Ushauri wenu wakuu katika hili kama familia tumebaki njia panda

Mmea Jr

JF-Expert Member
May 20, 2016
551
1,222
Habari zenu wakuu ?, kwanza napenda kuwapa pole kutokana na uchovu utokanao na majukumu mbali mbali ya ujenzi wa taif letu . Lakini pia napenda kuchukua nafasi hii kuwakupusha ndugu zangu kuwa Corona ipo hivyo tuendelee kuchukua tahadhari mbali mbali zinazoweza kutusaidia kujikinga kama inavyoshauriwa na wataalumu wa afya.

Moja kwa moja kwe mada .

Miaka 4 iliyopita kaka yangu alingia kwenye mahusiano na mwanamke mmoja ( nisingependa andika jina lake humu) , wakati mahusiano haya yanaanza kaka yangu alikuta mwanamke huyu tayari akiwa na mtoto mmoja wa kike ( binti ambaye anaumri wa miaka kaa 11 au 12 hivi kaa sijakosea ) . kipindi hicho chote mwanamke huyu hakuwa na mawasiliano yoyote na mzazi mwenzie (kwa mujibu wa bro) lkn baba wa binti huyu alikiwa yupo hai akiendelea na maisha yke huko . mahusiano yaliendele na kaka yangu aliamua kwenda kujitambulisha kwa wazazi wa huyu mwanamke na wakampokea vzr tu na kumtambua bila shida.

Baadae mwanamke huyu alishika ujauzito na kujifungua mtoto wa kiume akiwa anaisha na kaka yangu , baada ya kujifungua hapa ndyo shida ilianza , mama mkwe ( mama wa binti ) alimtaka kaka yangu amtolee mali mwanamke huyu , kaka yangu hakulikataa ombi hili lkn aliomba apewe muda kidogo coz financially haku vizuri kwa wakati huo.

Maisha yaliendelea baina ya wawili hawa mbaka mtoto akatimiza umri wa mwaka mmoja , baada ya mtoto kutimiza umri huu kaka yangu alipata taarifa kuwa shemeji ( yani mwanamke aliyekuwa anaishi naye ) amekuwa akionekana mara nyingi na mwanaume mwingine . kaka yangu hakutaka kulikurupukia jambo hili kwani alijipa muda wa kutosha kulifanyia uchunguzi , mbaka hapo alipopata uwakika kuwa ni kweli mkewe amekuwa akionana na Mwanaume mwingine ambaye alikuwa ni baba wa yule binti ambaye nimemuelezea hapo mwanzo.

Baada ya hili walijaribu kuliongelea swala hili lakin mahusiano yao design kaa yalikuwa yashaingia mdudu kwani kulikuwa na mivutano ya hapa na pale kama mnavyoelewa tena changamoto za mahusiano especiay pale kunapoenekana kuna dalili za usaliti ndani yake . Sasa kilichonileta kwenu wakuu ni hili

Wiki iliyopita yule Baba wa yule binti niliyemuelezea hapo mwanzo ( mtu wa kwanza kuzaa na mwanamke anayeishi naye bro ) kaenda na mali kwa wazazi wa mke wa kaka yangu ( mtanisamehe sijui kaa nipo sahihi kumuita mke coz mali haijatolewa mbaka muda huu ) . kuwa yeye yupo tayari kumtolea mali huyu mwanamke anayeishi na kaka yangu na kumchukua ili akaishi naye , lakini kama hili halitoshi jamaa akaenda mbali zaidi akidai hata huyu mtoto wa pili wa huyu mwanamke ambaye alipatika wakati huyu mwanamke anaishi na bro vile vile ni wakwake . Hivyo anataka Kaka yangu amuachie amchukue ili wakaishi naye .

Sisi kama familia tukajua jamaa ( mume mwenza na bro , baba wa yule binti ) hayuko serious anataka tu kumpressurize kaka yetu lakini ikabidi tuanze kuchunguza kimya kimya sisi kama familia sasa bila kumshirikisha kaka yetu sababu hatukutaka awe na stress za aina yoyote juu ya jambo hili ukizingatia tayari mtoto anaishi naye na kashamlea mbaka kafikia hatua mtoto anatembea anaoengea na kumtambua Kaka yetu kama Baba na mimi kama Baba mdogo .

Sasa kituko kinakuja hapa , baada ya uchunguzi wa kimya kimya uliofanywa na dada zangu wamegundua kuwa baadaya ya vuta ni kuvute ya hapa na pale ya maneno baina ya Kaka yangu na huyo mume mwenza juu ya huyu mtoto wa kiume ambaye ni wapili kwa huyu mwanamke ,huyo mume mwenza aliamua kwenda kushita kwa mwenyekiti wa mtaa ambao huyu mwanamke alikuwa anaishi pamoja na wazazi wake . jambo lilipolekea huyu mwanamke aitwe na mwenyeketi wa huo mtuu na kukalishwa kikao ambacho kilihusisha huyu mwanamke familia yake pamoja huyo mume mweza wa kaka yangu .

