Dah! Kuna mambo yanatia hasira jamani

PetCash

JF-Expert Member
Mar 20, 2012
1,997
1,999
Kuna mshkaji wangu mmoja tulisoma wote. Katika harakati za kutafuta maisha tukawa tumepotezana kidogo. Jirani kidogo na nnapoishi kuna jamaa tumezoeana anaishi na familia. Na hasa mazoea yalianza kwa sababu mke wake huwa kwenye shughuli za utafiti huwa tumewahi kukutana mara kadhaa (Ila tunafanya kazi kwenye fields mbalimbali kabisa). Ikawa sasa jamaa kwenye shughuli nyingi za kijamii tunakutana na hata kuwa kwenye magroup ya social na hatimaye tukawa kwenye kugonga moja hot na washkaji tupo group moja.

Kipindi flani nyuma tulikua mkoa fulani kwa issues za kutafuna donor funds(maendeleo endelevu). Tulikutana taasisi mbalimbali na hata private companies. Mke wa jirani alikuwepo. Kukawa na rumors analala rum moja na bosi wake fulani hotelini(Yani bi dada hatumii hela ya accomodation if u catch my drift).

Kuna siku tulikuwa chimbo na masela mara yule bosi akaingia akakaa kona flani. Mara kidogo mke wa jirani kaletwa na boda. Kaenda kukaa kona na mshkaji. muda wote hawatuoni (Kwanza boss hatujui vizuri). Wakapeana vinavyodhihirisha hadharani kuwa sirini wanajuana. Nikacomfirm mke wa msela anamegwa. I didn't mind na nikapuuzia hiko kitu.

Kwenye semina hiyo hiyo nikakutana na yule mshkaji wa mwanzo tuliyesoma naye. Hapo yeye ni dereva wa boss wa taasisi fulani. Tulipiga story sanaa, akagusia kuna demu pale ni ex wake anamuwinda akumbushie. Baadae nikaja kujua ni mke wa yule jirani. Nikamwambia mshkaji wangu sasa hivi huyu kaolewa achana naye.

Yakaisha. Jamaa kapiga story na madereva wenzie wakamtonya yule analiwa na boss wake. Jamaa akaja kuniambia, hata kama huyu demu ana mume mbona anamegwa tu. Akaahidi kupambana, nikamwambia usije kuniambia chochote kuhusu yeye. Basi wakati wa kurudi toka mkoa huo, kwenye gari letu tunafanya review ya vilivyojiri, dereva wetu akatuhadithia jinsi dereva mwenzie (yule mshikaji), alivyokuwa anakula sahani moja na bosi fulani hadi wakatishiana maisha. Hapo sasa ndo nikafahamu yule mshkaji alifanikiwa.

Muda ukapita yule jirani yangu akafanya tukio (kupiga mkwanja) ofisini kwao akasimamishwa kupisha uchunguzi. Akawa yuko tu home, mkewe dharau kama zote. Nikawa namshauri avumilie tu, maana hakuna namna. Kuna kipindi akawa anahisi anamegewa, ila sikumwambia chochote. Katika watu tulio kwenye social group kuna jamaa akatuambia mke wa jirani analiwa na boss wake (Mhusika hakuwepo), ila wote tukakausha. Sasa jamaa(jirani) kwenye kupiga hela kuna vitu alimwambia mkewe.

Kuna siku mkewe kachelewa bila sababu yenye mashiko jamaa kamchapa makofi. Mkewe kesho yake akampigia simu mtu fulani kwenye kampuni ya mumewe akamueleza mishe jamaa alizopiga. Jamaa kesi na kazi ndo akafukuzwa. Tukajiorganise tukaongea na kampuni chini chini tukachanga kiasi kidogo, na jamaa naye akatoa kampuni ikamchomoa jamaa kwenye kesi coz uhusika wake ulikua mdogo sana.

Baadaye jamaa katika ugomvi na mkewe akaja jua mkewe alimchomea. Ss jamaa kuja kutuelezea washkaji wakawa wanamshauri ampige biti mkewe kisha wayajenge. Mi nlikuwa na hasira zangu nikamwambia jamaa, ingekuwa mimi ndo mke wangu ningepiga chini sasa hiv *****(pardon my french). Basi siku zikaenda, jamaa kasettle na mkewe maisha yakasonga.

Kipindi flani baadae mke wa jirani alipata msiba, tukaenda kama ilivyo ada ya ujirani/urafiki. wamemaliza msiba siku ya pili wakawa wanarekebisha matatizo ya ukoo na kupatanisha hapa na pale. Sisi wengine ikawa ni story tu tukisubiri kusepa.

Dada yake jamaa akanifata akiwa na hasira akilalamika kaka yake anakubalije matatizo ya ndoa kujadiliwa ukweni? Na akagusia jinsi ghafla nilivyoonekana sumu kutaka kuvunja ndoa takatifu. Na kweli nilitazamwa vibaya sana pale msibani ctakuja sahau! Kumbe jirani alimwambia mkewe ushauri wangu, mkewe akawa kajenga beef. Kila nikikumbuka kuonekana snitch mbele ya jamii dah!

Basi ndo ivo hata cku izi mtaani kuna wamaza wakinicheck wananiona snitch tu yani! Ss nashikwa na hasira balaa
 
Kikubwa uhai..ayo mengine waachie wenyewe kwanza hamna wanacho kuongezea
 
Write your reply...NDO UACHE U SNITCH MZEE BABA WE POTEZEA KUNA WANAUME WENGINE WAMEKAA KAMA MASHOGA WAMESHIKIWA AKILI NA WANAWAKE
 
Mambo ya kutoa ushauri uwa sio yaani unatoa ushauri mzuri kabisa mwisho wa siku unaonekana bure kabisa
 
CARPOZA"sasa snitch si must die!"
OKA"Hiyo snitch ndo nn"
CARPOZA"Najua baasi!"
OKA"sema ina sound good"

😂 joking tu wazee,ila mkuu pole sana kwa yaliyo kukuta, sometimes it's better to mind your own business...
 
Hahahaa ndio maana mimi huwa sitoi ushauri wa mahusiano... Mambo ya kumpa mtu ushauri anaenda kukuchomea nani anataka? Baadae uambiwe kisa wewe huna ndoa ndio unataka kuvunja ndoa ya mwenzio
 
PetCash pole sana , kinachokuumiza ni kitu kidogo , kwan Huamini kua ulifanya jambo sahihi?


Kama unamini ulitoa ushauri sahihi basi usijiumize ivo.


Kwenye maisha yetu kuna watu kupokea mashauri yakweli huwa ni tizi sana.

Fanya kuwavalia miwani, piga mishe zako , hao wamama wakitaani wanaokumind ni sababu wote wana tabia moja !!.


Embu fanya kuamini kua kuna mmoja alikuona umefanya jambo la maana sana, nahuyo mmoja, anatosha kukupa Faraja... ACHANA NA MAMBO YA "WANANIONAJE"...


nakupa MF wa karibu.. Sisi tuna Mjomba Wetu wa makamo tu,, alipoachana na mkewe mkubwa akapata Kademu Ka miaka 30+ ivi, yule demu ukimuona ni MTU kabisaa lkn kwenye harakati na mahali ya mizunguko, unakakuta kana kunywa pombee, kamevaa ovyooo , Mjomba akirudi Nchini ,basi katakaa mwezi mzima kametulia..Ila akishasafiri kanaanza , nasisi wana tukawa tunakutana nako tu mizunguko .



Aahhh bwana ,Ndugu yako ni ndugu yako, ilibidi tukae na Mjomba tumweleze.

Mjomba bana kumbe akarudi akamwambia Mkewe , kale kademu mazee kalituchukia sana Yan kalichukia kinoma ,wazee tukakata mguu Pale .....( si una maisha yako ?)


Yakaenda, Jamaa kasafir tena, kurudi akakafuma hahahahahha tena kana mwanaume ndani..... Alianzaga kututafuta nakutuomba msamaha weee, mwisho akarudiana na mke wake mkubwa, now wanakula Mafao !!.




Fanya kuwapuuza Jooh !! Izo hasira mwisho utaishia kujiona Choo!!....... Waivo huwa wanakuja kuelewa..


IN FACT ,USIACHE KUA SEHEM YA UPONYAJI KWA MTU ASOJUA KUA ANAUMIA, MWENYE AKILI ATAKUSHUKURU.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Fanya mpango mle huyo mke wa janaa maana huyu mshikaji wako hana adabu kbs mwanaume gani hana koromeo.
 
Back
Top Bottom