Ushauri juu ya Ford explorena escape

musobogo

Senior Member
Sep 13, 2010
106
111
Habari zenu wakuu. Nimeona magari ford expore na ford escape yana bei nafuu na hata kodi yake sio kubwa sana. Kwa wenye uzoefu na hizi gari vpi kuhusu uimara wake, utumiaji wa mafuta , vipuri na mafundi wake.

Nimetamani kuwa nalo lkn ningependa kupata ushauri wenu wa kina.

Natanguliza shukrani kwa ushauri wenu.
 
Yani usifikirie kabisa hiyo gari kama we ni bahili wa pesa ya mafuta.

Hiyo gari ina Torque Speed na inakula mafuta balaa yani kutumia km 5 ka lita ni swala la kawaida kwa mjini mkuu.

Engine zake ni kubwa na kama nilivyosema zinakimbia sana na ulaji wake wa mafuta ndo unafanya ziwe na bei chini coz upo juu.

Unaweza kupata kwa Milioni 17 kama ukiagizia na show room ni more kidogo
 
Nashukuru sana kwa ushauri wenu.

Je ni gari gani nzuri ambayo ni 7 seaters kwa familia. Namaanisha hizi suv size ya kati.
 
Nashukuru sana kwa ushauri wenu.

Je ni gari gani nzuri ambayo ni 7 seaters kwa familia. Namaanisha hizi suv size ya kati.
Chukua Volvo XC90 nigari nzurii sana chukua ile yenye CC 2500. Hutajuta ushaurii wangu kwanza imekaa poa sana na ina seatrs 7
 
Chukua Volvo XC90 nigari nzurii sana chukua ile yenye CC 2500. Hutajuta ushaurii wangu kwanza imekaa poa sana na ina seatrs 7
Vipi kuhusu spear na ulaji wa mafuta. Kwa mtu wa kawaida anaimudu kuifanyia matengenezo yake yanvyotakiwa. Maana napenda kutunza vitu vyangu viwe safi muda wote.
 
Nashukuru sana kwa ushauri wenu.

Je ni gari gani nzuri ambayo ni 7 seaters kwa familia. Namaanisha hizi suv size ya kati.

Mkuu 7seaters ni gari ndogo sio za juu kama unavyomaanisha mfano Spacio New Modelunapata 7seaters

Ila kama una budget ya 25M to 30M unaweza pata hii gari Suzuki Escudo I repeat Suzuki Escudo with engine TD54W ya CC1990. Narudia tena simaanishi Suzuki Grand Vitara maana zinafanana na vitara nyingi zina engine kubwa kwahiyo utaingia matatizoni

Spares zipo available na inatumia mafuta vizuri kama 9km per Lita na ukiendesha vizuri unaenda kilomita nyingi zaidi kwa lita

suzuki_escudo_a1217867587b1937661_orig.jpg

suzuki_escudo_a1217867587b1937661_4_orig.jpg
 
Mkuu 7seaters ni gari ndogo sio za juu kama unavyomaanisha mfano Spacio New Modelunapata 7seaters

Ila kama una budget ya 25M to 30M unaweza pata hii gari Suzuki Escudo I repeat Suzuki Escudo with engine TD54W ya CC1990. Narudia tena simaanishi Suzuki Grand Vitara maana zinafanana na vitara nyingi zina engine kubwa kwahiyo utaingia matatizoni

Spares zipo available na inatumia mafuta vizuri kama 9km per Lita na ukiendesha vizuri unaenda kilomita nyingi zaidi kwa lita

View attachment 480156
View attachment 480158
Hata Klugger 2.4 ziko Poa sana
 
Hata Klugger 2.4 ziko Poa sana

Sure kluger hiyo 2.4 2AZ ni nzuri sana,na naipenda sana hiyo engine. sasa akikutana na wajuaji kama hajui anapigwa ile 1MZ ambayo ni 3.0 mbona ataita mama.

Na siku hizi wauzaji wa magari hasa kinondoni wanaweka label ya 2.4 nyuma ili wasiojua kukagua gari waingie mkenge kwenye hiyo 1MZ coz haziuziki yani watu wanapaki everyday hizo gari coz ya consumption kuwa kubwa sana.

Unakuta gari imewekwa badge ya 2.4 ukifunua kwenye engine unakutana na bonge la engine la 1MZ
 
Mkuu 7seaters ni gari ndogo sio za juu kama unavyomaanisha mfano Spacio New Modelunapata 7seaters

Ila kama una budget ya 25M to 30M unaweza pata hii gari Suzuki Escudo I repeat Suzuki Escudo with engine TD54W ya CC1990. Narudia tena simaanishi Suzuki Grand Vitara maana zinafanana na vitara nyingi zina engine kubwa kwahiyo utaingia matatizoni...
Shukrani mkuu. Hii Suzuki Escudo inapatika kwa 7 seaters?
 
Hata Klugger 2.4 ziko Poa sana
Shukurani kaka Mshana. Naomber ushauri wako tena. Kluger 2.4 na Suzuki escudo aliyoiongelea hapo juu. Hipi ni nzuri zaidi. Bajeti yangu haizidi 25m. Lkn nahitaji gari ya juu (midsize suv kama kluger na suzuki escudo) iwe ni 7 seaters.
 
Kama unaweza mvue mtu hapa mjini kwa sababu kuna watu kibao wanauza gari nzuri tu kwa bei za kutupa ambayo ni more than half price ukiagiza Japan na kulipia ushuru.
 
Shukurani kaka Mshana. Naomber ushauri wako tena. Kluger 2.4 na Suzuki escudo aliyoiongelea hapo juu. Hipi ni nzuri zaidi. Bajeti yangu haizidi 25m. Lkn nahitaji gari ya juu (midsize suv kama kluger na suzuki escudo) iwe ni 7 seaters.

Mkuu go for any hapo juu ila Suzuki ni more comfortable na luxurious kuliko kluger 2.4 ya budget hiyo.

Matumizi ya mafuta hayapishani sana kutokana na wewe mwenyewe kwenye kupiga pedal.

7Seater sijawahi ona kwenye hizi gari labda uamue mwenyewe kutengeneza siti huko nyuma kwenye mizigo, maana wenzetu wakiwa na mahitaji huwa wana customise vizuri tu na kuoneza siti utadhani imetoka kiwandani.
 
Back
Top Bottom