Chakushangaza baada ya mwanamke huyo kuuliza mtoto wapili aliyeza ni wanini kati ya kaka yangu na huyo mume mwenza huyu mwanamke alijibu ni wa huyo mume mwenza . Mwenyekiti akamtaka aweke sahihi kabisa kwa alichokisema na kukiandika akaweka na dada zangu wamefika hadi kwa mwenyikiti na kawaonesha hayo maelezo pamoja na sahihi kabisa . Just Imagine huyu mwanamke amekuwa akiishi na bro for more than 5 yrs now but still she have all the guts to do this to my brother ? , bro amekuwa akimlea kwa upendo sana huyu mtoto muda wote huo ambao wamekuwa pamoja , mtoto anaumwa, mtoto anasumbua tunaangaika but still she is coming up with this non- sense , really ?,

Sasa basi kama familia kesho kutwa ndyo tunaitwa kwenda kujadili hatima ya huyu mtoto pamoja na familia ya upande wa pili lakin bad enough mbaka muda huu naandika hapa kaka yangu hana habari na kinachoendelea nyuma ya pazia we are all quit coz hatupo tayari kumuona akipitia maumivu makali ambayo yapo mbele yake .

Lengo la kuileta hii kwenu nilikuwa naombeni msaada au njia ambao tunaweza kutumia ili kudhibitisha ukweli wa mtoto juu ya hili jambo maana kwa namna yoyote najua kaka yangu hata kuwa tayari kumkabidhi huyu mtoto eti kwa kukuwa mama yake kasema huyu siyo mtoto wake .

Napenda nitangulize shukurani zangu za dhati kwa wotee ambao watachangia maoni yao kwa namna moja au nyingine ushauri wenu ni wamuhimu sana kwa niaba ya kaka yangu na familia yangu kwa ujumla .
 
Mwenyekiti wa mtaa,mke,mume wa kwanza,polisi,jamii,kaka yako,wewe au yeyote yule hata mahakama yenyewe vyote hivyo havina haki ya kusema kuwa huyo mtoto ni wa nani.Mwenye haki ya kusema huyo mtoto ni wa nani ni DNA test tu.Kwenda kumsikiliza mwenyekiti wa mtaa ni uwendawazimu wa kiwango cha lami.Kama DNA test itafanyika na kubaini kuwa mtoto siyo wa kaka yenu basi cha kufanya daini malipo ya malezi ya huyo mtoto kisha achaneni na uchafu wote kwa kumwacha huyo mwanamke akaolewe na jamaa yake wa mwanzo.

Hitimisho:Nikiwa mkubwa nitakuwa mwanaume kwelikweli,a man of decision yaani mwanaume wa kufanya maamuzi magumu.
 
Mwambieni kaka yenu ajibidishe kwenye kutafuta hela huyo Mrupo na mtoto aachane nao kwanza pampers zimepanda bei.Kama baba DIAMOND wa mwanzo katundika daluga sembuse huyo kaka yenu.Akishindwa kuelewa muanzisheni dozi ya K VANT mtakuja kunishukuru.
 
Njia sahihi ya kumjua baba halali was huyo mtoto Ni DNA tu.

Lakini mnaweza kumuomba mama wa mtoto awe mkweli tu maana katika hali ya kawaida mama ndie mwenye kujua baba halali wa mtoto.
 
Aiseee hii kali. Nimeshindwa nishauri nini ila natamani watu wa sheria watoe muchango yao hapa ili kk yako alipwe stahiki zake zote mana hakuna haja ya DNA coz mama wa mtot kakiri huko kwa mwenyekiti. So kilichobaki n sheria kuchukua mkondo wake tu bc no more
 
Mbaka hapo mimi kama Ticha wa Kiswahili Sijadhibitisha huyo mtoto awe wa nani.

nje ya mada;

hivi ninyi wakati tunafundishwa kusoma na kuandika mlikuwaga mnaenda wapi!? Huwezi kuandika neno Kuthibitisha au Mpaka!? Ukiulizwa unajitapa kabisa ni mhitimu pia wa chuo kikubwa nchini! Pathetic
 
Hamuwezi kuthibitisha mtoto ni wa nani bila kumshirikisha kaka yenu labda kama ni copyright ya Kaka yenu. Umeshamuona mtoto? Anafanana na kaka yenu au yeyote katika familia yenu? Kama hafanani basi wa kuamua hili sakata ni DNA tu maelezo ya huyo kicheche na signature yake hayahusu kitu katika kuamua Baba halali wa huyo mtoto.
 
Mbaka hapo mimi kama Ticha wa Kiswahili Sijadhibitisha huyo mtoto awe wa nani.

nje ya mada;

hivi ninyi wakati tunafundishwa kusoma na kuandika mlikuwaga mnaenda wapi!? Huwezi kuandika neno Kuthibitisha au Mpaka!? Ukiulizwa unajitapa kabisa ni mhitimu pia wa chuo kikubwa nchini! Pathetic
Asante teacher, next time nitakuwa makini
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom