Ndugu
Yogati,
Natofautiana kidogo na baadhi ya wachangiaji kuwa wewe kueleza kuhusu 'site' ya mpenzi wako wa zamani ndiyo sababu tosha ya kukufanya 'umtake'..maana ninaitafsiri(ni ukaribu fulani ndani ya mji mmoja(city) wenye kukufanya utake kumuona kila leo! yaani kuwepo hapo jirani kunakufanya ushawishike zaidi kutaka kumuona kuliko alipokuwa Mwanza kama zamani.
Hata hivyo kuna vitu unapaswa kuzingatia.
1. Kwanini mliachana na huyo mpenzi wako wa zamani?
-Kusema kirahisi tu, kuwa, "tuliachana bila ugomvi" haimaanishi mrudiane!Umesema kuwa 'umbali' ulichangia, ikimaanisha kulikuwa na sababu hasa kuu na si umbali.
2. Hisia zisizoeleweka.
-Kunatofauti kati ya Kupenda , Kutamani, Kukosa(Miss), na kukumbuka.
Sijui unamaanisha nini kati ya hivyo..lakini iwapo utasema kuwa unampenda naomba ujiulize haya,
-Huko 'kupenda' unakosema, kulikuwepo kabla au kumeanza baada ya kuambiwa na dada yako?
-Iwapo ungeletewa taarifa kuwa bado anakupenda tena ukiwa umeshaolewa ungeendelea kumchukulia hivyo?
-Unategemea nini kwa mchumba wako wa sasa iwapo akijua kuwa unataka kuanzisha mahusiano based on hisia usizozielewa tena wakati wa uchumba?.
3. Tabia:
- Je, unajua huyo mpenzi wa zamani alikuwa na mwenendo gani?
-Iwapo anataarifa kuhusu ndoa yako(presuming,since kama anakupenda na kutaka mrudiane ameshakufuatilia na kujua), Unadhani atakuchukuliaje wewe hasa MSIMAMO wako kupitia suala tu la kutaka kuonana kwa haraka namna hiyo?
'Memories'..tulia, tazama unataka nini..kisha chukua uamuzi lakini so far, endelea na mipango yako ya ndoa maana yaliyopita si ndwele! Ukisema kila mtu amrudie mpenzi wake kwa sababu tu hawakuachana kwa ugomvi, kuna watu watamiliki mtaa/vijiji.
Goodluck.