo kwenye hii field kwa miaka nane sasa kwa maana ya kuajiriwa na mojawapo wa hizi taasisi ( TAWA,TANAPA,NCAA),kwaiyo ushauri nitakaokupa uzingatie sana.

1. Ajira za Bachelor Degree kwenye hizi taasisi ni ngumu sana na ni adimu kuzitoa na hata zikitolewa zina competition kubwa sana maana unaweza kuta wanataka watu kumi tu na hizo nafasi zinaweza kutoka kwa interval hata ya miaka mitano hadi saba kwaiyo sasa ushauri wangu kwako kama utaweza achana na kusoma bachelor ya hii course nenda kasome Technician Certificate in Wildlife Management ambacho kinatolewa Chuo cha wanyamapori Pasiansi Mwanza utasomea mwaka moja tu ada yake ni Millioni tatu kwa huo mwaka moja baada ya hapo hautakaa sana mtaani kwa sababu ajira za Technician certificates na Basic certificates ni rahisi mno kutangazwa na pia kupata ni rahisi ila changamoto yake kwa hizi level wanaajiri wale wasiozidi umri wa miaka 25 tu.


2.Ukishapata ajira yako utajiendeleza mwenyewe au taasisi itakuendeleza(kukusomesha) kama utataka ukiwa ndani ya mfumo tayari na ndio maana ajira za Degree ni shida sababu wakishaajiri hawa wa elimu ya chini mara nyingi wanawaendeleza kielimu wale wachache wanaotaka au waliojiendeleza wenyewe ndio baadae wanakuja kukamata hizo nyadhifa za juu za uongozi hii inatokana na wanaamini watapata good results kutoka kwa wale viongozi waliotokea chini kuliko Degrees ambazo ni fresh from schools.

3.Huku kuna maisha mdogo wangu mimi nimeajiriwa na Basic certificate ila nimejikokota saivi nina Diploma yangu,Degree nawaza kupiga tourism Mgt ili niswitch kutoka wildlife kuingia Tourism nataka nideal na utalii zaidi sasa kuliko doria, Kwaiyo ukiingia huku na elimu yako ya chini hizo Degree utasoma tu hata usijali
 
Huo ushauri ni kama unataka ajira kwa maana ya kuingia kwenye mfumo wa hizo field ila kama unataka uwe tu na bachelor ya Wildlife halafu uanze kusotea ajira basi unaweza kufanya kile moyo wako unataka ila nakusihi kama unatokea familia zetu hIzi za kutegemewa au kutaka kuajiriwa basi anzia na elimu ya chini itakusaidia kupata ajira chap,

NB: Mshahara anaoanza nao mtu wa Technician certificate wa hiyo kada kwenye hizo taasisi ni mara mbili ya mshahara wa mtu mwenye Bachelor Degree aliyeajiriwa serikalini mwenye zaidi ya miaka mitatu kazini kwaiyo chaguo ni lako mdogo wangu

Karibu tupambane na majangili
 
Back
Top Bottom