Ushauri: Amesema nimtafute tu msichana mwingine ila bado nampenda

AUTOCATALYST

Member
May 27, 2015
69
95
Nimekuwa na mpenzi wangu(mchumba) kwa takribani mwaka sasa, mara nyingi tumekuwa tukikwazana lakini tunasuluhisha na kusonga mbele. Ugomvi mkubwa hasa naweza sema ilikuwa pale alipoambiwa tu kwamba nilijaribu kumtongoza rafiki yake na alilazimisha tuachane lakini mimi ilinibidi kumueleza kweli yote na kumsihi asiyasikilize ya watu tena na alionekana kurudi nyuma na akakubali tuendelee.

Sasa ndugu zangu, kwa muda kama wa wiki mbili ulopita kutokana na vile alivyokuwa akiona namkosea mambo mengine madogomadogo nahisi alihisi huenda simpendi na ni kwa sababu ya Ex girlfriend wangu (japo si kweli na sina mawasiliano naye) nahisi alifikiria hivo kwa sababu siku fulani tulipogombana nilimtaja huyo Ex kwa kumwambia hiyo tabia alonionesha my Ex hakuwa nayo(nadhani hapa nilikosea).

Kutokana na hilo alianza kufuatilia namba za huyo Ex na akafanikiwa kuzipata na huyo Ex (ambaye kimsingi nilimuacha mimi)alimueleza mambo mengi kunikandia na mbaya zaidi alimweleza kuwa nilimtongoza tena nilipokwenda likizo nyumbani(Jambo nililonianya nishangae), baada ya hapo aliniita vizuri tu kama kuna amani na nilipofika aliniambia alichoambiwa kwa uchungu.

Nilionesha kuchoka kujitetea kwa jambo moja kwani angeniona muongo lakini ilinibidi nifanye hivyo ila hakuonesha kunielewa kwani hata kwenye simu aliniblock kabisa nisimpigie kwani alinambia hataki mapenzi tena ameumia sana, ilibidi niwatumie ndugu zangu hapo alionesha kuelewa na siku hiyohiyo alinipigia simu yeye kuniuliza nipo wapi na ninafanya nini, nilimjibu na baada ya hapo aliniaga kwa kusema "usiku mwema" cha ajabu ile asubuhi tu nilipompigia alikuwa akinijatia simu naalizidi kukumbushia ya nyuma yote (kwa meseji alidai mapenzi hataki tena).

Ilinibidi nimtafute ana kwa ana kidogo akaonesha kurudi nyuma tena na akaniomba tusubiri mitihani iishe tutazungumza, tuliendelea kuwasiliana hata kiss nilipomuomba alinipa lakini hakutaka nimuite mpenzi akidai bado moyo wake haujarejea katika mapenzi. Wakati huo wa mitihani tulishirikiana na niliendelea kumsaidia nikisubiri mitihani iishe tuzungumze kama alivyosema yeye.

Wakuu, tupo wote chuo na tunakaa hostel japo kwa sasa tumefunga na tulipofunga tu aliniaga anatoka kidogo kwenda kwa birthday ya rafiki ake nimsubiri hostel atarudi tuzungumze cha ajabu wakuu muda aloniahidi kurudi ulipita sana na nilipompigia simu alikata na alinitumia meseji kwamba msimamo wake ni uleule kama inawezekana nimtafute tu mwingine lakini yeye ahitaji tena kusikia mapenzi na tayari amekwisha ondoka yupo nyumbani(maanake hostel harudi) na kuanzia hapo niligundua kaniblock tena calls, whatsapp na jana kaniblock hata fb, nimekuwa nikimtumia meseji hajibu tena mpaka leo.

