Ushauri: Je, nimfanyeje huyu Bw. Harusi mtarajiwa?

Ushauri: Je, nimfanyeje huyu Bw. Harusi mtarajiwa?

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Joined
Jul 13, 2013
Posts
63,761
Reaction score
128,257
Hivi huyu mwanaume nikimkandika mingumi ya haja na ya uhakika nitakuwa nakosea jamani?


  • Kadi yake ya mchango wa harusi kima cha chini kutoa ni tsh laki tano.
  • Mpaka sasa ana kama tsh milioni 20 lakini anataka afanye harusi ya tsh milioni 40.
  • Mke wake ni golikipa lakini ndiye anayempelekesha huyu mumewe mtarajiwa.
  • Mke wake kamwambia kuwa havai shela la milioni bali anataka la kuanzia milioni 5.
  • Jamaa mshahara wake wa mwezi take home ni tsh laki nane na kakopa milioni 5 benki ili aoe.
  • Nyumba wanayokaa wamepanga na jamaa hana hata kibanda na mpango wa kuwa nacho hana pia.
  • Kwa sasa ana hizo milioni 20 lakini leo kaja kunikopa milioni 2 ili alipe kodi wakati mchango wake sijamaliza.

Hivi nyie wanaume wenzangu kwanini mnapenda sana kupelekeshwa na hawa mademu zenu pasipo mpango? kinawashinda nini kuwakomalia tu na kuwapa ukweli wa maisha ili wawaelewe? mbona mnakuwa wadhaifu kiasi hiki?

Na nyie dada zangu kwanini mnapenda kutufanya sisi wanaume ni "mapoyoyo " wenu? Hivi nyie hali ngumu hii ya maisha hamuioni? mbona mama zenu hawakuwa materialistic hivi kwa baba zetu kama mlivyo nyie siku hizi? nani kawarogeni?

Huyu jamaa ndiyo anatoka ofisini kwake sasa anakuja kwake na kanitumia meseji kuwa anakuja kwangu ana mazungumzo na mimi ya kumkopesha hizo hela ili alipie nyumba yake na cha kushangaza na kusikitisha ni kwamba hata hali yangu ya maisha anaijua jinsi ilivyo ngumu na kidume ninavyo hustle na maisha haya.

Naombeni tu ushauri wenu je nimfanyeje huyu bwana harusi mtarajiwa? Yaani nimeshikwa na hasira mpaka basi na ukizingatia leo nimeenda mjini na nimetoka kapa na balance niliyonayo ni hiyo hiyo Tshs milioni 2.

Hivi huku siyo kutukanana matusi ya rejareja members wenzangu?

Naomba kuwasilisha..
 
Hivi mtu akiomba mkopeshe ni lazima umpe...?...just trying to think outside the box...!
 
Wewe nawe ni mbea umejuaje yote hayo ya mwanaume mwenzako??? utajibu ni rafiki yako anakuambia kila kitu! kweli wewe ni rafiki yake kweli na umbea wote huu unaomletea huyo rafikio jamvini?
 
Mke ni wake peke yake hivyo akomae kivyake.. kama huna pesa usimpe,, akizingua mchane makavu kama ulivyoandika humu.
 
Mhhhhhhh kwani 2.0m yeye ndo alikuwekea benki? maana inaonesha kana kwamba anazijua hizo m2 zako. Potezea tu, kumkopesha mtu si must.
 
Umelazimishwa kuchanga toa kile unachoona unahitaji kutoa....hayo yakuleta anakukopa hayana maana sana sana unamuumbua unayedai rafikio
 
Hahaaaa.., kama sinema vile.., a.k.a life in the movies!!
 
asisingizie mwanamke yeyee naye anapenda hiyo harusi. muulize yeye atavaa suti ya Tsh ngapi?. kuna wanaume wanapenda sherehe hadi aibu.
 
Wewe ndo ulitakiwa uwe rafiki ake kwa wakati huu...
Kwani urafiki ni wa pombe tu?, unashindwa nini kumuweka kitako na kumueleza hali halisi??
 
Izo milioni ishirini si atoe kumi agungue duka kumi afanye harusi???
 
Ushajua.kua huyo mtu akili zake fupi mwambie sina.mbona.neno dogo.sana.au unataka.kujionesha kwake kua unazo.acha kuogopa.watu
 
Back
Top Bottom