Wakuu naombeni ushauri wenu nifanye nini kiukweli nampenda. Wote naihitaji ushauri wenu kutokana na experiences zenu katika hili utanifaa sana.
 
pistmshai

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
1,315
2,000
Kuna wakati mwingine ku-give up ni ushujaa, maana muda mwingine huwa tunatakiwa kuyaacha baadhi ya mambo yapite na yabaki history za maisha yetu, huo pia ni ujasiri ambao ni zawadi waliobarikiwa watu wachache sana (be among them, man)

Trust me, nothing good gets away
 
Raynavero

JF-Expert Member
Apr 29, 2014
38,489
2,000
huyo mwanamke wako utapata shida nae sana huyoo kwa kua anasikiliza sana mambo ya nje na nimemtoa akili alivyompigia simu ex wako

ulikosea sana kumtongoza rafiki yake

na pia kitendo cha kumtaja ex wako mbele yake ulimuumiza kwa kweli

ushauri mpotezee kwa muda hivi usome mchezo km wako atarudi tu..
na kama siyo wako basi
 
Nashukuru kwa ushauri wako ndugu
 
Numbisa

JF-Expert Member
Dec 12, 2016
187,276
2,000
Fanya hivi
IMG-20170210-WA0022.jpg
 
Castr

JF-Expert Member
Apr 5, 2014
23,355
2,000
Mbele ya huyo utaishi kwa kujitetea kila siku katika mahusiano yenu, siyo nzuri sana hii kitu unapokua unataka mahusiano yenye afya.
Anaonekana kua nafasi ya kwanza ya kuanzisha ugomvi akiiona anaitumia hapo hapo, wakati mwingine ataitafuta makusudi.

Pia unaonekana ni dhaifu kwake au kuongea sana hauwezi.

Anaonesha bado anakupenda ila anahitaji kuendelea kushawishiwa, kama unampenda kiasi cha kutoyawazia niliyoandika hapo juu au kama utaweza kumbadilisha, bembeleza ataelewa tu.
 
kedekede

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
4,557
2,000
Nimekuwa na mpenzi wangu(mchumba) kwa takribani mwaka sasa, mara nyingi tumekuwa tukikwazana lakini tunasuluhisha na kusonga mbele.Ugomvi mkubwa hasa naweza sema ilikuwa pale alipoambiwa tu kwamba nilijaribu kumtongoza rafiki ake na alilazimisha tuachane lakini mimi ilinibidi kumueleza kweli yote na kumsihi asiyasikilize ya watu tena na alionekana kurudi nyuma na akakubali tuendelee.

Sasa ndugu zangu, kwa muda kama wa wiki mbili ulopita kutokana na vile alivyokuwa akiona namkosea mambo mengine madogomadogo nahisi alihisi huenda simpendi na ni kwa sababu ya Ex girlfriend wangu (japo si kweli na sina mawasiliano naye) nahisi alifikiria hivo kwa sababu siku fulani tulipogombana nilimtaja huyo Ex kwa kumwambia hiyo tabia alonionesha my Ex hakuwa nayo(nadhani hapa nilikosea).Kutokana na hilo alianza kufuatilia namba za huyo Ex na akafanikiwa kuzipata na huyo Ex (ambaye kimsingi nilimuacha mimi)alimueleza mambo mengi kunikandia na mbaya zaidi alimweleza kuwa nilimtongoza tena nilipokwenda likizo nyumbani(Jambo nililonianya nishangae), baada ya hapo aliniita vizuri tu kama kuna amani na nilipofika alinambia alichoambiwa kwa uchungu.Nilionesha kuchoka kujitetea kwa jambo moja kwani angeniona muongo lakini ilinibidi nifanye hivyo ila hakuonesha kunielewa kwani hata kwenye simu aliniblock kabisa nisimpigie kwani alinambia hataki mapenzi tena ameumia sana ,ilibidi niwatumie ndugu zangu hapo alionesha kuelewa na siku hiyohiyo alinipigia simu yeye kuniuliza nipo wapi na ninafanya nini, nilimjibu na baada ya hapo aliniaga kwa kusema "usiku mwema" cha ajabu ile asubuhi tu nilipompigia alikuwa akinijatia simu naalizidi kukumbushia ya nyuma yote(kwa meseji alidai mapenzi hataki tena).Ilinibidi nimtafute ana kwa ana kidogo akaonesha kurudi nyuma tena na akaniomba tusubiri mitihani iishe tutazungumza, tuliendelea kuwasiliana hata kiss nilipomuomba alinipa lakini hakutaka nimuite mpenzi akidai bado moyo wake haujarejea ktk mapenzi.Wakati huo wa mitihani tulishirikiana na niliendelea kumsaidia nikisubiri mitihani iishe tuzungumze kama alivyosema yeye.

Wakuu, tupo wote chuo na tunakaa hostel japo kwa sasa tumefunga na tulipofunga tu aliniaga anatoka kidogo kwenda kwa birthday ya rafiki ake nimsubiri hostel atarudi tuzungumze cha ajabu wakuu muda aloniahidi kurudi ulipita sana na nilipompigia simu alikata na alinitumia meseji kwamba msimamo wake ni uleule kama inawezekana nimtafute tu mwingine lakini yeye ahitaji tena kusikia mapenzi na tayari amekwisha ondoka yupo nyumbani(maanake hostel harudi) na kuanzia hapo niligundua kaniblock tena calls, whatsapp na jana kaniblock hata fb, nimekuwa nikimtumia meseji hajibu tena mpaka leo.

Wakuu naombeni ushauri wenu nifanye nini kiukweli nampenda..? Wote naihitaji ushauri wenu kutokana na experiences zenu ktk hili utanifaa sana.
Achana naye tafuta mwingine!Unahangaika nini?kwa nn anakuumiza?furaha inaanzia kwako,najua inavyochosha kujielezaeleza kila mara,kwa nn akamuamini mtu uliyemuacha au mliyeachana kuliko wewe mpenzi wake?tumia line nyingine mwambie umekubali afuate mambo yake hutamsumbua tena!Then ujikaze uendelee na yako!
 
AUTOCATALYST

Member
May 27, 2015
69
95
Mbele ya huyo utaishi kwa kujitetea kila siku katika mahusiano yenu, siyo nzuri sana hii kitu unapokua unataka mahusiano yenye afya.
Anaonekana kua nafasi ya kwanza ya kuanzisha ugomvi akiiona anaitumia hapo hapo, wakati mwingine ataitafuta makusudi.

Pia unaonekana ni dhaifu kwake au kuongea sana hauwezi.

Anaonesha bado anakupenda ila anahitaji kuendelea kushawishiwa, kama unampenda kiasi cha kutoyawazia niliyoandika hapo juu au kama utaweza kumbadilisha, bembeleza ataelewa tu.
Duh ahsante mkuu, nahisi kumbadilisha itawezekana kama atakubali kurejea kwa sababu yapo mapungufu mengi nilomkosoa akakaa sawa.
 
jolya002

Senior Member
Nov 5, 2014
154
225
Mkuu piga chini for good.huyo kesha amua kuto kukuamini hivyo hatokuamini kamwe.chamsingi endelea na maisha yako kwa muda utapata mwingine.pia utakapo pata mwingine uchunge ulimi wako.kwani "usitumie matofali na misumari ya nyumba ya zamani kujenga nyumba mpya"hope umenipata
 
AUTOCATALYST

Member
May 27, 2015
69
95
Mkuu piga chini for good.huyo kesha amua kuto kukuamini hivyo hatokuamini kamwe.chamsingi endelea na maisha yako kwa muda utapata mwingine.pia utakapo pata mwingine uchunge ulimi wako.kwani "usitumie matofali na misumari ya nyumba ya zamani kujenga nyumba mpya"hope umenipata
Kwa maana hiyo mkuu hawezi kukubali kuwa na mimi tena? maana lengo si kumwacha lakini ikinibidi nitafanya hivo kwa kufuata ushauri wa wanaJF baadhi.
 
Bonny

JF-Expert Member
Feb 21, 2013
13,274
2,000
Kama ulikua mwanaume kamili ukamfata ukamtongoza akakubali
Bas kua mwanaume kamili kumuacha aende zake sa hvi kuomba omba sana msamaha kuna shusha hadhi ya kiume
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom